Maskini rais wanguuu...

Status
Not open for further replies.
Sasa mnataka mpaka waseme live kuwa nyie wajinga si watakosa ulaji? wameamua kufikisha ujumbe kijanja
 
Kuna haja ya kuajiri wasaidizi wa rais kutoka nje hahahahahaha, au tusubiri tamko rasmi la serikali kwamba kuonyesha cheque hiyo ni kuatarisha amani na utulivu na kuifanya serikali ya CCM isiweze kutekeleza sera zake barabara.mwaka huu tutaona mengi
 
Nadhani hao jamaa waliandika makusudi ili kuona kama watanzania tuko serious na misaada ya fedha tunayopewa na wametupata. Inawezekana jamaa walikuwa wanamfanya rais kituko, na majira wamefanya hivyo hivyo.
 
I think the Wazungu huwa wanatumana kujaribu uelewa wa excutives wetu kuona kama wanaweza kushtukia vitu. Isije ikawa hawa jamaa wanajiandaa kusaini mkataba wana test zali kwanza.

Hilo zungu pembeni ya JK nafikiri lilikuwa linachekelea moyoni, yaani bango limepita kwa watendaji wote hadi kwa Rais bila kustukiwa.

JK aanze kuelewa hana timu makini, amezungukwa na waganga njaa. kinachofuata watamtia gundi machoni badala ya mchnga.

Hii ni ngumu kabisa
 
Hiyo hundi ni ya EXIM BANK (!!!).

Hivyo ni wao waliyoiandika. Hii inaweza kutupa picha of how serious is this bank in managing our mfuko wa pembejeo.
 
Majira_09_Oct_07.JPG

The message is self explanatory! Nothing more nothing less! Kuna mwenye kujua nini namaanisha? Kazi ipo... Ni kutoka gazeti la Majira la leo Oktoba 9, 2007

Jamani hapa nilipo sina mbavu yaani hata kahawa yangu imemwagika watu wakinisikia watasema nimechanganyikiwa. Nilikuwa sijaona hii thread kuifungua tuu ni kituko. Ipo siku watu watavaa nguo ya ndani juu ya suti. Hili jambo si la kucheka bali ni la kuhurumiwa maana ni kiboko au kali ya mwaka. Nimeamua niprint kabisa hata hii picha nitaiweka kwenye kumbu kumbu zangu za maisha. Duh yaani watu wote hawakuona?

Nani anajua sitory ya mfalume juha alipotoka uchi watu wakashangilia akafikiria kavaa vizuri?
 
Hiyo hundi ni ya EXIM BANK (!!!).

Hivyo ni wao waliyoiandika. Hii inaweza kutupa picha of how serious is this bank in managing our mfuko wa pembejeo.

Bank wanatoa hundi lakini hawaandiki wao. Wenye makosa ni World Bank ambao waliandika hiyo hundi na watu wa JK ambao hawakuweza kuona kosa. Walikuwa wanafurahia jinsi picha itakavyotoka vizuri kwenye magazeti, ni USANII ule ule.
 
I mean't dola laki tatu... nafikiri si sahihi na kusema ni sawa na zaidi ya shilingi milioni mia nne.. nadhani ingekuwa sahihi angalau wangesema Ni chini kidogo ya shilingi milioni mia nne za madafu...
 
inawezekana kulikuwa na cheki mbili... Yaani Exim wametoa 500,000 kwa maana Scholarship fund iende 300,000 na hizo 200,000 ziwe ni za mazabe... sema muandaaji wa hiyo chakula alikuwa anatetemeka akaibua hadharani!!

Nakuunga mkono. au pia jamaa wasidizi wamepanic kwa jinsi mambo yalivyo kweupe hivi sasa kiasi hata kazi hawawezi thena kufanya.

Kitu unafanyiwa tu, hata kuona pia huwezi, hata mikataba wanasaini hivihivi wakiamini imeshaandaliwa na kumbe nao mianya ya makosa inapotokea. What a shame!
 
Bank wanatoa hundi lakini hawaandiki wao. Wenye makosa ni World Bank ambao waliandika hiyo hundi na watu wa JK ambao hawakuweza kuona kosa. Walikuwa wanafurahia jinsi picha itakavyotoka vizuri kwenye magazeti, ni USANII ule ule.

Hawa jamaa hawakuwa na nia ya kutoa hiyo pesa bali wametoa ili kuona umakini wa wakuu wa nchi kufuatia mfululizo wa mi scandal ndani ya GOVT. sasa nadhani wameprove kuwa hakuna umakini kabisaaa!!!!!!
 
Bado mi sijaamini macho yangu, yaani hata hao wa Majira walikimbia iweka gazetini hawakuona? hii ni aibu tena Muungwana anatia dole kabisa mwendo mdundo!! kweli hapa ni mdundiko tu!
 
I mean't dola laki tatu... nafikiri si sahihi na kusema ni sawa na zaidi ya shilingi milioni mia nne.. nadhani ingekuwa sahihi angalau wangesema Ni chini kidogo ya shilingi milioni mia nne za madafu...

Ndio mkuu nimekuelewa hapo ni kuongeza zero tatu tuu amayo kama ulivyosema ni chini ya sana ya hiyo pesa uliyosemsema
 
Bado mi sijaamini macho yangu, yaani hata hao wa Majira walikimbia iweka gazetini hawakuona? hii ni aibu tena Muungwana anatia dole kabisa mwendo mdundo!! kweli hapa ni mdundiko tu!

Inawezekana Majira waliiweka makusudi tuu ili kuwaumbua.
 
I mean't dola laki tatu... nafikiri si sahihi na kusema ni sawa na zaidi ya shilingi milioni mia nne.. nadhani ingekuwa sahihi angalau wangesema Ni chini kidogo ya shilingi milioni mia nne za madafu...

Mwanakijiji,

Kama unafuatilia magazeti ya Tanzania kwenye numbers ni mbumbumbu kweli kweli. Mara nyingi wanapoandika namba huwa wanafanya makosa.

Alasiri ndio kabisa yaani huwa hawajui kujumlisha.

Nafiriki editorial standards zetu ziko chini sana. Hakuna watu wengi wa kuhakiki na kuhakikisha walichoandika ni sahihi.

Kosa kama hili la hundi ya JK ingelikuwa huku majuu kuna jamaa wangepoteza kazi lakini kwa TZ itaishia kuwa karaha tu na hakuna litakalotokea.

Pia Mwandishi wa majira kashindwa kuona hii ni habari muhimu mno. Kaandika kama hakuna tatizo. Hiyo mimi ningeiita failure of perception, yaani hata kama waliona hayo makosa, haikuwaingia kichwani kwamba hii inaweza kuwa big story, that is an opportunity lost kwa gazeti la majira lakini mafanikio kwa JF.
 
Sidhani kama huyo mzungu hakuona, tena ni worlbank tukumbuke. Hawa jamaa wameamua kutest zali kwa kikwenga. Duh ni kama kuvuliwa nguo ukweni. kweli nchi hii inatisha
 
Kumbe maimuna wako hadi kwenye tarakimu sio!
Kwani haiwezekani kuandika hiyo hundi kwa kiswahili?
Watu bwana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom