Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye, Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanaweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
Namkubali sana TAL.
 
Kama Magufuli angekwenda Mossad na FBI ili kujua mimi ni nani basi nasema alistahili kufa. He was a sinister...
IP yako inaweza kukutrace na kujua machine unayotumia, watu wakakudukua mafaili yako na credentials zako unazolog in sehemu mbalimbali wakakujua kuwa ni wewe.
Hizo software mashirika ya kijasusi kama FBI, Mossad wanazo
Wakikutaka kwa udi na uvumba wanakupata tu
 
Kulikuwa na vita Tanzania; Watanzania wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nae hakushinda, wala mahali pake hapakuonekana tena Tanzania.

Yule joka akatupwa hata kuzimu, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa amani, na haki, na umoja katika Tanzania.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hivi roho ya kumtoa mtu uhai unaitoa wapi?..kisa tu mtu anakukosoa upumbavu wako unaoufanya!!

TLissu ni namba nyingine..huyu ni shujaa aisee
 
Jamaa alikuwa shetani ktk umbo la mwanadamu. Yule wa Adam na Hawa alikuwa katika umbo la nyoka.
Hivi roho ya kumtoa mtu uhai unaitoa wapi?..kisa tu mtu anakukosoa upumbavu wako unaoufanya!!

TLissu ni namba nyingine..huyu ni shujaa aisee
 
wajukuu zetu watakapofika vyuoni watakuja kumtumia mwendazake kama sample au subject katika maandishi yao ya kitaaluma.

hakika yule hakuwa binadamu wa kawaida, ni shetani.

keep resting in hell jpm.
chunga kaul zako, ushetan wake ukowapi?? una ushahid na hayo maujinga yako
 
Waoga na w
Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye, Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanaweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
Waoga na wenye kujinyekeza kwa watawala kwaajili ya matumbo yao hukumu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto.
=> Tukipata watu hata elfu moja wenye kujielewa na kusimamia imani yao nzuri kwa ustawi wa taiga letu,hakika mama Tanzania atakuwa mbele mno kimaendeleo.
 
Kuna ndugu yangu ngosha mwenzangu PASCAL MAYALA yeye alipotishwa tuu from day one alipouliza swali akaambiwa kuwa 'anasumbuliwa na njaa kama tafasri ya jina lake' akanywea kabisaa akabadilika kuwa mtu wa kusifia tuu.Huyu jamaa ni mzuri sana kichwani ila Serikali hawajataka kumtumia ila siku wakiamua kumtumia , matokeo mazuri watayaona.He is mentally very smart ila uoga tu ndo unamharibia.
 
Angalau sisi tuko nyuma ya keyboard...
Kabisa, ila tukumbuke kwamba Maxence Melo kateswa sana na utawala uliopita. Alikua anashinda mahakamani kututetea na hizi FAKE ID, sirikali ilikua inataka ijue ni akina nani wanainanga hapa JF na kuweka document zake ambao ni CLASSIFIED. Amesimama kidete sana.
 
Kuna ndugu yangu ngosha mwenzangu PASCAL MAYALA yeye alipotishwa tuu from day one alipouliza swali akaambiwa kuwa 'anasumbuliwa na njaa kama tafasri ya jina lake' akanywea kabisaa akabadilika kuwa mtu wa kusifia tuu.Huyu jamaa ni mzuri sana kichwani ila Serikali hawajataka kumtumia ila siku wakiamua kumtumia , matokeo mazuri watayaona.He is mentally very smart ila uoga tu ndo unamharibia.
Kuhusu Pascal Mayala huyu mwana JF mwenzetu, wala usiwe na wasi wasi.. kamwe haiwezi kufika 2025 bila kupewa teuzi. Kwa sasa anatafutiwa sehem sahihi itakayomfaa kulingana na CV yake.
 
Unamkubali Kiongozi kwa Lipi Hasa ?

Unamkubali kwa haki au ni sababu ya zege na lami. Wengi sasa wanababaika wakisikia neno haki, katika kipindi hiki wanataharuki kama wameona shetani. Wakati haki ni kitu kizuri kinaleta Amani, furaha na kisha neema inafuta kwani Maendeleo ya Watu yatapatikana katika utulivu.
Source: Bishop Augustine Mpemba
 
Back
Top Bottom