Maskini ACT Wazalendo, KAMPENI ZAO HOI KWA KUKOSA FEDHA

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Anna-24Sept2015.png

Mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.

Wakati zikiwa zimebaki siku 30 kuelekea uchaguzi mkuu, kampeni za mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira zinakabiliwa na uhaba wa fedha ambazo sasa zimebaki Sh. milioni mbili tu.


Tangu mgombea huyo alipozindua kampeni zake Agosti 30, mwaka huu hadi sasa, chama hicho kimeshatumia Sh. milioni 363 ambazo ni wastani wa takribani Sh. milioni 15 kwa siku.

Lakini kutokana na ukata unaokikabili, kwa sasa kinalazimika kutumia Sh.66,667 kwa siku.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa ACT-Wazalendo, Nixon Tugara, jana aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kutokana na changamoto wanayokabiliana nayo ya uhaba wa fedha anatoa wito kwa Watanzania popote walipo kuchangia kampeni za chama hicho.

“Mtu anaweza kutoa kiasi chochote na tutashukuru sana kwa ushirikiano wa kuijenga Tanzania yenye misingi ya haki...chama chetu kinakabiliwa na wakati mgumu kifedha, tumekuwa tukijitahidi kuzunguka sana kutafuta fedha kwa marafiki zetu na kuchangishana miongoni mwa wanachama lakini hatujafikia lengo letu la kiwango tunachohitaji cha fedha za kufanya kampeni bora,” alisema Tugara.

Hata hivyo, Tugara alisema licha ya changamoto hiyo ya kifedha, ACT-Wazalendo wataendelea kufanya kampeni za kistaarabu katika kipindi kilichosalia kabla ya uchaguzi.

“ACT-Wazalendo ni chama cha hoja, tutaendelea kujikita katika kujenga hoja na si mbwembwe na ulaghai kama ambavyo vyama vingine vimekuwa vikifanya,” alisema. Tugara na kuwa lengo la chama hicho ni kuwafikia wapigakura wengi ili kuwashawishi kwa sera kuwachagua wagombea wao kwenye sanduku la kura ili warudishe misingi iliyoasisi taifa.


CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom