Mashitaka 8 kati ya 9 'tupa kule' kesi ya kupinga matokeo ilemela, kesi yahairishwa walalamikaji wai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashitaka 8 kati ya 9 'tupa kule' kesi ya kupinga matokeo ilemela, kesi yahairishwa walalamikaji wai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  TUESDAY, OCTOBER 18, 2011

  MASHITAKA 8 KATI YA 9 'TUPA KULE' KESI YA KUPINGA MATOKEO ILEMELA, KESI YAHAIRISHWA WALALAMIKAJI WAINGIA MITINI
  [​IMG]

  Wakili Tundu Lisu akitoa maelezo ya mwenendo wa kesi hiyo huku mteja wake Mbunge Highness Samson (wapili kuia) akimsikiliza kwa makini.

  Kesi namba 12/2010 yakupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la ilemela mkoani Mwanza iliyompatia ushindi mbunge kupitia tiketi ya CHADEMA bw. Highness Samson imeahirishwa tena leo jioni katika mahakama ya rufaa jijini humo.


  [​IMG]

  Wakili T. Lisu (kulia) akiwa ameambatana na mteja wake mbunge H. Samson wakitoka kwenye ukumbi wa mahakama.

  Kati ya mashitaka tisa yaliyofunguliwa dhidi ya mbunge wa sasa wa Ilemela mashitaka nane yametupiliwa mbali na kubaki shitaka moja tu ambalo ni dai la watu wapatao laki moja na elfu kumi na nne kudaiwa kuzuiwa kupiga kura.


  [​IMG]

  Shitaka hilo lililosalia linaonekana kukosa nguvu kwani linafananishwa na kesi ya uchaguzi ya mwaka 1995 ya bw. Silvester Masinde na Pius Msekwa, ambapo Mahakama ya Rufaa Tanzania iliamuru kuwa kura ambazo hazikupigwa au hazikuhesabiwa kugawanywa kwa uwiano wa asilimia walizopata wagombea kwenye uchaguzi.


  [​IMG]

  Mashitaka nane yaliyofutwa ni pamoja na kufanyika kampeni kwenye vituo vya kupigia kura na makanisani siku ya kupiga kura, wafuasi wa chadema kuzuia watu wasipige kura, mgombea wa chadema na mawakala wake kutoa rushwa kwa kujenga visima kwa wapiga kura na kutoa vinywaji na vyakula kwenye misiba, mahela yalitolewa kwenye eneo la Manguruwe, mshtakiwa mbunge pamoja na mawakala wake walinunua shahada za wapiga kura, kulikuwa na mabadiliko ya vituo vya wapigia kura vituo vya soko la Kirumba na kwenye viwanja vya Furahisha, jingine ni kuwa kuna mawakala wa Sangabuye na Buhongwa hawakula kiapo cha kutunza siri.


  [​IMG]

  Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Fish' akiteta jambo na mh. mbunge na wakili wake mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ambapo inategemewa kusomwa tena Ijumaa hii 21oct2011.


  [​IMG]

  Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura
  31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Namwamini sana tena sana TUNDU LISSU angalia kesi ya kupinga Ushindi wake ilivyo tupiliwa mbali tena hatua ya kwanza kabisa
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Magamba fitna zitawaua, wasicheze na peoples power!
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Habari nyingine zinashangaza sana! Yaani ccm wanalalamika wananchi kuhongwa msosi, kuzuiliwa kupiga kura, mawakala kula kiapo, kununua shahada, kujengewa kisima! Kama walijua ni makosa na wamefungulia mashtaka huko mwanza ilikuwaje wakayafanya hayohayo Igunga. Wao walivyokuwa wanagawa mahindi na kununua shahada huko Igunga huku wakijua ni makosa walikuwa wanategemea nini kwenye kesi baadae!? Huu si ujinga wa Abunuasi wa kukata mti uliokalia!? Shame on U!
   
 5. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hadi kieleweke.
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kila kitu wanataka wao, CCM bwana
   
 7. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  We are a winner always
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wadau hapo kwenye red naona kama vile panahusika nchi nzima. hawa jamaa walipiga kampeni kwenye masinagogi kwa kenda mbele nchini kote. Angalia sehemu kubwa ya majimbo waliyoshinda, wengi wa wapiga kura wanahusika sana na hilo. Ndugu zangu niwaase na niiase nafsi yangu, hii ni hatari iliyoko mbele yetu. mdharau mwiba......
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Suala kubwa na gumu zaidi....kwa CDM ni kujipanga na kuwa wamoja kuelekea 2015 maana najua mamluki wapo na watajitahidi kuharibu...chama kudhoofisha la sivyo naona wabunge nusu kwa nusu uchaguzi ujao!!demokrasia kwenda mbele
   
Loading...