Karishia Mbarikiwa
Member
- Aug 1, 2017
- 7
- 5
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, ni namna magari almaarufu kama EICHER yanayofanya kazi katika viunga mbalimbali vya maeneo ya mijini na vijiji. Imekua kero kubwa kutokana na kelele za honi zao ambazo ni kero kutokana na kelele zake pale tuu inavyopigwa.
Nitoe mfano wa hivi majuzi nlikiwa maeneo ya posta mpya hapa mjini Dsm ilitokea basi moja ya aina ya EICHER ilipiga honi nkiwa nimesimama pembeni na mzee wa makamo ilitushtua sana. Mzee yule alishtuka mpaka kupelekea kukaa chini huku mapigo ya moyo yakimwenda mbio sana. Ilinibidi kumnunulia maji ili mwili kukaa sawa. Na hii sio mara ya kwanza kwa madereva wa magari hayo pindi tuu wanapokua wakiingia kwenye vituo vya mabasi hupiga honi hizo pasipo kua na ulazima wowote ile.
Rai yangu ni kwa mamlaka husika kuchukua hatua stahiki juu ya wamiliki wa vyombo hvyo kuangalia nmna nyingine ya kubadilisha honi hzo na kuweka zitakazo kua za kistaarabu au ikiwezekana ziwekwe honi za kawaida ambazo hazitapelekea watu kushtuka ama sivyo zinaweza kuleta madhara makubwa maana watu wengi wanamagonjwa ambayo hayaitaji kelele za kiasi kile. Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app