Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro awamu ya nne Stephen Mashishanga ameitaka serikali ijitathimini upya kuhusu matukio ya mauaji yanayotokea Kibiti Pwani.
"Ni aibu kwa kinachoendelea. Serikali iangalie imekosea wapi au wananchi wake wamefanya nini hadi hali hiyo ikatokea na ikomeshe matukio hayo kabla hayaleta madhara makubwa".
Hadi sasa zaidi ya watu 31 wameshauawa wakiwemo,
Viongozi 15 wa serikali za vijijini na makada 3 wa chama cha mapinduzi.
Polisi 10 na askari 3 wa Maliasili wakiwemo raia 3 wa kiume waliovalia vazi la baibui.
Akizungumzia chanzo Mashishanga alisema, "Wakati mwingine viongozi wanajisajau katika maamuzi yao. Bila kujua wanaweza wakawa wanapandikiza chuki na kusababisha kisasi ambacho kinaweza kuhusisha vifo vya namna hii".
Hongera Mashishanga angalau wewe umelisemea hili viongozi wengine wameogopa hata kulizungumzia akiwemo mbunge wao, Ally Ungando (CCM), amegoma kwa kuhofia usalama wa maisha yake.
“Sina comment yoyote juu ya mauaji hayo kwa sababu hata mimi ni binadamu nahofia usalama wangu pia vilevile,” alinukuliwa Ungando(MB) akisema kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
Gambo na Bashite waangalie wasidhani uonevu wanaowafanyia watu wasio na hatia wananchi watavumilia siku zote.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi.