Masikini Tanzania

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Tanzania ni nchi iliyopo Afrika Mashari ikiwa ni nchi kubwa na yenye wakazi wengi kuliko nchi nyingine za ukanda wake kwa kuwa na eneo la kilomita za mraba 947,303 na wananchi wake wasiopungua 50,760,000. Eneo hilo la Tanzania lina jumuisha ardhi kubwa yenye rutuba ambayo ipo wazi bado(haijakaliwa na binadamu), yenye madini na vito vya thamani vya kila aina pamoja na gesi asilia, misitu minene iliyojaa miti imara, mbuga za wanyama wa kila aina, mito na maziwa makubwa duniani km vile Victoria na Tanganyika. Pamoja na majaliwa yote hayo ya Mwenyezi Mungu lakini bado wananchi wake ni masikini wanaishi chini ya dola moja.
Kutokana na Umasikini huo kila mmoja amekuwa akimtupia lawama mwenzie ndiye amehusika na hali hiyo. Wanasiasa wanatupiana lawama kwa hoja za aliyepo madarakani ndiye Chanzo cha hali hiyo hata km aliyepo ktk upinzani aliwahi kuwa madarakani hilo halijalishi. Je, tatizo ni nini kwa nchi hii iliyojaliwa na Mwenyezi Mungu?
Kwa mtazamo wangu nchi yetu hii imekwama ktk mambo mengi sana ambayo yametufanya tubaki kupiga kwata pale tulipo. Hebu tuangalie mambo haya kadha wa kadha;
1:SIASA; Ili nchi iendelee inahitaji ardhi, watu na uongozi bora. Ardhi tunayo tena yenye rutuba na na madini ya kila aina. Watu wapo ambao ni nguvu kazi, utawala bora ndilo limekuwa tatizo sugu katika nchi zetu za kiafrika.
Siasa ndiyo imekuwa sehemu pekee ya watu kujitajirisha hivyo kuondoa kabisa dhana ya utawala bora kutokana na wanasiasa kuwa wabinafsi wenye uchu wa madaraka, wasaliti wa wananchi wao kwa ajili ya maslahi yao. Hivyo mwananchi amebaki kuwa mtaji wa wanasiasa kwa maslahi yao.
2:ELIMU; Elimu yetu imekuwa ikionekana kujikita sana katika nadharia kwa muda mwingi kuliko vitendo hali ambayo inasababisha hata mhitimu wa Shahada ya Uzamili kuzunguka na vyeti vyake mtaani mchana kutwa bila kupata kazi kutokana na kutohusianisha elimu aliyoipata darasani na ulimwengu halisi. Elimu ambayo imekosa kumpa mhitimu ubunifu wa kupambana na mazingira tofauti na kuajiliwa tu.
3:WANANCHI WENYEWE: Kwa upande wetu wananchi tumeshindwa kutimiza wajibu wetu kuanzia kwenye sanduku la kura kwa kutochagua viongozi bora bali kuchagua viongozi kwa mihemko ya ushabiki wa kisiasa. Wananchi tumekuwa hatuwajibiki ipasavyo katika nafasi mbalimbali tunazozitumikia kwa wakati huo kama vile makazini watu wamekuwa wakifanya ili mradi liende mwisho wa mwezi nachukua changu. Hivyo uzalendo umepungua km si kukosekana kabisa.

Wadau km unanyongeza waweza ongeza.
 
tujilaumu sisi wenyewe kwa unafiki wetu maana kuna mijitu ni mijizi na bado tunaipa uongozi na baada ya muda tunaanza kulalama
 
tujilaumu sisi wenyewe kwa unafiki wetu maana kuna mijitu ni mijizi na bado tunaipa uongozi na baada ya muda tunaanza kulalama
Ndiyo huo ushabiki wa kisiasa ambao ni moja ya changamoto tulizo nazo!
 
UZALENDO wa kweli ndicho kinachokosekana na kulididimiza taifa letu. Neno uzalendo lilikuwa na uzito uliostahili katika katika awamu ya kwanza pale ambapo viongozi wa wakati huo chini ya Mwalimu Nyerere waliweka maslahi ya taifa mbele. Hata kama walikuwepo waliokuwa na tamaa zao walidhibitiwa na miiko ya uongozi. Miiko hiyo ilipoondolewa kwa kisingizio cha kwenda na wakati ndipo uzalendo ulipoanza kupotea. Matokeo yake in hii hali iliyopo nchini sasa.
 
Tatizo letu tunadanganyika sana wakati wa uchaguzi. Baada ya uchaguzi tunaanza kulalama.
 
Kuna mahali tulichezea mfumo wa elimu, sasa wale ambao walikuwa wanaandaliwa enzi hizo ndio hawa kwa sasa wapo maofisini, wakiwa na uzoefu wa miaka mitatu au minne ya kazi. Wanachangia sana katika kuthibitisha jinsi ambavyo kitaaluma tulivyo chini. Kila sekta inapwaya kwa sababu wasomi hao hao ambao walikuwa wakiimba "kama sisi wewe nyerere na uhuru tungepata wapi", lakini wanaimba maneno hayo wakishaishiwa fedha, zikiwepo ni kujirusha kwa kwenda mbele!. Aina hiyo ya wasomi kwa sasa wanazalisha madudu, walisoma ili wafaulu mitihani na baadae waweze kuajiriwa kumbe kuajiriwa ni kitu kimoja na kuweza kuongeza tija kwa yule aliyekuajiri ni suala jingine.
 
Na ndo maana wametuachia mfumo ule ule wa kusoma ufaulu mitihani uajiriwe. Bahati nzuri wakati wao ajira zilikuwa za kuchaguwa niende wapi niache wapi. Leo dunia imebadilika mfumo wa elimu ni ule ule, watu wanazunguka na vyeti mtaani no creativity!
 
Back
Top Bottom