Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,606
- 696,727
Ukila na kipofu usimshike mkono, wahenga walisema!
Zimebakia dakika chache kumaliza siku hii ya Jumamosi. Kwa wale wenzetu wanao abudu siku hii. Ndio wanamalizia Sabato yao. Kwa wasijua ni kwamba kila siku ya wiki ni siku ya ibada kwa imani fulani, kwa hapa kwetu maarufu ni:
Ijumaa - Waislam
Jumamosi - Wasabato
Jumapili - Wakristo wa madhehebu mengine kama Wapentekoste, RC, Protestant, Anglican na haya makanisa ya kiroho ya mitume na manabii.
Kesho tunahitimisha siku tatu zilizotolewa na mkuu wa nchi za kufanya maombi nchi nzima kuomba kwa Mwenyezi Mungu atupunguzie na kutuondoshea kabisa hili balaa.
Makanisa yale ya kiroho ya mitume na manabii na vituo vya maombi na maombezi ghafla wakalipokea hili la maombi kwa mikono miwili na kwa kasi ya ajabu wakaanza kutangaza ratiba zao kwa kisingizio cha kumuunga mkono mkuu wa nchi kwenye maombezi.
Sina tatizo na hilo hata kidogo. Shida yangu ni moja kwao. Sikuona hata mmoja aliyehimiza waumini kufuata tahadhari za afya ikiwemo kuvaa barakoa kanisani na kuwa mbalimbali kwa mita walau moja. Waliojitahidi sana waliweka ndoo za maji na sabuni huko makanisani, ghafla waumini wote wakapona na kusahau matatizo yao mengine yote ya kiafya na kimaisha.
Hata mapepo na majini yalionekana kugwaya. Hakuna kuanguka tena wala kushuhudia uponyaji. Wote ni maombi ya Corona. Safi kabisa.
Sasa ndugu zangu hawa niwakumbushe jambo moja muhimu sana. Wamuunge mkuu wa nchi kwenye hili la michango pia. Wengi wenu mko vizuri kifedha na inajulikana wazi ni mojawapo ya watu wanaokula bata sana. Wengi wenu mko kwenye orodha mitume na manabii matajiri wenye ukwasi wa kutisha.
Onesheni utu wenu sasa. Rudisheni percent kwa jamii.
Breweries wametoa
Vodacom wametoa
Wafanyabiashara wametoa
Taasisi mbalimbali zimetoa
Watu mbalimbali wametoa
Nyie mmenyuti kimya kabisa
Ikiwapendeza kesho. Sadaka za kesho zote kusanyeni zikawe mchango wenu kwenye mapambano dhidi ya Corona. Msiwakamue waumini wenu kwa kutangaza sadaka maalum ya Corona.. Lock down inakuja WAHURUMIENI.
Tengenezeni kolabo kama zile mnapokuwa na majanga ya kufumaniwa na kuibiwa sadaka mlizoficha majumbani mwenu.. Mtoe zile za bank zikawe mchango wenu. Punguzeni uchoyo na rohombaya mkatoe sasa kumbukeni ni kwa kutoa ndio mtapokea. Mkishindwa hili baada ya Corona sijui mtaweka wapi nyuso zenyu.
Jr