Msukuma Original
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 928
- 3,330
Maslahi ya kisiasa kwa kikundi kidogo cha CCM sio sawa. Taifa hili limejaa watu wenye uhitaji. Hizi propaganda za kutuaminisha kuwa Tanzania haina uhitaji wa misaada ilihali uhalisia wa raia wa Tanzania wanahihitaji hii misaada sio sawa hata kidogo. Viongozi acheni kuwadhulumu watanzania kwa maslahi yenu ya kisiasa. Hawa watu ndio mnaodai mpo kwa ajili ya maendeleo yao. Maslahi yenu ya kisiasa yasiwe maumivu kwa raia wa nchi hii.