Mashoga Walana Denda Mbele Ya Papa(Video+News) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga Walana Denda Mbele Ya Papa(Video+News)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, Nov 8, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  VIDEO - Mashoga Walana Denda Mbele ya Papa
  [​IMG]
  Monday, November 08, 2010 2:42 AM
  Mamia ya mashoga wa nchini Hispania walinyonyana ndimi kwa dakika tano mbele ya Papa Benedict XVI katika kupinga kauli zake za kupinga ndoa za wanaume kwa wanaume. Ziara ya Papa Benedict XVI nchini Hispania imekumbana na vioja vya mashoga wa nchini humo ambao waliamua kunyonyana ndimi mbele yake ili kupinga kauli zake za kupinga utoaji mimba na ndoa za watu wa jinsia moja.

  Wakati gari la Papa ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 83 lilipokuwa likipita barabarani mbele ya maelfu ya waumini wa kanisa katoliki mjini Barcelona, mamia ya mashoga na wasagaji walinyonyana ndimi hadharani kwa takribani dakika tano ili kuonyesha upinzani wao kwa kanisa katoliki.

  Hata hivyo pamoja na mashoga kuonyesha upinzani wao, Papa katika hotuba yake aliendelea kukemea ndoa za jinsia moja na utoaji mimba.

  Papa alisema kuwa sheria za Hispania zimewapa nafasi wanawake kutoa mimba kirahisi na pia wanaume kuwaoa wanaume wenzao.

  Papa aliendelea kusema kuwa kanisa katoliki litaendelea kukemea hali zozote zinazopingana na maisha asilia ya binadamu katika kujenga familia bora.

  Chini ni VIDEO ya tukio hilo la mashoga kunyonyana ndimi mbele ya
  Papa.

  YouTube - Gay kiss protest at Pope visit
   
 2. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hii sasa hatari jamani.
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakti wa mwisho huu.....Allah atunusunuru...........
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inanikumbusha enzi za sodoma na gomora, mambo yalianza hivi hivi.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sina la kusema...lakini mwisho wa hii ni mbaya, na uko karibu!
   
 6. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata wakati wa Sodoma na Gomola, Malaika walipoenda nyumbani kwa Lotu, watu wengi waliivamia nyumba ya Lotu wakitaka kuwalawiti malaika hao. lakini watu wale walitiwa upofu na wasiwaone Malaika wale na hivyo wakaondoka bila kudhurika. Kwa hiyo jambo la uhuru wa ushoga na usagaji si jipya katika uso wa dunia. Hata hivyo kwa nguvu za Mwenyezi Mungu aliye juu ya kila kiumbe na hata Mamlaka za hapa Dunianai; tabia hizi zitaangamizwa kama ilivyoangamizwa Sodoma na Gomola. AMEN
   
 7. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mfano Wa Magugu
  Mathew; 13:24-29
  24Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema: '‘Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.
  27"Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, ‘Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi ?
  28Akawajibu, ‘Adui ndiye aliyefanya jambo hili.' Wale watumishi wakamwuliza, ‘Je, unataka twende tukayang'oe? "
  29Lakini akasema, 'Hapana, msiyang'oe, kwa maana wakati mking'oa magugu mnaweza mkang'oa na ngano pamoja nayo. 30Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji, wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto, kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.' ''

  Yana mwisho hayo!
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  :tape: gosh!!!

  Men wanakulana denda!!!
   
 9. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Dunia imeharibika sasa, imekosa mwelekeo.
   
 10. 2my

  2my JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli dunia imekwisha kwa stail hii!!!!
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yapo siku nyingi sana ila sema yalikuwa chini ya meza.

  Msijifanye neno Ms**ge na Ba*ha hamjawahi kuyasikia. Hata Bwabwa pia bado?

  Sisi jamii yetu imeweka kila kitu TABU tofauti na wenzetu.

  Mie siwashambikii hawa Mashoga na wala siwapingi. Ila sikubaliani na kitendo chao cha kwenda mbele ya PAPA na kuonyesha huo uchafu wao. Kama unataka kuwa Shoga basi lazima ujuwe kuwa dini hairuhusu. Siyo lazima uwe Mkatoliki na siyo lazima uwe shoga. Unaweza kuchagua kimoja wapo na ukaendelea kuishi salama bila kumtibua mtu mwingine.

  Tatizo lao hawa jamaa wanataka kula keki na kuendelea kuwa nayo mkononi. Ingelikuwa ni SHERIA ya nchi na Papa ndiye analazimisha hiyo sheria iwepo (kama ilivyo nchi za Siasa kali) basi hapo wangelieleweka. Ila Spain ni nchi inayowaruhusu wafanye wanayotaka. Papa anasema kwa waumini wake na si kwa watu wote. Kama wewe ni Mkatoliki basi ujuwe sheria inasema hivyo. Ila kama wewe si Mkatoliki, sidhani maneno ya Papa yana uzito wowote kwako.

  Mimi mwenyewe hapa siyo Mkatoliki. Maneno anayoyatoa Papa huwa nayachukulia kama maneno anayoyatoa Rais wa Peru au Sheick fulani. Kwanza hata huwa simsikilizi sasa hata akifokea mambo huko au kulaani, mie hilo halinihusu. Nguvu ya Papa imepunguzwa sana sasa hivi duniani. Hata Italy, wamebakiza nguvu zao ndani ya kimji chao cha Vatican tu. Sasa hawa Mashoga huu upuuzi wao wa kumfuata Papa sijui wanafikiria vipi? Ni sawa na Papa angeliwafuata wao kwenye Madangulo au Love Parade. Hebu fikiri siku kuna Brazil Carnival, mashoga wako kazini na ghafla Papa anaibuka na kuanza kuwalaani, si ingelikuwa uchokozi? Hawa jamaa ni WACHOKOZI. Na kwa hili hata mie Nawalaani.
   
 12. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nafikiria huko mbele biadamu wanaweza kutoweka haya mambo ya ushoga yanavyoenda kasi. Nani atazaa?
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,476
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Aisee hii ni hatari.
   
 14. M

  MUSINGA JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Tembelea Sweden kakangu utashangaa,kwenye treni limejaza kama daladala ya posta mbagala halafu jirani yako waliosimama ni midume miwili ya nguvu inakula denda pata picha na kuitana Baby
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Siyo Sweden tu Mkuu wangu. Huko ni cha mtoto......

  Mambo mazito yapo German na Uholanzi. Huko ni mwisho wa matatizo. Hasa Waholanzi, duuu!!!!

  Ila sema hawa jamaa kila kitu kiko maeneo special ambayo yanajulikana na jamaa wanalipa KODI.
   
 16. M

  MUSINGA JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  kaka dunia imeisha jamani,inafika mahali unaogopa hata kushika mkono wa mwanaume mwenzio maana huelewi nini kitatokea
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  dunia ilishaharibika toka zamani sema tu nyinyi taarifa zilikuwa haziwafikii , na inabidi muwashukuru hao hao mashoga na wanaoruhusu ushoga kwa sababu ndio wamewawezesha kuona mambo yanayotendeka duniani ..ila sio kitu cha kushangaza sana kwa sababu hawajaanza jana au juzi.
   
 18. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #18
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Tuzidi kusali jamani kwani dalili ndo hizi
   
 19. w

  wikama Member

  #19
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huu ndo mwisho wa dunia maana shetani nae ana watu wake anaowatuma kufanya matakwa yake, ina maana hakuna wanaume mpaka wanawake wasagane au hakuna wanawake mpaka wanaume waowane hii ni aibu mwamini yesu uepukane na haya ni balaa tupu na ufusika !
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  eww..:puke:
   
Loading...