Mashtaka mapya yanayowakabili Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashtaka mapya yanayowakabili Viongozi wa Kitaifa wa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nanyaro Ephata, Feb 21, 2012.

 1. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA,Freeman Mbowe,Dr Slaa,Mwigamba,Magoma,Wabunge Lema,Selasini,Ndesamburo,na wanachama wengine,inaendelea leo,kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha.
  Baada ya kubadilishiwa mashtaka,leo wakili wa serikali anasoma mashtaka mapya 13,
  Ntaendelea kuwajuza.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mkuu tunashukuru tupe habari mambo yanatukimbiza mpaka tunasahau
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watarekebisha sana hati ya mashtaka mpaka watakapogundua kuwa watuhumiwa hawana kesi ya msingi. Tunashukuru kwa taarifa kamanda. Keep us posted
   
 4. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  poa mkuu,
  Maana watu wamekalia wimbo slaa slaa slaa slaa!how.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu.Endelea kutujuza
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Washtakiwa wapo mahakamani?
   
 7. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wakili wa serikali anaomba mahakama,itoe hati ya kukamatwa kwa Dr Slaa,Aquiline Chuwa na Josephine kwa kutokufika mahakamani leo,hoja ambayo imepingwa vikali na wakili wa utetezi na kuomba mahakama kuwa shauri liendelee na mashtaka yasomwe.
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba haki ya msingi itajulikana na kupatikana kwa mahakama kuu ya wananchi na sio mahakama hizo zinazoongozwa kwa maslahi ya watu au kundi fulani..
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja, haki ya mnyonge husimamiwa na mungu!
   
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyo Wakili wa Serikali ni wale wale, Masaburi anajua akili zao wanazotumia kufikiria zilipo.
   
 11. e

  evoddy JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tupo pamoja watabadilisha sana mashitaka mwisho wa siku CHADEMA tutashinda,ikiwezekana wafungue kesi kila kona ya nchi hii lakini CHADEMA itashinda maana inatumia NGUVU YA UMMA na wala siyo nguvu ya polisi wala mahakama
   
 12. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hii kesi haina dadline??
   
 13. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Mashtaka hayo ni
  1.Kati ya tarehe 3-5Jan 2011.Kula njama ya kutenda kosa
  2.Washtakiwa wote,kasoro Mwigamba.Kula njama ya kufanya kosa kinyume cha kanuni ya adhabu 385,kutotii amri halali
  3.Wote kasoro Mwigamba.Mkusanyiko usio halali
  4.Wote kasoro Mwigamba,Kufanya vurugu baada ya amri iliyowakataza kufanya vurugu,chini ya kanuni 384
  5.Dr Slaa,na Ndesamburo,kati ya Jan 3,na 5,kutoa matamshi ya uchochezi,ndani ya manispaa na wilaya na mkoa wa Arusha
  6.Dr Slaa,Ndesamburo na Mwigamba.Kushawishi watu wengine kufanya kosa
  7.Washtakiwa wote kasoro Mwigamba.Jan 4 na 5,kukataa kutii amri halali ya polisi na huduma zake,iliyowaelekeza jinsi ya kufanya maandamano(walikataa njia walizokubaliana na polisi)
  8.Kufanya kusanyiko lisilo halali,eneo la hotel ya Mount meru,wakiwa zaidi ya watu watatu,kinyume na kanuni ya 45,pia kukataa kutii amri ya OCD
  9.Kufanya fujo,eneo la Mount meru hotel,hata baada ya tamko la OCD,kinyume na kanuni ya 179.
  10.Linamkabili Dr Slaa peke yake,na halikusomwa kwa kuwa Dr Slaa hayupo mahakamani
  11.Mh Ndesamburo pekee yake,kuwa alitoa maneno ya uchochezi.Maneno yenyewe ni.Kikwete unanipiga mabomu?Kikwete polisi wako watapiga risasi zitaisha lakini tutawashinda,Kikwete huna Baba?maneno hayo yalitolewa kati Jan 4 na 5,eneo la NMC
  12.Dr Slaa,Mh Ndesamburo,na Mwigamba,eneo la nmc,kufanya kosa la kushawishi watu kwenda kuwakomboa watu waliokuwa wameshikiliwa kituo cha polisi kihalali
  13.Kusababisha hofu kwa wananchi
  Washtakiwa wote wamekana mashtaka yote,kesi imeahirishwa hadi kesho kwa ajili ya kusikilizwa
   
 14. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyo wakiri wa serikali kasoma wapi?tupatie cv yake asije akawa ndo walewale wa kata
   
 15. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  wafungwe maisha hao!
   
 16. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Mwanzo walishtakiwa kwa makosa gani na ni kwa nini wamebadilisha mashtaka tena? Sasa hawaoni na wao kuwa hawajatulia wanakurupuka tu?
  Natamani nisikie wamehukumiwa vifungo vya miaka 3 jela? Nchi ingeshika adabu yake
   
 17. a

  a man of the hill Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watabadilisha sana hati za mashtaka!.,Haki haijawahi kushindwa hata siku1,..Makamanda watashinda,waTz tutashinda na taifa litakombolewa lazima.Msiogope kwa hayo yanayotokea,ni udhihirisho wa kuanguka kwa utawala wa kidhalimu.Huko ndo kutimilika kwa ISHARA za ANGUKO!!!,...
   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  hizi kesi za kisiasa kazi kweli kweli.
   
 19. a

  a man of the hill Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TIMU KALI YA VIONGOZI CDM IMEPATIKANA JIMBO SEGEREA!...Uchaguzi uliofanyika j2 ya tar19 baada ya kujiuzulu kwa uongozi uliokuwepo,umepelekea kupatikana kwa timu kali(Barcelona).Viongozi waliochaguliwa ktk nafasi ya uenyekiti,ukatibu,na ukatibu wa itikadi+uenezi inasemekana wanapikika chungu kimoja na wamebatizwa jina la 'mapacha wa3',..Inaelezwa kwamba kwa kikosi hiki ccm imekwisha!!
   
 20. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo namba 11 ni laana kwa JK na wote waliomshauri wala siyo kosa la kisheria! Laana itamtafuna JK hadi mwisho wa uhai wake kama hatatubu!!
   
Loading...