Mashoga wahukumiwa kifungo cha miaka 14 Malawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga wahukumiwa kifungo cha miaka 14 Malawi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Ni baada ya kukamatwa wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja
  BLANTYRE, Malawi
  JAJI wa mahakama ya Malawi, Nyakwawa Usiwa amewahukumu kifungo cha miaka 14 jela wanaume wawili waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

  Akitoa hukumu hiyo jana Jaji huyo alisema kuwa hukumu hiyo ni sehemu mojawapo muhimu ya kukomesha vitendo vya aina hiyo nchini humo na hata katika nchi jirani zinazolinda tamaduni za Afrika.

  Mashoga ambao ni wapenzi ni Steven Monjeza, 26, na Tiwonge Chimbalanga, 20, ambao tangu kukamatwa kwao Desemba 21 mwaka jana walikuwa wakishikiliwa mahabusu ilikuwa ikisubiriwa huku ikiibua mijadala kuhusu vitendo vya ushoga na sheria ya nchi hiyo inayopiga marufuku vitendo hivyo.
  Kwa pamoja walikamatwa wakati wakiwa katika sherehe yao ya kuvalishana pete ya uchumba, hatua iliyoibua mshangao nchini humo na kwa nchi jirani.

  “Hukumu hii ni sehemu mojawapo muhimu ya kukomesha vitendo vya aina hiyo nchini humo na hata katika nchi jirani zinazolinda tamaduni za Afrika.” Alisema Jaji Usiwa.

  Suala la mapenzi ya jionsia moja ni kinyume cha sheria katika nchi 37 za Afrika. Nchini Uganda, watunga sheria wanaendelea na mjadala wa sheria mpya inayotaka kutoa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani na adhabu nyingine zinazoambatana na adhabu hiyo.

  Hata kwa Afrika Kusini, nchi pekee ya Afrika inayotambua haki za mashoga, yamekuwa yakijitokeza makundi ya watu ambao wamekuwa wakiwabaka makusudi wahusika yakieleza kwamba hatua hizo ni kwa ajili ya kuwakomesha na kuarekebisha wahusika hao.

  Serikali ya Malawi imekuwa ikipuuza upinzani kutoa baadhi ya mataifa ya Ulaya tangu kukamata kwa watuhumi ahao wawili, ambapo miezi kadhaa kabla ya kutiwa hatiani, Waziri wa Habari, Leckford Thoto alisema iko wazi kwamba wamevunja sheria za nchi hiyo.

  Viongozi wa makanisa nchini humo wamekuwa wakiunga mkono hatua hiyo ya serikali yakisisitiza kwamba mapenzi ya jinsia moja “ni dhambi” na mataifa ya magharibi hayatakiwi kutumia ushawishi wake wa kifedha kuilazimisha Malawi, ambayo inategemea ufadhili wa asilimia 40 ya bajeti yake kutoka kwa wafadhili ikubaliane na dhambi hiyo.
  AP

  Mashoga wahukumiwa kifungo cha miaka 14 Malawi

  NINGEOMBA MUNGU NA HAPA KWETU BONGO MHESHIMIWA JK AWEKE SHERIA HIYO KAMA YA WAMALAWI MNASEMAJE WENZANGU WANA JF?
   
Loading...