Embu tupe data kidogo Mkuu...sijui km namfaham sana so far as navyojua ni mwanamama aggressive aliyetumia kalamu yake vizuri kuiibia serikali!...sina hakika na kumbu kumbu zangu!
Kuna watu mmekula chumvi humu duh.... skendo za tangu 1980's bado mnazikumbuka tu.
Hii thread itatuonyesha under ages ni akina nani humu JF
Kwa hiyo humjui ATHUMANI MAUMBA wa 1987 pale mnazi mmoja?....fataki la wakati huo kaka
Hakufanya jema mkulu , huyu mama alikuwa mwizi,aliiba, aliiba fedha nyingi, alikuwa pale NBC Foreign branch sasa hivi ni makao makuu ya NMB Post mpya.Alishirikiana na kijana mmoja wa kiarabu jina lake nimesahau kigodo.Back then ilikuwa fedha nyingi approximately 60ml
.. kwanini tulikuwa very serious wakati ule..? Leo kuna mama mwingine anatuhumiwa kuiba bilioni 1.3 na hakuna watu wanaoshtuka!
HAKUNA jinsi ungeacha kumchukia maana alifanya kitu cha ajabu kinyume na mtu wa kawaida...ni kama leo usikie jirani yako kamchinja mwanaye kama kuku!mimi binafsi nilimchukulia Sara Martin Simbaulanga kama mtu hatari sana hasa ukizingatia magazeti ya wakati ule yalivyokuwa yakiripoti habari ile. .
Toroha hakuwa mume wa Sra bali mshkaji tu,.. mumewe ama walitengana au kuachanaMkuu Heshima yako,
Una kumbukumbu nzuri sana juu ya kesi ile, Sara na mumewe Toroha walitoka nadhani kwa msamaha wa rais, walikuwa wanaishi kule Kawe Mzimuni, mumewe nadhani alifariki kama sikosei mwaka juzi.
Huyo jamaa ndio alimponza Sara kama leo akina papa Msofe wanavyojua kuwavuta karibu wale wanaojua watawasaidia kukamilisha deals.Mkaka alicheza na saikolojia ya Sara tu ... kumwona ana matatizo ya ndoa hivyo akijifanya anampenda kumbe ana ajenda yake.Nakumbuka kama huyu mama alikuwa na uhusiano na Jamaa fulani ambaye alimpa yale madola.
Haswa! SARA alikuwa kiwezesho tu!Mastermind alikuwa marehemu TOROHA MOHAMED TOROHA huyu mama alikuwa 'inside person'
Haikuwa genuine love bali opportunity kwa mkaka Toroha! Ndio tatizo la kuingia kwenye mapenzi ukiwa na matatizo.Huwezi kufikiria vizuri na hapo ndipo unajikuta umeruka majivu ukakanyaga moto!Wengi walichosahau ni the love story behind yule mdada aisee..
Kwa hiyo humjui ATHUMANI MAUMBA wa 1987 pale mnazi mmoja?....fataki la wakati huo kaka