Mashoga na Wasagaji Waruhusiwa Kuliongoza Kanisa Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashoga na Wasagaji Waruhusiwa Kuliongoza Kanisa Marekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Wawakilishi wa kanisa la kiinjili la kilutheri la nchini Marekani wakipiga kura kuruhusu wasagaji na mashoga kuwa wachungaji na viongozi wa kanisa

  Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani limepiga kura na kuruhusu wasagaji na mashoga kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini humo. Uamuzi huo wa kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na viongozi wa makanisa ya kilutheri nchini Marekani unaonekana kuzusha mzozo na unaweza kuwagawanya wanachama wake milioni 4.6 waliopo nchini humo.

  Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani (ELCA) ambalo lina dayosisi zipatazo 10,000 nchini Marekani, lilipiga kura ijumaa jioni kubadilisha baadhi ya vipengele na kuwaruhusu mashoga na wasagaji kuwa wachungaji na pia kuwapa nafasi za kuwa na vyeo mbali mbali kwenye makanisa.

  Baada ya majadiliano makali, wawakilishi wa kanisa walipiga kura 559 za kuunga mkono kulinganisha na kura 451 zilizokuwa zikipinga wazo hilo, alisema mkurugenzi wa habari wa kanisa hilo John Brook.

  Kanisa la kiinjili la kilutheri la Marekani sio la kwanza nchini Marekani kutoa uamuzi huo wa kuwapa mashoga na wasagaji nafasi za uchungaji na uongozi katika makanisa. Kanisa la Episcopalian la nchini Marekani lilishawahi kutoa uamuzi kama huo.

  Hata hivyo uamuzi huo wa kanisa la kilutheri la Marekani haukupita kirahisi, kwani kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa wachungaji mbali mbali akiwemo mchungaji Richard Mahan wa dayosisi ya Maryland magharibi, Virginia.

  "Siwezi kuamini kanisa ambalo nimelijua kwa zaidi ya miaka 40 linaweza kuruhusu vitu ambavyo mungu alivipinga" alisema mchungaji Mahan na kuongeza "Hakuna sehemu yoyote katika maandishi ambayo inasema watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja au watu wanaofunga ndoa za jinsia moja wanakubalika mbele ya mungu".

  Kwa upande wa watetezi wa uamuzi huo akiwemo askofu Gary Wollersheim wa dayosisi ya Illinois kaskazini walisema kwamba uamuzi huo ni sahihi.

  "Ni uamuzi wa kutoa haki kwa wote, ni uamuzi ambao yesu angetutaka tuuchukue" alisema askofu Wollersheim


  Source: nifahamishe.com
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,010
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu,

  ..kwenye mjadala mwingine X-Paster aliniambia kwamba Uislamu ni dini inayosambaa kwa kasi sana duniani na haswa ktk mataifa ya magharibi.

  ..swali langu kwake lilikuwa ana uhakika gani Uislamu hautapata matatizo na misukosuko inayoipata imani ya Kikristo ktk mataifa ya magharibi.

  ..hawa wenzetu ushoga ni utamaduni wao. sasa ukiwapelekea Dini/Imani yoyote ile wanajaribu kutumbukiza mambo yao machafu humo.

  ..hata huku kwetu AFRIKA wako Wachungaji na Mashekhe wengi tu wana imani za kishirikina kwa sababu huo ni utamaduni wa Mwafrika.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  JokaKuu Lakini İmani ya hao Wachungaji na Masheikh ya Ushirikina imekatazwa katika Vitabu vyao Vya Dini Biblia na Qur-ani sasa wasiingize hao Wachungaji na Masheikh Dini na mambo ya Kishirikina upo na mimi joka Kuu?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nyakati za mwisho zina mambo! Wengi wamejitenga na imani na kusikiliza mafundisho ya shetani! Yaliyotokea Sodoma na Gomora naona wameyasahau!
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hakika huu ndio mwisho wa Duniya.

  Eeh Allah tuepushe na hayo sisi na vizazi vyetu.
   
 6. Koiya

  Koiya Member

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Yaani huu ndio wakati wa kukesha tukiomba maana dunia inakwenda mrama bila kuomba msaada wa mwenyezi mungu tutaangamia wote, si unajua samaki mmoja akioza ni wote.
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Abdulhalim Upooooooo hapo?
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  JokaKuu, Rafiki lazima utambue kuwa kuna tofauti kati ya Uislam na Muislam, Mkristo na Ukristo.

  Unaweza kuwapata Mashoga kwenye imani za dini zote na hata kwa wale wasio na dini hapa duniani. Lakini linapokuja suala la Imani ya dini fulani kukubali na kuhukumbatia ushoga na usagani na kuuona kuwa ni jambo lenye kukubalika, inabidi tujiulize mara mbili mbili, kulikoni!?

  Uislam upo wazi kabisa katika suhala hili la ushoga.

  Amesema Mtume (Salla Allahu, Alayhi Wasallam)

  Anayefanya kitendo cha kaumu Lut muuweni anaefanya na anaefanywa...

  Albani katika Sahih Tirmidhiy

  Nathubutu kusema kwamba, Tabia hii imezidi kujiimarisha na kulazimisha kukubalika katika jamii za kimagharibi na haswa wakristo, mpaka kufikiwa kupatikana kwa maaskofu na mapadri mashoga, na sasa imetungiwa muswada washeria kuzilinda hizi tabia chafu za kikristo na kuanza kusomeshwa mashuleni, mfano: Uingereza.

  Tayari ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa ambapo wakristo wanaume wanaweza kuoana wenyewe kwa wenyewe. Vile vile wanawake wa kikristo wanaweza kuoana wenyewe kwa wenyewe na sasa linakuja hili la watoto waelimishwe kuikubali hali hii kama sehemu ya maumbile na wasijenge tabia ya kuwatenga kwani nao ni sehemu ya jamii...!

  Ni dhahiri kuwa zile hadithi zinazoelezea zama za mwisho na mporomoko wa maadili zinathibitika hivi leo. Hadithi moja inasema kuwa kutoweka kwa aibu katika dhambi ya ukahaba ni dalili ya kiama:

  Kutashitadi maingiliano haramu ya kijinsia wazi wazi
  (Bukhari).

  Saa hiyo itafika wakati uzinzi utakapokuwa umeenea sana
  (Al-Haythami, kitab al fitan)

  Kufifia kwa maadili na hisia ya aibu kunaelezwa kwa maneno haya:

  Saa ya mwisho haitasimama hadi pale watu watakapofanya uzinzi njiani (njia wanazopita watu)
  (Ibn Iban na Bazzar).
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,010
  Trophy Points: 280
  X-PASTER,

  ..kwa uelewa wangu ni kwamba imani hizi za Uislamu na Ukristo zinakataza kabisa zinaa, pamoja na masuala ya kuingiliana kinyume.

  ..lakini kuna siku uliwahi kuniambia ktk majadiliano yetu hapa na ukanitumia link hapa hapa jamii forms ikielezea kwamba Waislamu wanaongezeka kwa kasi kubwa Marekani na Ulaya Magharibi.

  ..swali langu kutokana na maelekezo ya taarifa ulizozileta ni kwamba: kwa kusambaa kwake Marekani na Ulaya je Uislamu hausumbuliwa na hizi tamaduni za kuingiliana kinyume kama ambavyo Ukristo unasumbuliwa sasa hivi?

  ..binafsi nimeshaona documentary ya mwanamke Muislamu toka Pakistan anaishi Canada ambaye anahoji kwanini wanawake wanatenganishwa na wanaume wakati wa swala. zaidi anahoji kwanini wanawake hawaruhusiwi kuongoza swala mbele ya wanaume wakati wanafanya kazi za kila aina huko mitaani.

  ..halafu tatizo la hawa mashoga mwanzoni hujificha, sasa wakishapata kuaminiwa na kupanda ngazi za kimadaraka ndiyo wanajitokeza. kuna Askofu alijificha mpaka alipostaafu ndiyo amekuja kulipua bomu. kuna wengine wanaoa kabisa halafu wanakuja kuzitelekeza familia zao.

  ..kwa hali ya kidunia ilivyo sasa hivi Ukristo umetekwa nyara na mashoga Marekani na Ulaya magharibi. Uislamu nao umetekwa nyara na magaidi Asia na mashariki ya kati.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hayo ni maoni yako, ila kwa kukumbusha tu, hao magaidi chanzo chake ni hizo hizo siasa za kimagharibi.

  Wamarekani na rafiki zake siku watakapo wacha ugaidi wa kuvamia nchi za watu kijeshi ndio siku ambao hatutaona tena ili suala lililo pewa jina la ugaidi.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,010
  Trophy Points: 280
  X-PASTER,

  ..unaweza kuelekeza lawama kwa Wamarekani. lakini hudhani kwamba hao Waislamu wanaosumbuliwa na Wamarekani wanapaswa kuinusuru/kuihifadhi/kuitenganisha/kuitofautisha dini yao na vitendo vya kigaidi?

  ..hata Wapalestina walianzisha PLO na walitenganisha dini na harakati zao za kukomboa ardhi yao. sasa nini kilichotokea mpaka kuanzishwa kwa Hamas na Hizbollah? kwanini wasianzishe chama kingine tu bila kutumbukiza dini humo?

  ..Shekhe anayehubiri Ugaidi waziwazi amevamia na anachafua Uislamu, sawasawa na Mchungaji anayehubiri ushoga na kuingiliana kinyume alivyovamia na anavyouchafua Ukristo.

  ..anyway, those are facts on the ground as i see them. naamini Dini zote ni safi, tunaozichafua ni sisi waumini.
   
  Last edited: Aug 24, 2009
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hao Hamasi na Hizbollah waanzilishi wake ni hao hao wayahudi. Kama vile ilivoanzishwa Alqida na wamarekani.

  Wametengeneza zimwi linalowala wenyewe.
   
 13. s

  shabanimzungu Senior Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwanawe this world is free let them enjoy themselves! Later they burn in hell anyways
   
Loading...