Mashuka na neti kuwaka na kama kutoa miale ya moto hivi

Mimi inanitokea hata wakati navua tshirt, huwa zinatoka mwanga kabisa na sauti yake inafanana na makaa unavyo lia wakati unatoa cheche
 
Habari za mida hii!

Hii kitu huwa naiyona sana hasa usiku nikiwa nataka kulala kama kuna kigiza flani huwa naona kama nikisugua shuka au hata neti naona kuna miale kama vitu vinametameta kwenye mashuka,

Huwa najiuliza ni vitu gani vinavyowekwa kwenye mashuka na neti mpaka unaona zinameta na kutoa miale kama ya moto. Wadau mnijuze
Ni umeme huo unaotokana na msuguano wa vitu vitu viwili/ mada mbili. Hata ndege zinapokuwa zinasafiri angani, msuguano wa bodi na hewa huwa unasababisha kukusanyika umeme kwenye bodi ya ndege. Hata hivyo, umeme huo huwa unafyonzwa kitaalamu na kifaa kingineu kwenye bodi hiyo, vinginevyo karibia watu wote kwenye ndege wangekuwa wanakufa kwa kupigwa shoti ya umeme, pindi wanapotokea kugusana na bodi ya ndege inayosafiri angani. Hata baada ya kutua, umeme huo ungeendelea kuwepo kwenye bodi ya ndege
 
Back
Top Bottom