Masikini Tanzania! Kwa sera hizi itagawanyika vipande vipande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masikini Tanzania! Kwa sera hizi itagawanyika vipande vipande

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amanibaraka, Apr 8, 2011.

 1. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nilikuwa namsikiliza Waziri kivuli wa sekta ya utamaduni Joseph Mbilinyi au Mr. 2 kupitia Chadema. Akiwasilisha kambi ya Upinzani anadai vyombo vya habari viruhusiwe kutangaza kilugha. Msikilize mwenyewe katika link hii hapo chini:
  Hivi jamani sera hizo zikitekelezwa hautokuwa mwanzo wa fujo?
  Tunao uwezo wa ku monitor hizo radio, Tv na magazeti yote kuhakikisha hazichochei vurugu za kikabila na kidini? Jamani tuwe waangalifu katika mambo haya.

  Kwa kweli mimi naogopa hasa nikikumbuka sera zile za majimbo ambazo nazo zilipigiwa debe sana na wapinzani. Eee Mungu inusuru Tanzania yetu yetu ambayo haina spea.

  YouTube - Mbeya urban MP Joseph Mbilinyi speaks in parliament for first time (Michuzi Blog)
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Je wajua kuwa Radio Terati ya kule Simanjaro hurusha matangazo kwa lugha ya Kimasai??
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mtu mwenyewe kivuli sasa unategemea ataongea nini kwa wasiokuwa vivuli?
   
 4. f

  fumbe free New Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba twende tukasome kwanza mapendezekezo yote yaliyotolewa na msemaji mkuu wa kambi ya upinzani mr two juu ya mswada ule wa unesco then turud tujadili kwa kina zaid juu ya pendekezo la kutumia lugha za makabla ktk tv na radio statn sio una jaji kwa point moja tu ya lugha wakat hata ule mswada wa uhfadhi wa tamadaun zinazoshkika na zisizoshkika au hata mswada wenyewe ulikuwa huujui? omba tukutumie na ufunguke
   
 5. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani ifikie wakati tuache kupinga kila jambo na kuchukua misimama tofauti kisa tu sisi ni wapinzani. No matter what, hili la kuhimiza radio za kikabila ni hatari kwa umoja wa nchi.
   
 6. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Amezungumzia mambo mengi yanayohusiana na kuhifadhi utamaduni na sio lugha peke yake...Hata kwenye suala la lugha amesema kuwepo na matangazo kwa lugha za makabila mbali mbali lakini kwa usimamizi wa karibu wa serikali, kwa hili hakuna ubaya hata kidogo.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  haya ndo madhara ya kufikiria kutumia makalio. hata kama kasema mazuri basi hili baya limefunikwa? hivi wewe unajia madhara ya hili analoliongea? Tz kuna makabila zaidi ya 120 hebu jiulize hivi leo tukienda huko tunatafuta nini kama ni yale ya wahutu na watutsi. hebu tuondolee haya mawazo yako ya chooni hapa. usitetee kila kitu tu hata kama ni pumba kwa sababu aliyesema ni waChadema. tunaelekea pabaya hapa. kama unamapenzi sana kwa huyo sugu wako basi kaa kimya kuliko kutuandukia utumbu humu.
  wewe unajua kabisa bado tunatibu majiraha tuliyonayo tangu uhuru halafu unataka kuanzisha lingine? inaudhi sana.
   
 8. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hili ni jambo la maana sana, unajua kuna lugha nyingi sana za asili zimekufa, na nyingine zina wasemaje 200 tu waliobaki, lugha ni utamaduni wa mtu hivyo tunapoteza urithi wa taifa, hili swala la kuogopa ukabila ni jinsi unavyofirkiri tu, kuna nchi kama india, south africa uswis, congo, zina makabila na wametunza ligha zao ila hawana ukabila, ukabila na udini ni ufinyu wa kufikiri, na stereotype, huna haja ya kuogopa, tanzania haikuwapo kabla ya makabila iweje leo imekuja tanzani na makabila yakafutika.
  Yaani lugha moja ya watu wa mashariki mwa nchi yaani kiswahili ilichukuliwa na kufanywa lugha ya wote halafu zingine zikaonekana ni ukabila , then huo ndio uzalendo mbona kituko.

  Nawapongeza sana UNESCO na hatua hii, lazima tukubali asili yetu kama huna asili basi itafute, sio kuiogopa.
   
 9. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mdau , huwezi kukataa asili yako, usifikiria kama wazungu ambao wanaona utamaduni wetu ni ushenzi, ukweli ni kuwa hakuna kitu cha kujivunia kama lugha, hivi sasa utamaduni wa mtanzani umetawaliwa na asili ya dini za kuletwa na hili ni janga la taifa, tukiwa kama taifa moja tumetoka katika sehemu mbali mbali hata kiswahili chetu kinatofautina sana sasa hiyo tuu haiwezi kuepusha kuficha asili yetu mimi naunga mkono kutunza lugha zetu za asili, usiunganishe hili na ukabila ukabila ni ufunyu wa kufikiri, huwezi kupinga kitu kwa kuogopa kulizungumzia bali kwa kuto hoja
   
 10. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haina maana kuchukua cha mtu na kujivunia kama chako halafu uite ni uzalendo(mfano kiingereza na kiswahili), wengi wetu kiswahili ni lugha ya pili kama kiingereza sasa kiswahili pia si ilikuwa lugha ya waswahili. Tunapoteza utajiri mkubwa sana wa lugha zetu za asili. Tanzani ilikuta haya makabila na mwisho tanzania itapotea na itaacha haya makabila hivyo hakuna haja ya kuficha asili yetu
   
 11. d

  drgeorge Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuache ushabiki, ni sawa kuna haja ya kuusoma na kuuelewa mswada, ila suala la vyombo vya habari kutangaza kimila, labda kama ni matangazo ya biashara au elimu fulani lakini wakati uo huo yakiwepo matangazo hayo hayo kwa kiswahili. Kutangazia kabila fulani tu siungi mkono haifai. Na DSM iwepo redio inayotangaza kizaramo?
   
 12. papaa-H

  papaa-H Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama hizo lugha zitatufanya kuwa watanzania basi ni vizuri tuzitumie ILA KAMA ZITATUFANYA TUGAWANYIKE NA KUJIITA CC WACHAGGA NA WAO WAPARE AU WALE WAZIGUA BASI TUOGOPE HILI AZIMIO KAMA EBOLA coz we are no longer going to have the tz we used to have. We have to be very careful c kwa sababu tu unesco wamesema basi ni jambo zuri. if we allow it we should first hav a way of monitoring them
  .......Nawasilisha.......
   
 13. F

  Fenento JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa ujumla sikubaliani na hili la matumizi ya lugha za makabila kwenye vyombo vya habari. Najivunia kuwa Mngoni na naongea kingoni inanitosha lakini pia najivua kuwa na Lugha yangu ya Kiswahili kama lugha ya taifa yaani nikiwa Tanzania nitasema ni Mngoni wa Songea na kiwa nje ya nchi yangu nitasema ni Mtanzani na naongea kiswahili kama lugha yangu ya Taifa. Baba wa Taifa hili Mwl. J.K. Nyerere aliliona hili jambo ndiyo maana alizuia kwa nguvu zake zote. Lakini ebu tujalibu kuliangalia kwa umakini suala hili kwa vile tunayo mengi sana ya kufanya kwa upande wa utamaduni wetu.
   
 14. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaka hilo unaloongea ni stage ya juu sana ya uelewa wa wananchi katika nchi husika. Mfano wa Congo huwezi kuwa wa maana zzaidi maana hauna maslahi kwaTaifa. Tunacho kataa kwenye hili la ukabila au udini, ni ILE HALI YA MTU KUJIHALALISHA KUPITIA UDINI, UKABILA NI KITU KIBAYA SANA KWA UHAI WA TAIFA. Ila kama wananchi watakuwa wanaelewa maana halisi ya kutunza mila zetu, hilo unalolizungumza halitakuwa na shida. Usichulie kwamba UNESCO wamesema, eti na wewe unafuata kama walivyosema. UNESCO sio Mungu wa kutuongoza kwa kila kitu...maana nao pia maoni yao hayazingatii mazingira ya nchi husika.... Chukulia mfano masharti ya IMF na WB yanyohusu kukuza uchumi, sio applicable kwa kila nchi.... HAPA NATAKA KUKWAMBIA KUWA SIO KILA KITU WANCHOSEMA HAWA WANAJIITA (UNESCO, UN, IMF, WB) unatakiwa uyachulue kama yalivyo....lazima uangalie mazingira yetu..... (DONT COPY, PASTE NDUGU YANGU) NDO MAANA UMEPEWA AKILI YA KUFIKIRI NA KUAMUA, KULINGANA NA MAHITAJI YAKO, NA HASA KUANGALIA MAZINGIRA YAKO KWA WAKATI HUO
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mbona mmeingia kwenye mtego wa kujichukia wenyewe, ina maana babu yako alikuwa mjinga kutumia lugha yenu kwa mawasiliano, ongezeni kiwango cha uelewa endelevu kwa faida yenu binafsi
   
 16. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Narudia tena swali langu: Je wajua kuwa Radio Terati pale Simanjiro inarusha matangazo yake kwa lugha ya Kimasai?? Je kuna sheria inayoruhusu hilo?? Je serikali haijui?? Mimi nadhani kitu chochote kikifanywa kwa nia nzuri hakina matatizo!! Je wajua kuwa mpaka sasa kuna kazi inaendelea kuandika Agano jipya kwa lugha za kienyeji hapa Tanzania??
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..hata radio au gazeti la Kiswahili linaweza kuvuruga umoja na amani ya wa-Tanzania.

  ..kitakachovuruga amani na umoja ni content ya matangazo, lugha ni "vehicle" tu ya kuwasilisha ujumbe ambao unaweza kuwa mzuri au mbaya.
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Sugu wa CHADEMA amechemka sana, hasa anaposema ulaya kila nchi wana lugha moja na wanatofautiana kwa matamshi.Huyu sugu lazima awe anasoma historia ya mahala kabla hajaitolea mfano. Ulaya walikuwa na makabila yao karne hizo na waliyaua taratibu taratibu mpaka kufikia hapo walipo, kutambua hilo kwamba kulikuwepo makabila ndo huko anakokuita sugu kutamka maneno tofautitofauti.

  Leo hii, tukiua makabila yote na wote kuongea kiswahili hata baada ya miaka 2000 ijayo, utamshi na uzungumzaji wa kiswahili tutatofautiana kilingana na asili ya kilugha cha mahali hapo kama ilivyo huko ulaya.

  Malengo ya Nyerere ya kuanzisha vijijini vya ujamaa nafikiri yalikuwa na nia yakuunganisha watanzania wote na kuua kabisa makabilamakabila kitu ambacho binafsi nakubaliana 100% kuwa na mchakato wa kuua makabila yote.
   
 19. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Someni link hiy on European Charter for Regional or Minority Languages. Kwa wenzetu waliondelea lugha zao asili zimekufa sasa wanahangaika kupreserve hizo Lugha, kwani kunatatizo gani mtu akizitumia hizo Lugha au unataka zife kabisa haarafu baadaye tuje tuhangaike kuzitafuta?
  About the Charter
   
 20. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  About the Charter


  Ukisoma hiyo linki utajua kuwa wenzetu ulaya wanangaika kupreserve lugha zao za asili ambzo nyingi zimekufa au kumezwa na lugha zingine sisi mpaka baadaye sana ndio tuaamka usingizini. Kwa mawazo yaha watanzania wako tayari lugha za Kigeni zienezwe mpaka vijijini ila za asili hazina nafasi tena, kweli psycological colonialism in nguvu kuliko physical presence ya mtu mweupe
   
Loading...