thnx bro hao ccbt wapo wapi?
HABARI ndugu zangu mimi ninamatatizo ya kusikia ngoma zimepasuka nimehangaika sana kutafuta tiba lakini wapi.ninamshukuru mungu wakati nimeanza kuugua nilikuwa kidogo ninapesa hivyo nilizunguka sana katika hospitali zote kubwa na ndogo,sikuwa na shida na pesa ila shida yangu ilikuwakupona masikio lakini hamna kitu mpaka nikaamua kununua mashine ya masikio. sasa je ninaweza nikaja nikasikia tena ?au ndo SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA? nipeni data wazee.
dr 4ne hawajamaa ngoja niwatafute nitakufahamisha.
Mkuu NA Mimi nilipata ukiziwi kutokana NA sababu ya kuugua Malaria Kali na kupigwa dawa ya QUUININE na nilishawahi kupewa machine za usikivu lkn kwa BAHATI mbaya zilinisaidia kusikia SAUTI tu na sio kuelewa kwahiyo niliacha kuzitumia sababu tatizo lilionekana ni NEVA/mfumo Wa fahamu na sasa naendelea kupambana na maisha name nishaizoea hali hii na kujikubalikaka nguvuri3 kwanza nashukuru kwa kunifariji pili kwa ushauri wako juu ya kuonana na mabingwa .mkuu pia umesema Ningependa kufahamu sababu zilizopelekea masiko yako kutoboka. Je umewahi kuwaona wataalam wakathibitisha kuwa ngoma zimetoboka? [ Eardrum perforation].Pili unapotumia mashine unazosema, je hali inakuwaje katika usikivu. mkuu mimi ninahisi sababu zinaweza kuwa mbili kuu 1 nimewahi kufanya kazi kwenye mazingira ya kelele kama driller sehemu ambayo ilikuwa inalipua miamba kwa baruti 2niliwahi kuugua TB ambapo madaktari hawakuishitukia mapema wakawa wananitibu maralia kwakuwa sasa sikuwa napata nafuu waliamua kunichoma quinini ambazo ndo ziliniziba masikio hivyo nikawa sisikii tena. kuhusu mabingwa wa masikio nimeonana nao zaidi ya watano .bugando mmoja,muhimbili mmoja,ekenwa dispnsr mmoja,murugwanza mmoja,kahama hospital mmoja (huyu alikuja toka kenya) kifupi wote walikuwa wananipa moyo sana na nilijitahidi mno kuhudhulia kiliniki. vipimo vyao vilionyesha kwamba ngoma zimetoboka na sikio la kushoto linasikia kwa 20% huku jingine linasikia kwa 10%ningekuwa mtoto mdogo wangenipasua kisha wazibe ila kwa kuwa mimi ni mtu mzima haita saidia.wakanipa mfano mtu mzima akivunjika mguu kuunga huwa ni kazi ngumu sana. kuhusu hii mashine ninayoitumia nashukuru inanisaidia ila wakati mwingine huwa inazimika tu nakaa hata siku tatu siendi kazini kwakuwa sisikii na kazi zangu ni za ufundi hivyo wateja wangu ili wakupe kazi mpaka msikilizane mkubaliane. mashine yenyewe inauzwa bei ghari sana hivyo kumudu kununua mashine ingine kama spea ni kazi. kumbuka ni miaka mitatu tu iliyo pita tangu nipate tatizo hili. nashukuru kwa kunisoma.
Mkuu jisikie kawaida tu ila hata Mimi mwanzo ilikuwa hivyo lkn kwa sasa ni muda mrefu tangu nipate hilo tatizo na nimesoma Shule na chuo drs la kawaida tu..nilikaza hivyohivyo na kufanikiwa kuhitimu vizuri tunashukuru sana mkuu, ndugu usiombe hili tatizo limpate mtu ukubwani afu awe hana pesa ya kununua hiyo mashine.nikikumbuka mimi ilivyo nikuta nusu nife kwa mawazo nikakonda sana maana duniani nilikuwa najiona nipo peke yangu sina wakuongea nae hata ile lugha ya viziwi siifaham yaani nikajikuta nawachukia watu wote maana nilikuwa nikiwaona wanaongea nahisi wananiteta mimi.