figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,486
Heshima kwenu wakuu,
Jeshi la Polisi la Tanzania ni jeshi moja linalofanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu ikiwemo kutimiza majukumu yake ya Ulinzi wa raia na mali zao japo bado kuna changamoto ila Polisi wanajitahidi sana.
Huo ulikuwa ni Utangulizi, kilichofanya niandike hapa, ni hali ya baadhi ya wanasiasa kutukatisha Morali ya kazi na kutufanya tujione wanyonge. Wakati nipo kwenye mwendo kasi Kimara to kivukoni, nmesikia Malalamiko ya watu nahisi walikuwa ni Maasikari Polisi.
Leo kulikuwa na Semina Elekezi kwa Maofisa wa ngazi za juu wa Polisi wote Tanzania ambayo ilikuwa ifanyike Mjini Dodoma. Na hii ipo katika ratiba ya Mwaka sio kwamba imeshitukizwa na Bank ya NMB ilikuwa ishatoa udhamini kwa shughuli hii, kilichonisikitisha ni Stop order iliotolewa masaa machache kabla ya Semina kuanza kwamba kila mtu arudi kwenye kituo chake cha kazi.
Wengine walikuwa washafika Dodoma mfano watu wa Mtwara, Kagera Zanzibar. Wengine walikuwa njiani wakielekea Dodoma.
Huu ni Usumbufu sana, kwanini hawakusema mapema hadi tumeharibu nauli na muda wetu? Hii imenisikitisha sana.
Hata hivyo Kazi zitaendelea kama kawaida.
Nasikia kuna Malalamiko kwamba kuna mtu anauliza kwanini makamishina wa Polisi ni wengi sana?
Hii inachanganya sana.
=======
Je hii ina Ukweli? Nmewaonea huruma sana. Poleni wakuuu
Eti Waziri Mwiguli ndo alitakiwa awe Mgeni rasmi.