Masikio yangu yote yametoboka ngoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikio yangu yote yametoboka ngoma

Discussion in 'JF Doctor' started by Slave, Jan 4, 2011.

 1. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  HABARI ndugu zangu mimi ninamatatizo ya kusikia ngoma zimepasuka nimehangaika sana kutafuta tiba lakini wapi.ninamshukuru mungu wakati nimeanza kuugua nilikuwa kidogo ninapesa hivyo nilizunguka sana katika hospitali zote kubwa na ndogo,sikuwa na shida na pesa ila shida yangu ilikuwakupona masikio lakini hamna kitu mpaka nikaamua kununua mashine ya masikio. sasa je ninaweza nikaja nikasikia tena ?au ndo SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA? nipeni data wazee.
   
 2. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  pole mkuu. Nashangaa kina mzizi mkavu hawajaibuka kutoa maelezo ya kukusaidia
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nashukuru bro.kwani mzizi mkavu anakujaga na huku?maana huwa namuona sana kwenye jukwaa la sayansi na teknojia. Naomba utengeze link ili aje humu nae amwage mautaalam.
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote pole sana kwa matatizo. Ningependa kufahamu sababu zilizopelekea masiko yako kutoboka. Je umewahi kuwaona wataalam wakathibitisha kuwa ngoma zimetoboka? [ Eardrum perforation].Pili unapotumia mashine unazosema, je hali inakuwaje katika usikivu.
  Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha ngoma kupasuka ikiwa ni pamoja na Ear infection au Physical damage inayoweza kupasua ngoma, hii ni pamoja na kuingiza vitu ndani ya sikio, au ajali n.k.
  Lakini pia inaweza kuwa kulikuwa na sababu za kimaumbile [in born] ambazo hazikuwa bayana kwa nyakati fulani na kadri siku zinavyosonga ndipo dalili zinavyojiopnyesha.
  Kwa vile unatumia mashine na kupata usikivu, na kwa vile bado unasikia kwa msaada huo, si rahisi kujua kiwango cha uharibifu wa ngoma. Kwa mantiki hiyo ni kwa vipimo vya kitaalam ndivyo vinaweza thibitisha hatima ya sikio lako. Ningekushauri ukaonane na Daktari bingwa wa maradhi ya masikio, pua na koo [ENT SPECIALIST], Huyu atatoa msaada wa hatima ya masikio yako.
  Usikate tamaa bado kuna nafasi ya marekebisho, lakini kumbuka kumuona ENT Specialist kwa msaada zaidi.
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kaka nguvuri3 kwanza nashukuru kwa kunifariji pili kwa ushauri wako juu ya kuonana na mabingwa .mkuu pia umesema Ningependa kufahamu sababu zilizopelekea masiko yako kutoboka. Je umewahi kuwaona wataalam wakathibitisha kuwa ngoma zimetoboka? [ Eardrum perforation].Pili unapotumia mashine unazosema, je hali inakuwaje katika usikivu. mkuu mimi ninahisi sababu zinaweza kuwa mbili kuu 1 nimewahi kufanya kazi kwenye mazingira ya kelele kama driller sehemu ambayo ilikuwa inalipua miamba kwa baruti 2niliwahi kuugua TB ambapo madaktari hawakuishitukia mapema wakawa wananitibu maralia kwakuwa sasa sikuwa napata nafuu waliamua kunichoma quinini ambazo ndo ziliniziba masikio hivyo nikawa sisikii tena. kuhusu mabingwa wa masikio nimeonana nao zaidi ya watano .bugando mmoja,muhimbili mmoja,ekenwa dispnsr mmoja,murugwanza mmoja,kahama hospital mmoja (huyu alikuja toka kenya) kifupi wote walikuwa wananipa moyo sana na nilijitahidi mno kuhudhulia kiliniki. vipimo vyao vilionyesha kwamba ngoma zimetoboka na sikio la kushoto linasikia kwa 20% huku jingine linasikia kwa 10%ningekuwa mtoto mdogo wangenipasua kisha wazibe ila kwa kuwa mimi ni mtu mzima haita saidia.wakanipa mfano mtu mzima akivunjika mguu kuunga huwa ni kazi ngumu sana. kuhusu hii mashine ninayoitumia nashukuru inanisaidia ila wakati mwingine huwa inazimika tu nakaa hata siku tatu siendi kazini kwakuwa sisikii na kazi zangu ni za ufundi hivyo wateja wangu ili wakupe kazi mpaka msikilizane mkubaliane. mashine yenyewe inauzwa bei ghari sana hivyo kumudu kununua mashine ingine kama spea ni kazi. kumbuka ni miaka mitatu tu iliyo pita tangu nipate tatizo hili. nashukuru kwa kunisoma.
   
 6. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pole sana Mungu Yupo utapata ufumbuzi. tunakuombea.
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nashukuru sana mkuu, ndugu usiombe hili tatizo limpate mtu ukubwani afu awe hana pesa ya kununua hiyo mashine.nikikumbuka mimi ilivyo nikuta nusu nife kwa mawazo nikakonda sana maana duniani nilikuwa najiona nipo peke yangu sina wakuongea nae hata ile lugha ya viziwi siifaham yaani nikajikuta nawachukia watu wote maana nilikuwa nikiwaona wanaongea nahisi wananiteta mimi.
   
 8. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
  pole mkuu ni chalange za maisha... ingawa mimi c mtaalam wa mambo hayo ila naamini iko siku utakuja sikia... pengine kuna ukungu tu au (mwangi) ndani ya sikio lako
   
 9. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nashukuru mkuu ila sio ukungu kwani wataalam karibu wote nilio wataja hapo juu waedhibitisha kwamba ngoma zimepasuka
   
 10. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamani pole sana, unahitaji vifaa maalumu vya kusikilizia,
  je kule ulikopata tatizo hili hukuwa na medical insurance ? Ok kama hakuna

  Ungeweza ku claim permanent disability na kulipwa kiasi fulani cha hela ambacho kingekuwezesha kumiliki mashine, unajaza workmen's compensation injury form na kama injury uliipatia kazini, kwa sheria mpya ya kazi unastahili kulipwa unless kama ulikuwa umejiajiri, bado hujachelewa.
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mzizimkavu humu ndio kwake uko kwingine anaforce tu
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu pole sana, usikate tamaa kaka endelea kuwaona wataalamu kila utakapo sikia wapo.
  ccbrt nahisi pia wanao wataalamu hilo tatizo, kama vipi ukipata muda jaribu kuwaona
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mkuu kwanza pole. Ila sasa umesema source yaweza kuwa kelele,lakini ulipochoma quinine ndo yakazidi. Kama source imekuwa accelerated na quinine,utapona japo baada ya muda mrefu. Otherwise sina utalaam wa kukupa zaidi ya kukushauri ukae sehemu tulivu mda mrefu. Kama ni quinine utapona na nadhani kama ni tatizo la kupasuka kabisa hapo pagumu! Ila eardrum ikipasuka huwezi sikia 20%. Hapa ni tatizo linaloweza kutibika ,meanwhile ntamtafuta mtu anaemjua mtaalam yuko bunju dsm ni bingwa wa ajabu!ngoja nimsake alaf ntakupa jawabu. Ukiona kimya naomba uniPM ili nikumbuke mkuu. Wish u fast recovery!
   
 14. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  thnx bro hao ccbt wapo wapi?
   
 15. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nashukuru. Ukweli hili tatizo limekuja nitokea hivi karibuni.wakati nilikwisha acha kazi muda mrefu.isitoshe tangu mwaka 92 -98 nilikuwa nimekwisha pitia makampuni zaidi ya 6.
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nashukuru kweli hilo neno challenge ndo lilo nifanya nikasimama imara nakujiona sina tatizo baada ya kugundua kwamba kuna watu wanamatatizo zaidi yangu.
   
 17. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mkuu dr4ne mtafute mzizi mkavu nahitaji mawazo yake.
   
 18. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mkuu dr4ne mtafute mzizi mkavu nahitaji mawazo yake.
   
 19. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kaka ninashuru na nita shukuru zaidi nitakapo pata maelezo ya dr nanitakukumbusha kwa kuku pm nikiona kimya.
   
 20. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mkuu dr4ne mtafute mzizi mkavu nahitaji mawazo yake.
   
Loading...