jamadari
JF-Expert Member
- Feb 13, 2010
- 295
- 92
LILE sakata la tuhuma za utapeli linalomkabiri Katibu Mwenezi wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara, leo limeingia katika hatua nyingine baada ya katibu huyo kupewa dhamana kisha ghafla kudakwa tena na polisi wa kituo kikuu jijini Dar es Salaam nje ya Mahakama ya Kinondoni. Kamanda huyo wa zamani wa CCM alidakwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni ambako anakabiliwa na kesi ya utapeli wa magari. Alikamatwa na askari watatu ambao walijitambulisha wanatoka kituo kikuu, walimwambia Haji kuwa ana tuhuma zingine nzito za utapeli wa magari mengine matano na shauri lake limefunguliwa katika kituo hicho.
Manara akiwa amezungukwa na askari kanzu wa kituo kikuu cha polisi mara baada ya kutoka mahakamani.
Manara akiwa chini ya ulinzi akielekezwa kuingia kwenye gari.
Gari lililombeba Manara likiwa tayari kuondoka kuelekea kituo kikuu cha polisi.