Mashuja wa m4c kutoka nyololo wapokelewa kishujaa mbeya jioni ya leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashuja wa m4c kutoka nyololo wapokelewa kishujaa mbeya jioni ya leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndyali, Sep 6, 2012.

 1. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Itakumbukwa kuwa makamanda kutoka Mbeya walijitolea kwa ghalama zao kwenda kuongeza nguvu katika vuguvugu la M4C kwa kutoa elimu ya uraia katika vijiji vyote vya mkoa wa Morogoro, kwa mafanikio ya Morogoro tayari ripoti ishatolewa na mkuu wa oparation hiyo. Walipotoka Morogoro Makamanda hao walitua katika vijiji wa mkoa wa Iringa wakienda nyumba kwa nyumba na kuharibu kabisa ngome za ccm vijijini katika vijiji vya jimbo la Mfindi, wote tulisikia Dr. Slaa akieleza mafanikio katika vijiji vya wilaya ya Mfindi, taarifa ya Dr. Slaa iliwashitua usalama wa taifa na polisi wakalazimika kupanga njama za kuwaunganisha Makamanda wa Mbeya na kesi ya mauaji ya RIP Mwangosi. Hivyo polisi waliamua kuwakusanya makamanda 32 wa Mbeya waliokuwa wamejichimbia vijijini kutoa elimu ya uraia. Siku ya leo baada ya kugundua kuwa somo lao halieleweki kwa watanzania wamewaachia, na jioni ya leo msururu mkubwa wa magali yaliyotoka kuwapokea mashujaa wetu mpakani mwa Iringa na Mbeya umepita hapa maeneo ya ccm kwa shangwe kuu ya ajabu. Kweli Mbeya wamedhamiria kuwa mashujaa wa M4C.
   
 2. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Polisi walikuwa wanazunguka mitaani wakitoa somo?.
  Je linahusu nini?.
   
 3. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Kyaiyembe, Usiwe mvivu wa kuelewa lol.
   
 4. z

  zee la weza Senior Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii habari umepika, inawezekana wewe ni gamba
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo waliokuwa Nyororo wooote ni wageni? Tunaambiwa Polisi walikuwa wageni na makamanda wa CDM nao kumbe walikuwa wageni toka Mbeya. Hatari wageni kwa wageni wanapambana!
   
 6. m

  malaka JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hili la kobe hili si bure. Mud ondoa hii kitu hapa.
   
 7. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari si ya kweli!hakuna kijana wa Mbeya aliyeenda Iringa,ila tulikuwa tumepanga kwenda tarehe 9-9,kwenye mkutano ambao ungefanyika Iringa Mjini,cku ya Hitimisho!
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Bado mnazidi kuchanganya mambo. Toka Mbeya kwenda Iringa kwa hiyo hakuna tofauti na CCM wanaobeba watu kwenye mafuso?
   
 9. t

  tenende JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo shule au bangi?!
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Ukombozi utaanzia Mbeya
   
 11. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli kwani sentensi yako haikuweka wazi nani hakueleweka kwa watanzania, na ndiyo nikataka kujua ni somo la nani halikueleweka badala ya kunielezea unaniambia tatizo nililonalo, Sawa sikukuelewa nifafanulie." Hivyo polisi waliamua kuwakusanya makamanda 32 wa Mbeya waliokuwa wamejichimbia vijijini kutoa elimu ya uraia. Siku ya leo baada ya kugundua kuwa somo lao halieleweki kwa watanzania wamewaachia"
  Ndiyo tatizo shule maana nilifundishwa kuwa kama kuna kitu sijaelewa niulize ili nieleweshwe zaidi. Hilo ni kosa?.
   
Loading...