Maskini RFA, ndiyo kwaheri hivyo

Inasikitisha sana, mimi bado nasikiliza watanzania tuongee magazeti, nayo mara matangazo yakatike, yaani ni shida, radio ilikuwa ya mfano hii jamani kwa vipindi vyake vya kueleimisha
hata mm ila kulingana na shughuli za kimaisha niliamia mikoa ambayo RFA haipatikan moja kwa moja ikabidi nitumie APP yao, lakin bado ni chenga..
 
Huyu Charles Machugu akiwa anatangaza habari Star TV ninaacha kuangali, jamaa anambwembwe za ajabu sana, ana cheza na macho, pua nyusi haa..mimi amenishinda kabisa.
Mie niliisha ingia hadi studio siku hiyo alikuwa anatangaza kipindi cha Mambo Mambo. Anaboa sana.
 
Satr TV kwenye ufundi wapo chini sana, mfano habari inapotangazwa tukio likioneshwa hawaoneshi mzungumzaji ni nani, yaani wao wakisha ongea wanaachia tukio sub tille kuonesha nani mzungumzaji wa tukio hakuna, hili si poa inatakiwa kuwe na taarifa za mzungumzaji wakati tukio linarushwa.
 
Inasikitisha sana... nakumbuka enzi nikiwa kachalii nilivipenda vipindi vya RFA kama vile Sindano 5 za moto by Fred Waa, Show time, Weekend Fever, Search Line, Je wajua? na Michezo.
Ukisikia Neeeeews ..sauti za watangaza news zilikuwa nzuri na makini sana...
God!
Umesahau kipindi cha Sitasahau
 
RFA ilikuwa moto sana miaka ya 2000's , kipindi hicho nakua, kulikuwa na vipindi Kama, search line - rahabu fred, uliza ujibiwe - Raruan mhuza, sitosahau - Fredrick bundala, tamaduni zetu - wambura mtani michezo Steve moyo mchongi n.k.

Pole zao r.i.p
 
4. Michael Noel
5. Alicia Evance
Awa na wale wengine wanabaki kwa kukosa work proposal kutoka kwingine au wameombwa na bodi ya Sahara media wasiondoke ikawa haibu?

Na au watalindwa kwa hali na mali wasikose mshahara ili mradi safari iendelee..
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Eheheheee nakumbuka kipindi niko shule nilituma maoni yangu ya kuponda msanii flan kwenye kipindi cha Showtime kipindi hicho kuna sauti nzuri ya Mtoto wa Mama Sabuni karibu shule nzima hadi baadhi ya Walimu waliniuliza nimewezaje kutuma ujumbe hadi ukasomwa...
 
Enzi za R.F.A

Mtangazaji: unaitwa nani
Mwili obare:naitwa Mwili obare kutoka musoma Mara
Mtangazaji: mwili obare

Naaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaammm

Yani jamaa alitika mpaka radio Betri zikaisha.
 
Wenzetu kumbe bado mnasikilizaga hawa watu mimi siku hizi nasikilizia na kuangalia vyombo vya nje! Nikichoka naenda kuangalia Simba wanavyotafuna nyumbu Safari Chanell!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
RFA Bonanza kwa hewa.
Naiskiliza on the daladala.......
89.3Fm Dar
89.0 Fm Arusha.
 
Ni kweli kuna shda, mimi naisikiliza kila siku asubuhi BBC na magazeti, siku hizi inapiga sana muziki, wanatangaza live vipindi vichache sana..wanaweka miziki tu, na matangazo yamekuwa ya kusua sua mfano hayo magazeti asubuhi..jana jioni kweli wakati DW ikitangaza imelia sana ule mlio wa kuunganisha ikiwa inataka kuunganisha BBC jioni, mpaka nikakumbuka miaka ya 90's tukisikiliza hizo sauti za kuunga radio kwa Short Wave (SW)..

Hakuna watangazaji vijana wenye morali na walio updated..yaani imekosa mvuto kabisaa na ipo ukingoni, zama zake zimekwisha.. Kiss FM ndio sijui hata ipoje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom