Mashoga Waliopo nchini Kenya Kuhesabiwa

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20


Mashoga Waliopo nchini Kenya Kuhesabiwa
Serikali ya Kenya iko mbioni kufanya sensa ya kuwahesabu mashoga waliopo nchini humo katika jitihada zake za kuwaelimisha watu juu ya ugonjwa wa ukimwi.

Serikali ya Kenya inajiandaa kuwahesabu mashoga waliopo nchini humo ingawa kwa sheria za Kenya mashoga huadhibiwa kwenda jela miaka 14 wanapokamatwa.

Nicholas Muraguri, mkuu wa taasisi ya kuzuia kuenea kwa ukimwi ya Nascop, akiongea na shirika la habari la BBC alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa serikali ya Kenya kufanya takwimu ya mashoga nchini humo.

Alisema kuwa mashoga wengi hawana elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanahofia kuwa mashoga wengi watahofia kujitokeza kuhesabiwa kwa kuhofia kukamatwa na kutupwa jela.

Muraguri alisema kwamba takwimu hiyo itahusisha pia mashoga kutajana wenyewe kwa wenyewe huku maafisa wengine wakiwapima kama wameambukizwa virusi vya ukimwi pamoja na kuwafundisha njia salama za mapenzi.

"Wakenya hawawezi kusema kuwa mashoga ni jamii iliyotengwa, ni miongoni mwa jamii zetu", alisema Muraguri.

"Kundi hili inabidi lifikiwe na lipewe mafunzo ya jinsi ya kujilinda wasiambukizwe", alisema.

Sensa hiyo ya mashoga imewagawanya Wakenya wengi huku baadhi yao wakisema hawaamini kama itasaidia chochote katika kuzuia kuenea kwa ukimwi.

Baadhi ya mashoga waliohojiwa na BBC walitanabaisha kuwa wako tayari kuhesabiwa iwapo sensa hiyo itafanyika kwa siri.

Mashoga na wasagaji wanapokamatwa nchini Kenya huadhibiwa kutumikia vifungo vya miaka 14 jela.



Source: BBC
 
Back
Top Bottom