Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Na. M. M. Mwanakijiji
Limetolewa pendekezo hapa kuwa mama Anna Killango Malecela ajitoe CCM kama yeye ni "mkweli". Lengo la hoja hiyo ni kuwa kwa vile CCM inaonekana wanampinga na yeye mama Malecela "alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!" (Jmushi) na zaidi ya yote ikatolewa hoja kuwa mama Killango afanye hivyo kwa kufuata mfano wa "MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm"
Ninachojaribu kuonesha hapa ni kuwa hoja ya kumtaka mama Killango ahame CCM kwa vile hawakubaliani naye au kwa vile anapata upinzani mkubwa haina msingi, haizingatii ukweli wa hali halisi, na endapo itazingatiwa itasababisha kufutika kwa kiasi kikubwa kwa mama Malecela katika siasa za Tanzania ingawa aweza kupata jina katika upinzani. Hata hivyo kuhama kwake kama haki ya kila raia kwawezekana kwa sababu za kwake yeye mwenyewe na uamuzi huo ni yeye aupime.
Lakini swali langu ambalo najaribu kulijibu ni kuwa je wale wanaopambana CCM na kukutana na upinzani mkubwa kama mama Malecela wakihame chama na kukimbilia kwingine? Je wote wanaopambana ndani ya CCM (akiwemo Anne Killango) watetemeke na kugwaya mbele ya NEC na chama chao wakizingatia ibara ya 15:1 ya Katiba ya CCM? Je wabunge wa CCM wangeamua kuipigia kura ya hapana Bajeti nini kingetokea?
Ndugu zangu mama Malecela na wengine ndani ya CCM wameamua kuchukua msimamo thabiti na dhahiri wa kukisafisha chama chao. Wamechukua msimamo wa kuonesha kuwa CCM haiwezi tena kuendelea kukumbatia mafisadi, kulinda wazembe au kuficha uchafu serikalini. Ni wazi kuwa msimamo huo ambao tumeuona kwa wabunge kadhaa sasa tangu mwezi ule wa Februari ni msimamo unaoweza kutishia maslahi ya watu wengi sana ndani ya chama hicho na nje yake.
Ni kwa sababu hiyo basi maneno yake kuhusu EPA kuwa kama maelezo hayataridhisha basi Bungeni patakuwa "hapatoshi" yalichukuliwa na baadhi ya wana CCM (kama Mhe. Anna Abdallah) kuwa ni changamoto kwa wabunge wengine. Ni mgongano ndani ya CCM na sasa kumtaka Anne Killango akimbie maana yake ni kuwa akubali kushindwa.
Endapo Anne Killango ataondoka kukimbia CCM atakuwa amekubali kushindwa mapambano ambano yeye mwenyewe ameamua kushiriki. Anayepambana na ambaye hajapima gharama ya mapambano hayo hafai kupambana. Maandiko matakatifu ya kikristu yanatolea mfano mmoja wa mtu ambaye aliamua kujenga mnara lakini kwa vile hakupima gharama yake alishindwa kuumalizia. Mama Killango kabla ya kuingia kwenye mapambano haya alijua kabisa kuwa nguvu anazoshindana nazo si kidogo. Hivyo akiamua kuondoa atakuwa amethibitisha kuwa hastahili kupambana.
Endapo mama Killango ataamua kuondoka CCM kwa vile hawamsikilizi atakuwa amethibitisha kuwa hakustahili kusikilizwa. Katika kundi lenye watu wengi na wenye sauti mbalimbali ni sauti iliyo ya juu zaidi na yenye nguvu zaidi ndiyo inasikika. Ndio maana watu kama kina Anna Abdallah wanapotokea na kudai kuwa na wao ni watetezi wa fedha zetu kwa ukimya ninawadharau. Walikuwa wanazitetea fedha hizo kimya kimya wapi? Yaani mwizi aje akwapue vitu nyumbani kwenu halafu mama anapiga kelele na baba anasema hana haja ya kupiga kelele ila na yeye anachukukia wizi huo?
Mama Killango na wabunge wengine wa CCM wameamua kupiga kelele na huko nyuma walikuwa hawasikiki lakini sasa wameanza kusikika. Wale waliokaa kimya muda mrefu na wenyewe sasa inabidi waanze kusikika ili tujue ni nani kweli analia "mwizi mwizi" na ni nani ananuia tu kimoyo moyo! Ni kwa sababu hiyo mama Anne Killango lazima aendelee kuwa CCM ili sauti ile iliyonyamaza kwa muda mrefu hatimaye isikike.
Endapo mama Killango ataamua kujiondoa CCM atakuwa ameonesha woga wa hali ya juu usiomfaa kiongozi yeyote yule. Waoga ndio hukimbia wakizidiwa na ni waoga ndio huweka manyanga chini na kusalimu amri. Wapambanaji wa kweli hawaweki manyanga chini na wanaposema kuwa "hapotoshi" humaanisha hivyo. Kama mama Anne Killango ni mwoga wa CCM, anayeogopa kuwaudhi watu wa NEC na ambaye anagwaya anapozungukwa na genge la magwiji wa kejeli basi ajitoe CCM kwa woga!
Hata hivyo kama yeye ni yule jasiri wa kweli na ambaye maslahi ya Taifa lake yako juu ya chama na itikadi basi kuendelea kumkoma nyani giledi humo humo CCM ndicho kitendo anachostahili kufanya. Waoga hawafai kuongoza, na wenye hofu hawafai kufuatwa!
Endapo wabunge waliochangamka ndani ya CCM na ambao wameanza kuwa watetezi kweli wa mali na raslimali za Taifa letu na ambao hawana hofu tena ya kuita uyoga uyoga wataamua kuondoka CCM utakuwa ni baraka kwa mafisadi ndani ya Chama hicho na wale ambao wanafurahia chama hicho kuendelea na madili mabovu bovu. Sauti za kina Malecela, Nyalandu (japo amechelewa sana), na wengine zinahitaji kusikika zaidi leo hii katika CCM kuliko wakati mwingine wowote. Wakiondoka CCM itarudi kuwa kile chama kilichokuwa kinatawala kwa siri huku kikitumia jinamizi lake la nidhamu ya chama kunyamazisha upinganaji (dissent).
Je wafuate mfano wa Mrema? Kujiondoa kwa kufuata mfano wa Mrema siyo mfano mzuri kwani kama yaliyotokea kwa Mrema yatakuwa kwa kina Selelii, Mwakyembe na Anne Killango au mtu mwingine toka CCM basi tutakuwa tumepoteza vipaji vikubwa sana. Mrema hakuwa na jinsi isipokuwa kuondoka kwani walikuwa wamuondoe vile vile. Mrema kwa kuondoka kwake alijikuta anawekwa nje ya "loop" ya kile kinachoendelea na kwa hakika uamuzi wake wa kutaka kugombea Urais umempotezea muda mrefu sana wa kuwa mchangiaji muhimu katika mjadala wa Taifa. Binafsi ningependa sana Mrema arudi Bungeni, na si yeye tu hata Lipumba, Seif, Mbowe, n.k kwani hivi ni vipaji vilivyoko nje ya uongozi wa serikali na vingeweza kutumika sana wakati huu.
Lakini mama Anne Killango akiondoka CCM anapoteza Ubunge wake wa Same Mashariki na mpambano wa kupata tena nafasi hiyo hautakuwa mdogo. Naamini kila kitu kina wakati wake na hapa alipo sasa ndio wakati muafaka. Huu siyo wakati wa kusalimu amri kwa mafisadi, na kwa hakika siyo muda wa kurudi nyuma kwa woga! Huu ni wakati wa kugangamala mumo kwa mumo!
Je angeweza kupiga kura ya hapana dhidi ya bajeti? Kati ya vitu ambavyo wengi hawaelewi ni kuwa Bunge lisipopitisha bajeti serikali nzima inavunjika na wakati huu ni pamoja na Rais na wote wanarudi kwa wananchi kwa uchaguzi mkuu mpya. Katiba inasema wazi kuwa endapo Bunge halitopitisha Bajeti ya serikali basi Bunge hilo litavunjwa na Rais (Ibara ya 90:2b). Hivyo badala ya kuuliza kwanini wabunge wote wa CCM walipigia kura ya ndiyo hiyo bajeti ni lazima waangalie kipengele hicho. Je wako tayari kurudi kwa wananchi leo hii na kufanya uchaguzi mkuu mpya? Kinadharia tunaweza kusema ni bora warudi wapate mandate mpya, lakini wakifanya hivyo watakaopoteza viti siyo wabunge wa CCM tu bali pia wabunge wote wa upinzani. Je wapinzani katika uchaguzi huo mpya ambao utafanyika ndani ya miezi mitatu wataweza kweli kusimama dhidi ya nguvu za mkono wa CCM na kupata viti vyao vyote walivyokuwa wanashikilia mwanzoni? I doubt it.
Kama wapinzani walishindwa kuchukua viti vya Tunduru na Kiteto wakati kilele cha mambo ya kifisadi kimefikia wataweza kweli kusimama wakati huu ambapo Rais anaweza kufanya mambo kadhaa ya kulitengeneza jina la CCM kwa wananchi? Lakini upande mwingine ni kuwa vipi kama wapinzani watakuwa wamejiandaa vizuri zaidi wakati huu na wale wana CCM walioko madarakani wakajikuta wako matatani. Je kina Karamagi, Msabaha, Rostam, Lowassa, n.k wako tayari kupoteza viti vyao kwa kutoipigia kura ya ndio bajeti ya serikali yao? sidhani. Ni kwa sababu hiyo basi mbunge wa CCM kama Anne Killango asingeweza kuipinga bajeti nzima na akaendelea kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu. Wabunge wa CCM wasingeweza kuipinga bajeti ya serikali yao na wakaendelea kuwa wabunge! Hapa ndipo suala la mabadiliko ya Katiba linapokuja tena na tena!
Ninachosema kwa maneno hayo mengi ni kuwa Mama Malecela na wengine kama yeye waendelee kugangamala humo humo CCM waendelee kupiga kelele kama Yohana Mbatizaji nyikani na pasipo hofu waendelee kupaza sauti zao hata kama itabidi wamwambie Herodi kuwa "huyo uliye naye si mke wako!". Hata kama hilo litamfanya Herodia atake kichwa chao kwenye sahani! lakini kukimbia kwa vile wanapingwa, kugwaya kwa vile wanaitwa majina mabaya, na kujificha kama mbuni kwa vile wanaoneokana vituko si alama ya kiongozi mzuri!
Ni sawasawa na wale waliohama upinzani na kukimbilia CCM kwa vile ati upinzani ulikuwa na matatizo. Kumshauri mama Killango kuhama ni sawa na kumwambia Wangwe kuwa kwa vile anagongana mara moja moja na wenzake Chadema basi akimbie kwenda CCM! Tunawakumbuka waliotoka upinzani kwa vile kulikuwa na migongano na matatizo.. waliamua kurudi CCM kwa vile upinzani kulijaa "ubinafsi, na hawana sera". Kwa wengine hao waliokimbia upinzani na kurudi CCM ni mashujaa! Kwangu mimi ni waoga na wasiostahili kuongoza kwani walikimbia kuwajibika na kushiriki katika matengenezo. Leo hii upinzani TAnzania una nguvu kwa vile kuna watu walisimama kidete na hawakukubali kukimbia matatizo yao ili kuwafurahisha watu fulani. Kwanini tuwatake wa CCM na wao wakimbie ati kwa vile mambo magumu CCM? Leo tunawahitaji watu hawa ndani ya CCM zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule.
Hata hivyo, kuna wakati na saa ambapo mtu kwa dhamira safi atajikuta kuchukua uamuzi wa kutengana na chama chake cha awali. Endapo saa na wakati huo utamfikia mama Killango au wana CCM wengine wowote wale itakuwa inamaanisha kuwa wanafanya hivyo kwa ujasiri wote na si woga au kutishwa. Wataamua kufanya hivyo kwa muda na masharti yao wenyewe.
Vinginevyo, kama CCM inaona haiwezi kuwa na watu kama kina mama Malecela na wengine, basi ni wao wawe wa kwanza kuchukua hatua; wawafukuze uanachama na kuwatimua watoke kwani mawazo na misimamo yao haiendani na chama hicho. Kama hilo ni kweli, basi mpira hauko kwa kina Killango bali uko kwa JK na NEC yake na Kamati KUU. Hamuwataki wafukuzeni, vinginevyo, wataendelea kuwaganda kama kupe hadi mkubali kuwa CCM siyo tena nambari wani, bali Tanzania ndiyo! Kwani, mashujaa hawakimbii, husimama na kupigana hadi tone la mwisho!