Masikini Haji Manara!

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
LILE sakata la tuhuma za utapeli linalomkabiri Katibu Mwenezi wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, leo limeingia katika hatua nyingine baada ya katibu huyo kupewa dhamana kisha ghafla kudakwa tena na polisi wa kituo kikuu jijini Dar es Salaam nje ya Mahakama ya Kinondoni. Kamanda huyo wa zamani wa CCM alidakwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni ambako anakabiliwa na kesi ya utapeli wa magari. Alikamatwa na askari watatu ambao walijitambulisha wanatoka kituo kikuu, walimwambia Haji kuwa ana tuhuma zingine nzito za utapeli wa magari mengine matano na shauri lake limefunguliwa katika kituo hicho.



1266935433_manara.jpg

Manara akiwa amezungukwa na askari kanzu wa kituo kikuu cha polisi mara baada ya kutoka mahakamani.

1266935433_manara_2.jpg

Manara akiwa chini ya ulinzi akielekezwa kuingia kwenye gari.

1266935433_manara3.jpg

Gari lililombeba Manara likiwa tayari kuondoka kuelekea kituo kikuu cha polisi.
 
Maskini Manara ananikumbusha baba yake tulivyokuwa tunamwita COMPUTER enzi hizo za Yanga ya miaka ya 70
 
mimi nashangaa sana Watanzania wenzangu ni nani alieturoga ? mbona tunahuruma sana, masikini Haji ? masikini wa nini.? sasa hata huyu Tapeli, tunamuhurumia.
Haji mwenyewe amekiri kua kajitia Aibu kubwa, yeye mwenyewe, fmilia yake, na hata chama chake cha majambazi oooh, sorry CHAMA CHA MAPINDUZI, aende akale maharage, iwe fundisho.
 
Da..
Hivi kwa nini hizo kesi wasingeziunganisha kwenye jalada moja?
Maana zinafanana
Sina uhakika kama watu wawili tofauti wakiwa wanamshitaki mtu mmoja kwa kosa linalofanana ni lazima waunganishe mashitaka kwenye jalada moja!!
 
Washikaji wake wa Saigon wameshindwa kumsaidia.

Ngongo, ukitaka kufahamu kama una marafiki wa kweli wewe patwa na tatizo ambalo linahitaji muda wao sana au kuzunguka buyu!!! Atakayesalia nawe hadi mwisho wa tatizo huyo ndiye rafiki wa kweli.

Tunajidanganya tunapokuwa na kipato una marafiki kibao, kwa kuwa mnaweza kutumbua pamoja wakati change zipo!!! Ngoja uonekane unafilisika kama hujaona kila mmoja akisepa taratibu!!! Waulize watu ambao walishavuma sana na utajiri au hela za mashaka halafu wakachinja uwaulize ni marafiki wa design gani na kiasi gani walikuwa nao awali na sasa wamebaki wangapi au kama hawajasepa wote na kupata wapya wa hali yake ya sasa!!!! Kuwa makini na marafiki zako!!!!!Usije ukafikiria kundi lako la kupigia ulabu na nyama choma na totoz basi ndiyo chanda na pete wako!!!! Thubutu!!
 
Kama ni tapeli anastahili huruma ya nini? Kweli watanzania mnabehave kama waumini wa Kakobe.......haya ndo mambo ya babu Seya, kaharibu watoto afu mnataka Mh.Rais amsamehe!!

Ukiishi kwa upanga ....utakula kwa upanga!!
 
Nilikuwa namuona haji mbali sana baada miaka 2 au 3 hv...hata ubunge angeweza kuja kupata au hata udiwani au hata ukuu wa wilaya....maana ana ujomba na mkuuluu wa kuutafutizaaaa...upooo
 
Hawa ndio sampuli ya vijana wa CCm; Haji anatapeli magari ya watu na wakina Nchimbi wanafanya utapeli/ufisadi wa elimu !! Hao ndio vijana mnaotaka kuwarithisha uongozi wa nchi sio? CCM mmefulia.
 
Ule msemo wa kisheria unaodai kuwa "mtuhumiwa hana hatia, mpaka pale mahakama itapomtia hatiani" unahitajika hapa.

Tuwaonee huruma waliotapeliwa kwa kiwango kile kile tunachohitajika kumwonea huruma aliyetuhumiwa.
 
hivi haji Manara sio yule mtoto wa sunday manara yule zeruzeru?samahani ninauliza tu kwa heri tu bila shari
 
Back
Top Bottom