Maskini wanapata wakati mgumu toka wanazaliwa mpaka milele wakiwa huko Jehanamu

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Fikiria mtu anazaliwa huku mama yake akisimangwa.anazaliwa katika wakati mgumu toka day one anasikia tu maneno ya kukatisha tamaa anakua katika mazingira magumu Sinza, Kijitonyama, Mwananyamala, Magomeni, Mwenge na maeneo mengine ya kipato cha chini.

Hewa ni ya kugombania jinsi kulivyoshonana.anayopumua mwingine wewe ndiyo unavuta, ukitoa naye anavuta.

Unaishi chakula cha shida milo mitatu tu kwa siku, tena chakula kilekile, afya ya mwili na akili itatoka wapi? Shule unaenda kufundishwa na walimu wamekata tamaa wanafundisha kitu ambacho hata wao hawakiamini.

Mimi nmesoma kwa wazungu huko; munapelekwa maabara, munapelekwa vituo vya sayansi, unakutana na akina Bill Gates wanakwambia How to Do Business. Na wanaeleweka, siyo habari zenu za sijui majini n.k

Huyu anakuwa mtu mzima, kupata demu tu nako ni kwa mateso sana. Akipata kirahisi ni wale mademu wa mkate kichwa, hawana mvuto. Mtu anakunja sura kama anakamuliwa jipu, lazima azeeke mapema. Na utamu wa love making unakosekana. Wengine hawacome, si kwa sababu wana nguvu sana, laaah! sababu hawafeel.

Maskini huyu hapa duniani anaishi kwa shida. Bado unakuta haendi mbinguni, anaenda motoni. Yaani anakuwa ni mtu wa kupata shida tu kotekote. Duniani hatakiwi na mbinguni hatakiwi. Anaishia jehanamu.

Maskini anaanza chomwa moto toka yupo duniani kwa namna ambavyo anapata shida na mateso. Wakati fulani nawaonea huruma sana. Unamwona mtu anaishi kwa shida, bado hataki kuwa mtu mwema. Hivyo anateseka hapa na huko kwingine anaenda kuteseka mara nyingi zaidi.

Nikawaza lile joto la huku Dar kama mtu usipowasha AC si ndo kama la jehanamu, nashangaa wanasema huko kuna moto mkali sijui mara 7 ya huu wa huku.

Ni bora basi uishi kwa starehe huku duniani ili hata ukienda huko ukapelekwa jehanamu uwe unasema "daaah lakini duniani nili-enjoy wacha tu nichomwe" Ukicheck pembeni wapo na wengine ambao duniani walikuwa jehanamu na huku kwingine wapo jehanamu. Hatari sana.

Tuchukie umaskini na pia tuache kutenda dhambi.
 
"Tuchukie umaskini na pia tuache kutenda dhambi "Nimependa kauli yako hiyo tu ndugu,ila hivyo vingine umeviandika katika muktadha ambao sio sahihi sana,ungeweza kuiweka mada yako katika muktadha mzuri usionekanike kwa jicho baya lenye ubaguzi,dharau na tabaka.Ni mtizamo wangu tu binadamu mwenzangu.
 
mkuu jehanamu siyo pa mchezo mchezo, utatamani maisha aliyoishi huyo maskini. rejea kisa cha lazaro na yule tajiri...
 
Luka 6:24-26

Lakini ole wenu nyinyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu. Ole wenu nyinyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu nyinyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia. Ole wenu nyinyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipofika mahali fulani ikabidi nirudu kuangalia mleta mada..kumbe Ni KIDUKU LILO, ikabidi niache tu

Kizibo
 
Back
Top Bottom