Masikini wasipewe vibali kujenga mjini. Huchafua miji na vijumba vyao

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,045
50,980
Habari Wakuu!

Kama kichwa kinavyoeleza hapo, ingawaje Masikini naye mtu japokuwa hana kitu lakini hatuwezi kuukataa ukweli kuwa Masikini ndio mashetani yanayoishi na kuonekana live kwa macho yetu wenyewe.

Kuna watu hapa watasema nawasema vibaya MASIKINI, wengine watasema najisikia, nawadharau na kuwatolea maneno makali hao Masikini. Lakini nataka kusema hapa mimi mwenyewe ni masikini, hivi mambo niyasemayo hapa yananihusu hata Mimi.
Sisi masikini ni mashetani tunaoishi live katika macho ya nyama.

Tatizo la miji kuwa michafu, na watu kujenga pasipo mpangilio linasababishwa na Masikini. Unajua masikini ni mashetani hivyo hawanaga mipangilio, wapo rafu wanajenga hovyo hovyo.

Kama ingekuwa amri yangu, masikini leo hii wasingepewa ruhusa/kibali kujenga kwenye miji na majiji makubwa. Wakaishi huko porini huko kwenye mashamba wakalime.

Serikali kama inataka miji ijengwe kwa mpangilio mzuri basi lazima litolewe tamko kuwa Masikini hawatapewa kibali cha kujenga mijini, na mtu yeyote anayetaka kujenga nyumba mjini anapaswa awe na kiasi cha pesa kisichopungua milioni 50.

Masikini wawekewe sheria kali zitakazowabana ili wasilete ushetani wao Duniani.

Kama wanataka kuishi mjini basi serikali ijenge nyumba za kupanga, au mashirika na makampuni ndio yafanye kazi hiyo kujenga Apartments ili hao masikini wapange.

Matajiri sina neno nao, nafahamu wao wanamuwakilisha Mungu kwani Mungu ni tajiri, ndio maana matajiri hujenga na kuweka mambo/vitu vyao katika mpangilio mzuri.

Miji yote iliyotekwa na masikini lazima iwe michafu inayonuka, vijumba vimejengwa hovyo hovyo Kama takataka.

Masikini wajengewe miji Yao huko nje kabisa ya miji au maporini huko wakae wenyewe, au Kama wanataka kuishi mjini basi wapangishe nyumba zilizojengwa na serikali au matajiri.

Sitaki kuzungumzua habari ya machinga jinsi wanavyovuruga miji na kusababisha uchafu wakaapo barabarani.

Niishie hapa Masikini wenzangu wasije nipiga mawe, najua wataniona lakini ukweli nimewapa, wengine watanichukia lakini hilo halinipi shida kwani mashetani ni kawaida Yao kuwa na chuki.

Mashetani yakikupenda jua ni Kwa unafiki na yanakitu yanakihitaji kutoka kwako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dodoma
 
Tajiri wa mwaka 1970 aliyejenga mjini kati ndiye masikini wa leo hapo mjini kati na kijumba chake kinatakiwa kiondoke hapo kati...

Hata wale wanaojenga nje ya mji baada ya miaka kadhaa watajikuta wapo mjini kati, kama hawatoupdate nyumba zao ina maana mji utaonekana una masikini katikati ya mji.

Unforgettable


Watafukuzwa,
Kama wameshindwa ku-maintain wafukuzwe.
 
Andiko lina upumbavu mkuu na halina hekima hata kidogo.

Acha ngano na magugu vikue pamoja. Hivyo vijumba unavyoviona uchafu vitaondoka vyenyewe miaka kadhaa ijayo.


Masikini wasipoondolewa husababisha umasikini uote mizizi na kuathiri mazingira.

Wafukuzwe au Nyumba nzuri zijengwe wapangishe humo
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom