Mashoga nchini Tanzania

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Nasikitika sana na ushoga nchini. Vijana wanaharibika
 
Last edited:
Sikutaka hii habari iwe kama TETESI kwakuwa nilichokiandika nimekisikia kwa masikio yangu kutoka kwa mtu live. Pia ni mahojiano niliyoyafanya na huyu kijana kwa takribani saa moja kwa umakini na hapa nimeandika machache tu kati ya mengi tulijadiliana na huyu kijana ikiwa ni pamoja na kuacha hii kazi kwa msaada atakaopewa na baadhi ya watu waliojitolea baada ya ushuhuda wake wakati wa tamsha ili la jinsia, lengo likiwa ni kumrudia MOLA wake na kuwa mjumbe wa AMANI kwa vijana wenzake wa Tanzania na dunia kwa ujumla. ila naona imeandikwa tetesi, sijui moderator ndie kaona iwe hivyo, sijajua sababu. Nway lengo ni kuelewa lakini narudia kusema kuwa SIO TETESI HATA KIDOGO
 
Sipo,
Mienendo inayoonekana haikubaliki, hujengwa na walewale wanaotegemewa kulea mienendo inayoonekana mema katika jamii - wazazi, walezi n.k.Kuhukumu bila kuangalia chanzo cha tatizo siyo njia nzuri ya kutatua tatizo.Kuna mashoga kulazimishwa kuwa mashoga kama huyu kijana, kuna mashoga wengine inasemekana huzaliwa mashoga......
Hapo hapo tunaambia kiimani za dini ushoga ni dhambi, jamii zetu nazo hazikubali watu kama hawa miongoni mwetu.

Kilicho dhahiri ni kwamba mashoga wapo tena kwa idadi kubwa mno miongoni mwetu tupende tusipende.Sasa sijui tutafanya nini..
tuwakubali kuwa ni sehemu ya jamii zetu au tufanyeje?
 
Last edited:
Jitahidi kutafuta kidatu cha Clash of Cultures and cha Samule ambaye Professor wa Havard anaelezea vizuri kuhusu mambo haya huku kwetu na misuguano yake
 
NO, sorry.You are wrong? What is huzaliwa mashoga.......? the anatomy must be there!

Huwa na hormones za kike/kiume zaidi ya zile wanazopaswa kuwa nazo..hivyo their sexual orientation tends to be inclined towards......
kama ni mwanaume (pamoja na kuwa mwanaume) huvutiwa zaidi na wanaume wenziwe.
Zipo tafiti zinazolenga kuthibitisha kuwa kuna kinasaba ( gene) kinacholeta hali hii.Ofcourse kuna wenye kujiendekeza kwenye ushoga kama hulka tu lakini wapo ambao huwezi kuwalaumu kwa kuwa katika hali hiyo.
 
NO, sorry.You are wrong? What is huzaliwa mashoga.......? the anatomy must be there!
yah sio kuzaliwa kuwa mashoga, lakini wanakuwa na homony nyingi za kike na akishafika muda wa kubalehe ndio vichocheo hivyo vya kike vinakuwa juu na unakuta mtu anaanza kuplactice hayo mambo na ndio maana akasema wapo waliozaliwa hivyo
 
katika sababu zilizotolewa kuna kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 ambaye naye ni shoga ambaye yeye alisema kuwa anajisikia kuwa na ahamu ya kuwa mwanamke. Na alipopelekwa hospitali na mama yake madaktair walisema hawana vipimo vya kitaalamu lakini walimwambia kuwa inaonyesha kuwa ana hormones nyingi za kike kuliko za kiume
 
Jitahidi kutafuta kidatu cha Clash of Cultures and cha Samule ambaye Professor wa Havard anaelezea vizuri kuhusu mambo haya huku kwetu na misuguano yake
Mkuu huwezi kutupatia means ya kukipata hiki kitabu kikatusaidia wengi zaidi
 
Kilicho dhahiri ni kwamba mashoga wapo tena kwa idadi kubwa mno miongoni mwetu tupende tusipende.
Ni wengi sana na cha kutisha sasa hivi wengi ni vijana wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 25 na kuendelea

Ila kinachosikitisha sana ni hao wateja wao ambao ni ELITES na watu wenye nafasi zao nzuri sana kwenye jamii na wengine wanasimama na kupinga ufisadi, UKIMWI na uovu mwingine

MUNGU atusaidie tuepukane na janga ili maana hukumu yake nu kubwa na ya jabu hapa duniani na jehanamu
 
ila kilichonishtua ni pale shoga mmoja aliposema ameshatembea na kiongozi mmoja wa dini ambaye anasimama mbele ya waumini na kutoa neno takatifu
Jamani, jamani, jamani jamani, dunia (Tanzania) inaenda wapi hii Mungu wangu
 
Ni wengi sana na cha kutisha sasa hivi wengi ni vijana wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 25 na kuendelea

Ila kinachosikitisha sana ni hao wateja wao ambao ni ELITES na watu wenye nafasi zao nzuri sana kwenye jamii na wengine wanasimama na kupinga ufisadi, UKIMWI na uovu mwingine

MUNGU atusaidie tuepukane na janga ili maana hukumu yake nu kubwa na ya jabu hapa duniani na jehanamu

Kuna rafiki yangu aliolewa na Mmarekani mweusi... aliwahi kuniambia kua moja ya changamoto kubwa kule ni kujua kama mumeo ni mwanaume kamili na siyo mwenye hulka ya ushoga ( bi-sexual)...Tanzania, hali pia imeanza kuwa kama hivyo... kuna wanaume wengi tena wenye kuheshimika katika jamii wamejiingiza sana kwenye tabia hii.Mungu apishilie mbali!Tuko zama za Sodoma na Gomorah!
 
yah sio kuzaliwa kuwa mashoga, lakini wanakuwa na homony nyingi za kike na akishafika muda wa kubalehe ndio vichocheo hivyo vya kike vinakuwa juu na unakuta mtu anaanza kuplactice hayo mambo na ndio maana akasema wapo waliozaliwa hivyo
Angalia ya Caster Semenya yule dada msauzi je akiwa msagaji watu watashangaa? hapana hii ni kutokana na matokeo yaliyotolewa kuwa ana homoni za kiume mara tatu kuliko za kike.
 
Hii tabia imeongezeka siku hizi, kuna jamaa wanasema watoto wa kike wa mjini wengi wanatabia za kufanya mapenzi kinyume na maumbile. japo pia kuna madingi wakubwa tu halafu ni mashoga cha ajabu watafuta vijana wa kutoka nao. sijui ndio utanda wazi, au makemikali ya kwenye vyakula au ndio kama sodoma na gomola
 
Kwa hiyo wanaofanya mapenzi kama Adamu na Eva, wanafanya kimbele na maumbile au kisahihi na maumbile?
 
Niilishiriki Tamasha la Jinsia 2009 kwenye viwanja vya TGNP Mabibo toka tarehe 8 hadi 11 Septemba mwaka huu. Kusema kweli kuna mada moja ambayo ilinigusa sana nayo ilikuwa ni kuruhusu mtu kujichagulia maumivu au raha kwenye masuala ya mapenzi. Katika mada hii lengo ilikuwa ni kuwapa MASHOGA NA WASAGAJI pamoja na MACHANGUDOA kuwa na uhuru wa kufanya wafanyacho pasipo kubugudhiwa.

NB: Kusema kweli binafsi yangu nilijisikia vibaya sana na nilihuzunika sana kwa historia hii ambayo kwa dunia ya sasa ya YATIMA wengi tunaweza kuwa na mashoga wengi sana hapo mbeleni kama tutaendelea kuwa na wazazi na walezi mabaradhuli kama baba mkubwa wa kijana huyu niliyemfahamu

Mkuu Sipo, hili tatizo sio tu kwa mayatima. Hili tatizo kimsingi litakuwa kubwa sana kwa jamii zetu hizi za kimasikini. Hebu fikiria wewe umejenga au umepanga nyumba yenye vyumba vitatu (waati mwingine sio umasikini bali fashion). Chumba kimoja cha kwako na mkeo, kimoja cha watoto wa kiume na kingine cha watoto wa kike. Tatizo linakuja pale anapokuja mgeni. Mara nyingi akija mgeni wa kiume huwa familia nyingi zinakuwa na tabia ya kumkaribisha kwenye chumba cha watoto wa kiume. Sasa hebu jaribu kufikiria, iwapo huyu mgeni ni basha na mwanao wakiume huwa analala peke yake chumbani na kuna kitanda kimoja tu, nini kitatokea hupo chumbani utakapochanganya chui na mwanakondoo bila wewe mwenyewe kujua?

Vivyo hivyo kwa watoto wa kike. Achilia mbali mgeni, mara nyingi huwa tunawaweka chumba kimoja na wahudumu wa nyumba (house girls). Je kama huyo mhudumu ni msagaji na analala chumba kimoja na mtoto wako nini kinaendelea huko? Watoto wengi wameathirika kwa njia hii. Wewe unaamini kuwa huyo mgeni ni shemeji yako (tumbo moja na mumeo/mkeo) kumbe ni simba mla watu

Jamani tuwe waangalifu, umasikini wetu usije ukatupeleka pabaya. Kama ikibidi kuchanganya watoto na watu wazima, tujaribu kuwa tunafanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kuzuia kabla tabia haijaota mizizi. Vinginevyo,mazoea haya inabidi tuyaache mara moja.
 
...alipompata mpenzi na kugundua kuwa ana tena nguvu za kiume na alipokwenda hospitali na kumweleza daktari ukweli daktari alimjibu kuwa kutokana na vitendo alivyofanya vya kishoga haotokuwa na uwezo tena wa kuwa na nguvu za kiume maishani mwake...

...Na tokea hapo ndipo aliendelea kufanya kazi hii hadi leo.

NB: Kusema kweli binafsi yangu nilijisikia vibaya sana na nilihuzunika sana kwa historia hii ambayo kwa dunia ya sasa ya YATIMA wengi tunaweza kuwa na mashoga wengi sana hapo mbeleni kama tutaendelea kuwa na wazazi na walezi mabaradhuli kama baba mkubwa wa kijana huyu niliyemfahamu
Hii habari niliwahi kuisikia kabla, ila ilkuwa kenye format tofauti kidogo, anyway... Kwa kuwa ulizungumza naye na kumuonea huruma (Kama si huruma za mamba) je ulimshauri kitu huyo schoolmate wako!?
 
Back
Top Bottom