Masikini Nape! CCM hawamwitaji tena Igunga

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,037
22,728
Kutoka Gazeti la MwanaHALISI - Sept 14, 2011

NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa hali si shwari tena. Wanaojiita waasisi wa "mpango wa chama wa kujivua gamba" wameanza kutuhumiana kukivuruga chama, imefahamika. Taarifa zinasema mlengwa mkuu wa kinachoitwa, "kukivuruga chama" ni Nape Nnauye, katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi.

Hatua ya Mukama inatokana na uamuzi wa CCM kumpigia magoti Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi wanaotakiwa kujiondoa ndani ya chama hicho. Wengine wanaotakiwa kuondoka ni Edward Lowassa na Andrew Chenge.

Kwa mujibu wa waliokaribu na Nape, safari ya kiongozi huyo mjini Igunga ililenga kuwatambia baadhi ya wapinzani wake wa kisiasa waliodai Rais Kikwete amempiga marufuku kukanyaga huko wakati huu wa kampeni.

Kuthibitisha madai hayo, Nape aliandika katika mtandao wa JamiiForum, mara baada ya tukio hilo la Igunga, "Mlisema chama kimempiga marufuku Nape kukanyaga Igunga, nikasema tusubiri. Leo, mmeona nilivyotinga Igunga…"

Kwa mujibu wa mashuhuda, mara baada ya Nape kutoka nyumbani kwa wazazi wa Peter Ezekiel, alikwenda moja kwa moja kwenye baa maarufu iitwayo The Peak, ambapo inadaiwa alinisurika kichapo kutoka kwa mmoja wa mabaunsa wa CCM.

Inadaiwa kijana huyo wa miraba minne aliyefahamika kwa jina moja la Shaban, ambaye inadaiwa ni kutoka kwa kundi la Rostam Aziz, mara baada ya kumuona Nape kwenye baa hiyo alifoka, "Wewe unatafuta nini hapa?"

Naye Nape akajibu, "Wewe unafahamu unaongea na nani?" Shaban akajibu, "Ndiyo. Nafahamu kwamba wewe ni Nape Nnauye."

Kauli hiyo ilianza kumfanya Nape anyong'onyee kidogo, lakini mtoa taarifa anasema alijipa nguvu na kusema, "…Nimekuja kikazi. Tupishe tunamazungumzo yetu."

Shaban aligoma kuondoka na kisha akasema, "…Ondoka hapa, vinginevyo tutakuonyesha. Umekuja kutuharibia uchaguzi siyo?"

Mara baada ya kauli hiyo, taarifa zinasema Nape aliondoka katika eneo hilo na kuingia kwenye gari lake haraka kuelekea Singida.

Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Igunga kwa nini anadhani amefanyiwa vurugu, Nape alisema, "Hakuna kitu. Nilikuwa napita njia tu."

Sokomoko hilo lilitinga hadi kwa viongozi wake wakuu wa chama, Mukama na Rais Kikwete. Inadaiwa mara baada ya kupata taarifa hizo, Mukama kwa hasira alihoji, "Nape kwa nini umekwenda Igunga?"

Alisema, "Umekatazwa na Kamati Kuu usiende Igunga, sasa mbona umekwenda?" Alipojaribu kujitetea kwamba alikwenda huko kuhani, Mukama alisema, "Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana, tafadhali usituharibie uchaguzi," Mukama anaripotiwa kufoka.

Kaazi kweli kweli..................
 
Mtu yeyote mwenye akili zake timamu Igunga akikipigia kura CCM hata baada ya kudhalilishwa kiasi cha KULALA NA MKE WAO WA NDOA hadharani, basi ni vema akaanza kujilaumu tu mwenyewe mapema maana watakachofanyiwa mara baada ya uchaguzi huo utakua hausemeki tena midomoni.

Chaguo ni lenu; kuwaenzi Vibaka na Wapiga Ramli au kutumia fursa hii kujikomboa wenyewe ki-uongozi hapo Igunga.
 
Aibu kwake hawezi kuja kujibu hoja hiyo maana anatakiwa azungumzie na Mcheba alieenda kubaka watu huko Igunga vijana wake watamshughulikia au ndo imetoka.
 
Kweli Nape ni Kilaza, alitumiwa akatumika sasa wanamwona kama mbwa. Hawezi onyesha hadharani jinsi alivyonyong'onyea lakini anaumia sana moyoni. Anajifanya kupokea kadi za wanachama wa vyama vya upinzani ila soon ataomba kuhifadhiwa Chadema.

Yaliyokuwa yanasemwa kwamba wao na Sitta wana mpango wa kuidhohofisha CCM kwa manufaa yao binafsi sasa yanamrudi kigeugeu huyu.
 
Maskini CCM, huna utashi tena! umebaki kuiibia nchi na kujibakiza madarakani kwa nguvu za dola! Ondoka tuachie nchi yetu ikiwa safi!
 
Mtu yeyote mwenye akili zake timamu Igunga akikipigia kura CCM hata baada ya kudhalilishwa kiasi cha KULALA NA MKE WAO WA NDOA hadharani, basi ni vema akaanza kujilaumu tu mwenyewe mapema maana watakachofanyiwa mara baada ya uchaguzi huo utakua hausemeki tena midomoni.

Chaguo ni lenu; kuwaenzi Vibaka na Wapiga Ramli au kutumia fursa hii kujikomboa wenyewe ki-uongozi hapo Igunga.

Mkuu nimependa maneno yako lakini kwanini husiende kuyaeneza Igunga Mkuu ili ujumbe ufike barabara.
 
Kwanini wasingempa kichapo uyo mjinga siasa hawezi anaganga njaa 2 kwa kuleta siasa za kibaguzi.
Oldonyo,

WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU.... SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...

MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI
 
....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI
Mafisadi wako chama gani vile? Ni wale wanaotakiwa kujivua gamba au?
 
inaelekea mukama alikuwa hamjui vizuri kijana wake.

Kutoka Mwanahalisi, September 14 - Alfred Lucas

NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa hali si shwari tena. Wanaojiita waasisi wa "mpango wa chama wa kujivua gamba" wameanza kutuhumiana kukivuruga chama, imefahamika...

.
"Mwiguru (Nchemba) anafanya kazi nzuri sana. Ameratibu mkutano huu vizuri. Kampeni zimekwenda vema. Ni kijana mwenye busara sana yule," ameeleza mtoa taarifa akimnukuu Mukama.

Kiherehere gani kilimpeleka Nape Igunga ?
 
MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACH WAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI

Haijalishi kuwa umeenda Igunga ama haujaenda. Hapa suala ni kwamba, ulizuiliwa kwenda Igunga na lile gamba kuu ccm ndo walilipigia magoti! Mbona unakwepa hoja wewe??? Unajisifu na vita dhidi ya mafisadi mbona ndo kwanza yanatamba ndani ya chama chako na wakati zile siku 90 zimeshaisha?

Aibu yako we mwenyewe Nnauye jr kwa kuamua kuuza utu wako kwa magamba!
 
WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU....

SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...
- C'moon bro for the last ten years unaweza kutuambia ulikuwa unafanya kazi gani zaidi ya siasa??????? - Huo mstari wa kuganga njaa siuungi mkono lakini hili la siasa kutokuwa ajira yako nadhani unatuongopea

MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA
Not everyone who challenges u au CCM ni magwanda, kifupi it's pple against CCM

MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA
Habari ya Nape kukatazwa kwenda Igunga iliandikwa kwenye magazeti chanzo kikiwa hukohuko kwenye NEC/CC ya CCM.
...MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA
Mkuu usiwasingizie JF hii imetolewa na MwanaHalisi, gazeti ambalo uko in records kuliita la udaku na kwamba hakuna mtu serious analisoma.

SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU
- Sasa hiyo ungemwambia huyo baunsa wakati ule

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA
- Ebanae wewe si ndiyo ulisema chama chenu huwa hakipeleki viongozi wa kitaifa kupiga kampeni kama vyama pinzani? Mbona unakula matapishi yako?????

...Mkuu kama kweli utaenda Igunga na kuhutubia mikutano ya kampeni ukaonekana kwenye Luninga naahidi $100 kupitia kwa invisible.

NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA
- Duh!!! Mkuu sasa yule fisadi wenu mkuu si ndiye alikuwa hai tebo wakati wa uzinduzi wa kampeni? Kumbuka ile siti ilikuwa ni yako
HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI
- Hawa unaowaita mafisadi na wewe ni mmojawapo wa wakuu wa chama kinachounda serikali mmewachukulia hatua gani????

Dogo inaonyesha umeshaanza kupoteza focus, maana ule moto wenu wa kujivua gamba nadhani ndiyo umeenda huo. Maana sijamsikia Kiongozi wa CCM yeyote huko Igunga akielezea ni namna gani CCM kilivyo chama bora na kwamba sasa kinajisafisha kwa kuvua magamba. Neno gamba vp nalo ni prohibited Igunga?

Ya mwisho, ni kaswali kafupi not meant to offend at all, una ID nyingine au zingine zaidi ya hii ya Nnauye Jr humu JF?
 
Oldonyo,

WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU.... SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...

MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI

Nakuonea huruma sana kwa mwenendo wako kwa sababu Marehemu baba yako alikuwa ni mtu mwenye uhakika sana. Nilikutana naye mara nyingi sana miaka ya sabini na themanini kwenye mikutano ya TANU na CCM akiwa na kinanda chake na kusema wapinga mapinduzi wote wageuke kuwa ng'ombe ili wanamapinduzi wawakamue maziwa.

Ni unfortunate kuwa kweli moto huzaa majivu; kwani umethibistisha tosha kuwa wewe ni majivu yatokanao na moto wa Kanali Nnauye, umegeuka kuwa ng'ombe ili wanapinduzi (na wapinga mapinduzi pia) wapate maziwa!!

Elimu yako inaonyesha kuwa walakini kiasi fulani.
 
very funny! nape, ungeachana na hii makitu! sasa rostam mlikua mnaangalianaje usoni? dd u have to 'explain' that u were just following instructions ama ilikuwaje?
 
Oldonyo,

WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU.... SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...

MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI

Ushauri binafsi NAPE ACHANA NA SIASA kama ulipata elimu nadhani ni vyema ukaendelea na taaluma yako. Majibu yako yanafanana sana na mwehu aliyepata nafuu.

Wewe ni katibu mwenezi wa chama tawala moja ya jukumu lako ni kuuza sera za chama chetu ili watanzania hasa vijana warudishe imani kwa chama chetu, wakati mwingine siamini kama ni wewe naona mtu anatumia jina lako kuingia ndani ya forum. Kama ni kweli umesoma basi hukuelewa ulichosoma. Tunategemea kijana kama wewe kusaidia kugeuza mwenendo wa chama chetu lakini wapi umegeuka kama hao wezi na walafi waliomo ndani ya NEC.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Oldonyo,

WAGANGA NJAA UNAWAJUA? MAANA HUMU NDANI KILA KITU NAPE ANAGANGA NJAA, KWA TAARIFA SINA NJAA KIASI HICHO, HATA NIKIKAA TU NIKAFANYA KAZI ZANGU MWENYEWE BADO NAWEZA ISHI TENA MAISHA MAZURI PENGINE KULIKO WENGI WANAONIKASHIFU HUMU NA KUDAI NAGANGA NJAA...... NIMEACHIWA URITHI NA MZEE NNAUYE SIO WA PESA BALI ELIMU TENA YAKUTOSHA TU.... SIASA KWANGU NAFANYA KAMA HOBI SI AJIRA HATA KIDOGO...

MAGWANDA WENGINE POLENI SANA SANA MAAANA HUMU MSIPOMTAJA NAPE WENGINE HAMLALI.... NIMEKWENDA IGUNGA TOFAUTI NA MLIVYOBWATA HUMU NAPE HAENDI IGUNGA....MKATUNGA STORI KAVAMIWA SIJUI NA BAUNSA SIJUI NA MAGWANDA, THUBUTU YAKE HAPA TUNGEKUWA TUKIZUNGUMZA MENGINE KABISA, KAMA ANGEPATIKANA HATA WA KUGUSHA KAMBA YA VIATU....

JUZI TU NILIKUWA IGUNGA, NA HIVI WIKI IJAYO NAKWENDA TENA IGUNGA....NAJUA KINACHOWAUMA NI KUINGIA KWANGU NA KUTOKA KWANGU BILA MAFISADI KUJUA, HILI NINAHAKIKA LINAWAPASUA KICHA SANA, NA BADO.... JAMBO ZURI NIMEFANIKIWA KUWANYIMA USINGIZI MAFISADI
Nape this post is rubbish, absolutely... utterly rubbish

How could jibu watu kama uko kanga moko laki si pesa???

Hao mafisadi ndio wenye jimbo na kwa taarifa yako tu, CCM sasa imekua kama Somalia... ni factions tu!!!! Kwahiyo Igunga sio ya kwako, Igunga na kundi jingine... HALAFU UNAJISIFIA ATI UMEINGIA IGUNGA NA KUTOKA BILA MAFISADI KUJUA KWAHIYO KINAWAUMA... Unanyatia jimbo??? and you still call yourself a leader??

Get a life Nape... acha siasa kapige piano kanisani Mungu akuokoe

SHAME ON YOU
 
Ni unfortunate kuwa kweli moto huzaa majivu; kwani umethibistisha tosha kuwa wewe ni majivu yatokanao na moto wa Kanali Nnauye, umegeuka kuwa ng'ombe ili wanapinduzi (na wapinga mapinduzi pia) wapate maziwa!!

Elimu yako inaonyesha kuwa walakini kiasi fulani.

the boy is a goner............
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom