Masihara Mengine Haya Yamevuka Mpaka Picha ya X-ray ikionyesha remote control ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masihara Mengine Haya Yamevuka Mpaka Picha ya X-ray ikionyesha remote control ndani

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Dec 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  Masihara Mengine Haya Yamevuka Mpaka
  [​IMG]
  Picha ya X-ray ikionyesha remote control ndani ya mwili wa mwanafunzi Huang Chen Friday, December 11, 2009 6:36 PM
  Mwanafunzi mmoja wa nchini China ambaye alikuwa amelewa chakari hajitambui alilazimika kuwahi mwenyewe hospitali baada ya pombe kuisha kufuatia kitendo cha marafiki zake kuizamisha remote ya Tv kwenye kiungo chake cha kutolea haja kubwa. Mwanafunzi Huang Chen mwenye umri wa miaka 19 aliamua kwenda hospitali baada ya kuhisi maumivu makali kwenye makalio yake kila alipojaribu kukaa.

  Pombe alizokunywa zikiwa bado hazijamtoka vizuri, Huang Chen aliwasili kwenye hospitali ya Hunan Hangtian Hospital katika mji wa Changsha akilalamika maumivu makali anayoyapata kwenye sehemu zake za nyuma.

  Wakati alipolazwa kitandani akifanyiwa uchunguzi na daktari, Huang aliwashangaza madaktari wakati alipojigeuza mwili wake na mara ghafla televisheni iliyopo kwenye wadi hiyo ilibadilika kwenda chaneli nyingine.

  Kwa uchunguzi zaidi, Huang alipigwa picha ya X-ray ambayo iliwashangaza madaktari walipoona remote control ya TV kwenye maeneo yake muhimu kwa kutolea uchafu mwilini.

  Polisi wa China walitoa taarifa kuwa Huang alfanyiwa masihara na marafiki zake anaokaa nao nyumba moja wakati alipolewa pombe na kushindwa kujitambua. Waliingiza remote control kwenye mwili wake kupitia sehemu zake za kutolea haja kubwa.

  Polisi hawakusema kama marafiki zake nao walikuwa wamelewa au la wakati walipokuwa wakifanya kitendo hicho.

  "Hatukujua tuanzie wapi, kulikuwa na damu damu kwenye sehemu zake za siri za nyuma lakini hakusema chochote kuhusiana na remote control. Hatukuamini macho yetu baada ya picha ya X-ray kuonyesha kilichotokea", alisema Dr Wei Lung Zhi.

  "Atapona kabisa baada ya kipindi cha muda mfupi lakini remote ya TV imeishaharibika kabisa, haifai", alisema alisema Dr Lung Zhi.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3729718&&Cat=2
   
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,740
  Likes Received: 8,335
  Trophy Points: 280
  Majuu hamnazo!
   
 3. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  masihara au ufirauni huo!!!!???
   
Loading...