Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,201
- 10,938
Maskini Karamagi
2007-11-09 18:07:28
Na Emmanuel Lengwa, Dodoma
Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Nazir Karamagi amerushiwa kombora lingine zito, akidaiwa kuwa baadhi ya kampuni zilizopewa leseni ya utafutaji madini nchini, zimekuwa zikijihusisha na uchimbaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi.
Aliyemkalia kooni Mhe. Karamagi safari hii, ni mwanachama mwenzie wa CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Msalala Mheshimiwa Ezekiel Maige.
Mhe. Maige amerusha kombora hilo wakati akiuliza swali Bungeni.
Akadai Kampuni ya Barrick Exploration Afrika Limited yenye leseni ya kutafuta madini katika eneo la Mwazimba, imekuwa ikichichimba dhahabu na kuonekana ikisafirisha madini hayo kutoka Mwazimba kwenda Mwanza na hatimaye nje ya nchi.
`Mheshimiwa Spika, kampuni iliyopewa leseni ya kutafuta madini katika eneo la Mwazimba imekuwa ikijihusisha na uchimbaji na pia imeonekana ikisafirisha dhahabu kwenda Mwanza...nadhani hapa tunastahili kupewa maelezo ya kina iweje kampuni hizi zichimbe madini wakati leseni zake ni za utafutaji,` akasema Mhe. Maige.
Hata hivyo akijibu tuhuma hizo, Mhehimiwa Karamagi amesema kampuni zilizopewa leseni ya utafutaji wa madini, kisheria haziruhusiwi kuchimba madini hayo.
Akasema endapo kampuni inayotafuta madini inafanikiwa kugundua au kupata madini katika eneo fulani, inalazimika kutuma maombi ya leseni ya kuchimba.
Akafafanua kuwa baada ya kutumwa kwa maombi hayo mkataba mpya wa uchimbaji huandaliwa na kutiliana saini na Serikali, kabla ya kuanza kazi ya uchimbaji.
Aidha akasema kama kampuni hiyo inajihusisha na uchimbaji wa madini, ni kinyume cha sheria na leseni waliyonayo na kuwa taarifa zipelekwe haraka kwa maofisa madini wa Mkoa, ili kampuni hiyo ichukuliwe hatua.
`Kama kampuni inayotafuta madini Mwazimba inachimba, taarifa zipelekwe kwa maofisa wa madini, tutawachukulia hatua na kuwafutia leseni,` akasema Mhe. Karamagi.
Awali katika swali lake la msingi, Mheshimiwa Maige alihoji kampuni gani zenye leseni za kutafuta madini katika maeneo ya Kaole (Nyangalagata), Nyamakwenge, Mwazimba, Malito na Masabi katika jimbo la Msalala.
Akijibu swali hilo, Bw. Karamagi alisema kampuni zenye leseni katika jimbo la Msalala ni pamoja na kampuni ya Pangea Minerals Ltd iliyo katika eneo la Nyangalagata, Tanzam 2000 na Northern Mining and Consulting zenye leseni katika eneo la Nyamakwenge na Barrick Exploration Afrika Ltd yenye leseni katika eneo la Mwazimba.
Nyingine ni kampuni ya Pine wood Resources Ltd yenye leseni katika eneo la Malito na Misolele na National Mineral Development Corporatio,MDC ya India yenye leseni ya maombi ya utafutaji wa madini katika eneo la Masabi.
SOURCE: Alasiri
Mwaka wa shetani kwa waziri wetu.
Sasa hivi aliyerusha kombora sio Zitto, ni mwa sisiemu mwenzake.
Haya sasa, na huyu naye wamwite mpinzani.
Tarishi hauwawi.