Mashuga mami na mashuga dadi

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Suala la mashuga mami na mashuga dadi linazidi kukua maeneo mengi nchini Tanzania huku maeneo ya majiji kama vile dar, arusha, mwanza, mbeya na tanga ikiwa ni vinara.

Kutokana kwamba jamii yetu imeonyesha kushindwa kupunguza au kuzuia kabisa, mimi nadhani hii tabia tunaweza kuitumia kwa manufaa ya jamii na nchi kwa ujumla.

KIVIPI!? Uchunguzi wangu umebaini ya kuwa ni nadra sana kwa mama mtu mzima kumsaidia kifedha binti asiyemjua vile vile ni nadra sana kwa wanaume mtu mzima kumsadia kijana asiyemfaham kirahisi.

LAKINI ni rahisi sana kwa mama mtu mzima kumpatia fedha kijana kadri ya uwezo wake hata kwa wababa pia huwapatia mabinti wadogo pindi wanapokuwa na uhusiano wa kimapenzi (Kapuya 2013). Na si pesa tu, huwasomesha, huwapa magari, huwajengea nyumba, kuwafungulia biashara n.k

Kama tutafikiri kiujasiriamali nadhani hiyo ni fursa kubwa tena sana.

Vijana wanamaliza chuo lakini wanakuwa hawana ajira wala mitaji ya kuanzisha biashara na kwenye banks mbali mbali masharti yao ni magumu sana ili waweze kukukopa pesa sasa kwanini kama wewe ni binti usitafute shuga dadi nawewe kijana usitafute shuga mami ili akupe fedha kisha ukaanzishe biashara yako.

Kumbuka, pesa ipo mikononi mwa watu wachache sana na jinsi ya kuipata ni kazi sana lakini kupitia shuga mami au shuga dadi utapata fedha nyingi sana, kwanini? anaamini njia pekee ya kukufanya ubaki kwake ni kukupa fedha (japo si kweli) pia anakupa fedha nyingi kama sehem ya kumfichia siri yeye ili watu wasijue kuwa anatembea na mtu ambaye sawa na mwanae.

Endapo ukapata fedha toka kwa shug mami/dadi na ukaanzisha mradi wako wa kufuga kuku hauoni ya kuwa utakuwa na uwezo wa kuajiri vijana wa kuhudumia kuku pamoja na kuokota mayai hivyo utakuw umetengeneza fursa kwa wengine.

Kama umepewa fedha na ukaanzisha mradi wa kilimo huoni ya kuwa utaajiri vijana wa kulima, kupalilia, kuvuna na kuongeza chakul chini.

Ajira zinapoongezeka maana yake ni kwamba maisha ya watu yatazidi kuimalika yanapoimalika ndipo uchumi wa nchi utazidi kukua.

Mashuga mami na Mashuga Dadi wanaweza kukuza uchumi wa Taifa endapo watatumika vizuri.
 
Mleta mada kama wewe elimu yako ni kidato cha nne au umevuka hapo, ni ishara tosha kwamba elimu ya Tanzania ni ya kwenye makaratasi tu, na siyo ya kutukomboa kimaisha au kiuchumi.
 
Mleta mada kama wewe elimu yako ni kidato cha nne au umevuka hapo, ni ishara tosha kwamba elimu ya Tanzania ni ya kwenye makaratasi tu, na siyo ya kutukomboa kimaisha au kiuchumi.

watu kibao wana elim kubwa na hawajaokoka kiuchumi, hii ni idea nzuri sana itakayopingwa na wengi
 
mkuu ulichoongea nisawa hasa kwa vigogo na watu wenye madalaka mbalimbali wanatumia pesa nyingi sana ilikuficha siri zako zisivuke nje na kuwahalibia sifa zao.vip kuhusu magonjwa ya zinaa hasa UKIMWI.hayawezi kuongezeka kweli????
 
ungetumia muda wa kuandika uzi huu hata kwa kukaa kimya ungekuwa umefanya la maana.zinaa tena unaipa promo?
 
mkuu ulichoongea nisawa hasa kwa vigogo na watu wenye madalaka mbalimbali wanatumia pesa nyingi sana ilikuficha siri zako zisivuke nje na kuwahalibia sifa zao.vip kuhusu magonjwa ya zinaa hasa UKIMWI.hayawezi kuongezeka kweli????

Suala la ukimwi si kwamba ni la watu wazima pekee, ukimwi haujali umri wala fedha. mtu yeyote anaweza kupata mahali poppte
 
Back
Top Bottom