ChizzoDrama
JF-Expert Member
- Sep 29, 2019
- 1,317
- 1,229
Hakika wahenga waliosema ukistaajabu ya Mussa hujayaona ya Filauni hawakukosea. Masikini kumfariji masikini mwenziye ni mara chache sana lakini masikini huyu huyu yupo tayari kupanda hata gari akatoe pole kwa tajiri fulani.
Haya tunayaona ,katika jamii tunazo toka mahala ambapo kuna matabaka ya walio na wasionacho
Hivi ulishawahi kuona msiba unapotokea katika nyumba ya kitajiri hapo mtaani kwenu? Jinsi watu wanavyo jihimu kuchotelea maji, kwenda mashineni, kubeba kuni na shughuli zinginezo hapo. Na wote hawa wanakuwa ni masikini kwa asilimia kubwa huku matajiri wengi wakisubiri muda fulani wa kuuaga mwilli ndiyo waje na kwenda kuzika shughuli iishe.
Tizama unapotokeà msiba kwenye nyumba ya hoehae kama huyo marehemu alikufa Saa 11
Basi balozi atazunguka kila nyumba kuamsha watu kuwa kuna jirani kafariki
Ili vijana wawahi kuchimba lakini kila nyumba atakayo gusa kijana anasema anaumwa
Akifika nyumba inayofuata wa nyumba ya nyuma utaskia "SIKUKUELEWA BALOZI NILIKUA USINGIZINI" Yaani watavutana mpaka basi
Masikini tunashindwa kujaliana sisi kwa sisi matajiri nao hawatujali ila tunalazimisha kuwajali wao (aibu hii) tubadilike
Masikini mwenzio anae kupa 1000 ukikosa unga na watoto ni wa maana kuliko, kuliko tajiri aliye tayari kukununulia pombe hata za laki na kisha uende zako