Maskini mwenzenu heslb yasababisha kuua baba yangu na mama yangu

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Aug 19, 2012
145
28
Kwanza kabisa nawaombeni msamaha wana jamii wote wapenda amani kwa kitendo changu cha kuwaua kinadharia wazazi wangu hali wangali wazima. nililazimika kufanya hivyo ili niweze kupata mkopo asilimia mia kwani hali za wazazi wangu ni dhoofili bin taabani hivyo nilichangamka na nikasajili vifo vya wazazi wangu na kupata death certificate toka RITA ili hali wenyewe wangali hai mpaka sasa na hivi ninavyoongea niko mwaka wa pili chuo kikuu kimojawapo hapa nchini napata mkopo asilimia mia na masomo na maisha yangu pamoja na wazazi wangu yanaenda vizuri kwani nikipata boom langu huwa nakata fungu nalituma kwa wazazi wangu ingawa kwa upande wa pili nikifikiria huwa na simanzi na huzuni. wana jf naombeni ushauri kwa kile nilichokifanya nawakilisha.
 
Hii mambo ulikubaliana na wazazi wako..au ulijiamulia mwenyewe bila kuwashirikisha....so sad kwa ulichofanya.
 
Tubu kwa Mungu wako kwanza maana ulianza kumuongopea yeye kisha ukawaongopea hlesb.
 
Dah:)kweli maisha ni matatizo kila siku,hivi Kwanini usiwaambie Wazazi kuhusu hilo jambo ili wake wakifahamu kinachoendelea kwa sababu baadae hisije ikakutokea Puani.
 
Dah:)kweli maisha ni matatizo kila siku,hivi Kwanini usiwaambie Wazazi kuhusu hilo jambo ili wake wakifahamu kinachoendelea kwa sababu baadae hisije ikakutokea Puani.

tubu kulingana na imani yako alafu ukimaliza masomo yako waeleze wazazi ulichokifanya
 
Maisha ya Mtanzania kila kukicha heri ya jana,Pole kwa mkasa mzima najua ulifanya hivo ili ujikwamue shuleni,OMBA MSAMAHA MAPEEMA
 
Dah:)kweli maisha ni matatizo kila siku,hivi Kwanini usiwaambie Wazazi kuhusu hilo jambo ili wake wakifahamu kinachoendelea kwa sababu baadae hisije ikakutokea Puani.
mkuu ndio maana nimeleta kwa wana jf nipate great advice zenu.
 
wewe ni mjinga, unadhani jmforums inatazamwa na members only! Mpaka sasa u're wanted by police.
 
Kukaa kwako kimya kutakupelekea kupata laana ni vema ukawaomba msamaa wazazi wako afu usiludie tena ush****zi huo
 
Khaa! wewe unaombaje ushauri wakati upo tayari mwaka wa pili kwa hiyo mbinu yako?
Je wengi wakikupinga, wakisema umefanya vibaya! utaacha chuo? Utajisalimisha?
 
Khaa! wewe unaombaje ushauri wakati upo tayari mwaka wa pili kwa hiyo mbinu yako?
Je wengi wakikupinga, wakisema umefanya vibaya! utaacha chuo? Utajisalimisha?

mkali naomba ujue kuwa si kila ushauri unafanyiwa kazi lkn nitajitahidi kwa yale ya busara kuyafanyia kazi
 
mi naamin ulikua unamaana kufanya hivyo kwaiyo kitu kitakachofata ni kumaliza chuo na kuwaeleza wazazi hope watakuelewa tu kama kweli walikwambia hawawezi afford chuo expensise huwa wanasema 'succes need sucrifice and things you ever do'
 
Umetenda dhambi mbele ya Mungu na Wazazi wako. Kama wewe ni mkristo,amri ya nne ya Mungu inasema "Waheshimu baba na mama yako upate miaka mingi na heri duniani" tafadhali chukua muda,ongea na wazazi wako,waeleze ukweli na uwaombe msamaha. Wakikusamehe,nenda mbele ya Mungu kadiri ya imani yako,utubu na kuomba msamaha,naamini Mungu wetu aliye mwingi wa rehema atakusamehe. Amini tu na ufanye hivyo.
 
Back
Top Bottom