Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,493
Siku za hivi karibuni kumekuwa na matumizi ya maneno hayo kuwa tunafanya jambo fulani kwa "maslahi ya Taifa" au watu fulani hawakufanya jambo fulani kwa "maslahi ya Taifa" n.k Kilele cha matumizi ya neno hilo ni madai ya Machunde wakati wa kujitoa kwenye Kamati ya Madini kuwa "wote tunajali maslahi ya Taifa" na hivyo isionekane kuwa wapinzani peke yao ndio walinzi wa haya "maslahi ya Taifa".
Sasa nimebakia najiuliza maswali kadhaa kuhusu hili dubwasha linaloitwa "maslahi ya Taifa" na majibu yake yatanisaidia kuandika makala yangu ya Jumatano. Na kama kawaida nayakaribisha mawazo yenu kwenu ninayo majibu yangu kuhusu maswali haya ila ningefurahi kujua majibu yenu kwani vichwa vingi ni bora kuliko kimoja (in certain cases anyway).
a. Maslahi ya Taifa ni nini?
b. Tunaweza kutambua vipi kitu au jambo fulani ni la maslahi ya Taifa?
c. Je maslahi ya Taifa yaweza kuwa sawa na maslahi ya kundi fulani la watu?
d. Je tunaweza kuhakikisha vipi kuwa watawala wanafanya mambo kwa maslahi ya Taifa?
e. Je mtu aweza kuwa mzalendo wa kweli bila kuweka mbele maslahi ya Taifa?
f. Je maslahi ya Taifa yakitishiwa ni jukumu la nani kuyalinda?
g. Je maslahi ya Taifa ni kitu kile kile na Taifa la Maslahi?
h. Je mtu anaweza kufanya kazi au utumishi wa umma au binafsi bila kujali maslahi ya Taifa na akawa mtumishi mzuri?