Mashtaka dhidi ya Viongozi kama DCs na RCs ni ufunguo wa Mashtaka dhidi ya viongozi wa juu

nabali

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
377
500
Haya ni maono tu.
Leo hii tunashuhudia mashtaka na vifungo dhidi ya watawala ngazi ya mikoa na Wilaya.
Huu ni ufunguo wa mashtaka na vifungo dhidi ya viongozi ngazi ya juu.
lets watch and see.

kwaherini kwa leo
#WAPOLOO A.K.A WAHUNI

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Kufungwa kwa DC Sabaya na Atapohukumiwa Makonda kituunganishe sote wana CCM na wana CHADEMA kudai kuondolewa kwa kinga ya kushitakiwa viongozi wa juu ikiwemo Rais wa Jamhuri ya Tz! Huu upepo usiishie kwa hao dagaa wadogo walokuwa wakitimiza walichotumwa!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,288
2,000
Haya ni maono tu.
Leo hii tunashuhudia mashtaka na vifungo dhidi ya watawala ngazi ya mikoa na Wilaya.

Huu ni ufunguo wa mashtaka na vifungo dhidi ya viongozi ngazi ya juu.

Let's watch and see.

kwaherini kwa leo
WAPOLOO A.K.A WAHUNI

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Ukiambiwa umesanda unarusha ngumi hewani
 

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,875
2,000
CHADEMA kushika madaraka siyo rahisi labda mwaka 2055
Mazoea ni mabaya sana.

Wewe unaona hao viongozi wote hawatakiwi kushtakiwa mbele ya sheria wanapofanya uhalifu?

Wakiua, wasishtakiwe kwa vile ni viongozi? Wakiiba wasishtakiwe, kwa vile ni viongozi?

Hii ni nchi au jalala la watu kujifanyia lolote wanalotaka, mradi tu ni viongozi?

Mada ya kipuuzi kabisa hii. CHADEMA wakishika madaraka, bado utang'ang'ania viongozi hao wasishtakiwe kwa kuwaonea tu mahasimu wao wa CCM wanaowatesa kwa sasa hivi?
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,356
2,000
Mahakama hutoa adhabu kwa aliyethibitika kutenda kosa na Lengo moja wapo la adhabu Ni kutoa somo na hofu kwa wengine.
Ni vyema endapo Kuna ushahidi dhahiri marehemu washitakiwe na kuhukumiwa japo hawapo duniani. Mfano muuaji watoto school bus, Kisha akajiua baada ya tukio, isishie hapo, kina Hitla pia na wengine.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
18,903
2,000
Kijiti kikupakacho haja kubwa ukikanyaga wakati unajisaidia!!
===
Asante mleta mada. Kwa sababu sasa rejea ya kesi zimeishapatikana.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Sheria haianzii nyuma
Ni kweli. Lakini hiyo kanuni imetungwa na Bunge. Ukipelekwa mswada Bungeni, sheria ikatamka kuwa hiyo sheria haitahusu makosa dhidi ya ubinadamu na viongozi kujinufaisha walipokuwa madarakani, kila kitu kitaishia hapo. Watakokotwa kwenda mahakamani. Ndivyo ilivyofanyika kwa Sadam Hussein kuke Iraq. Kinga haikusaidia.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
14,403
2,000
Kama ulikuwa kichwani mwangu. Hizi sheria za kinga wanazojiwekea zinakuwa na nguvu kutegemea nani yuko madarakani.

Wasitegemee akikamata nchi mzalendo kwamba watasalimika nyang'au hawa
Huyo mzalendo kama atatokea chama hiko hiko hatofanya lolote.. refer mzalendo aliepita? Aliwafanya nn marais waliopita,?
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,433
2,000
I
aMl ni maono tu.
Leo hii tunashuhudia mashtaka na vifungo dhidi ya watawala ngazi ya mikoa na Wilaya.

Huu ni ufunguo wa mashtaka na vifungo dhidi ya viongozi ngazi ya juu.

Let's watch and see.

kwaherini kwa leo
WAPOLOO A.K.A WAHUNI

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!

Mlikuwa mnafanya uhalifu mkiwa madarakani mkitegemea hamtakaa mshitakiwe? Na hapo ni bado maana CCM bado iko madarakani, iko siku mtatoka madarakani tutafukua yote maana jinai haifi.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,771
2,000
Hakuna aliye juu ya Sheria. Hata SSH ajiandaye siku nikiwa rais nitafuta kinga nakumpeleka mahakamani
Kwani sheria ikitungwa leo, inarudi nyuma? Nijuacho inaanza kufanya kazi siku inapotungwa kwenda mbele... Atajayetenda kinyume wakati ipo, huyo ndo itamuhusu
 

emmanuel mruma

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,706
2,000
Kama ulikuwa kichwani mwangu. Hizi sheria za kinga wanazojiwekea zinakuwa na nguvu kutegemea nani yuko madarakani.

Wasitegemee akikamata nchi mzalendo kwamba watasalimika nyang'au hawa
Hata aje mzalendo vipi hawezi jitolea Kinga yeye akiwa raisi Maan anajua nae Kuna siku atastafu mwenzie ajae kama alikuwa mpinzani wake kisiasa atamtafutia tu sababu amsulubu... Hichi kifungu ni wana nchi wenyew wakomae kupitia wabunge ili kiondolewe... Usitegemee Kuna raisi yyte atasema ajiondolee Kinga hamna uzalendo wa ajabu kama huo kwene siasa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom