Mashirika ya Umma Tanzania: Yapi bado yapo, yapi yamekufa na Kwanini?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,245
Wana JF,

--Hivi Tanzania yetu itakuja tena kuwa na mashirika mapya ya Umma?

--Ni yapi mashirika ya Umma yaliyokufa?

--Ni yapi mashirika ya Umma yaliyokufa lakini yakafufuliwa na kubakia mashirika ya Umma?

--NI yapi mashirika ya Umma yaliyoteteleka na kubinafsishwa na asilimia kubwa ya hisa kuwa ya watu binafsi, na ni yapi asilimia kubwa ya hisa imekuwa ya Umma?

Najua kunasababu kemkem na nyingi ni zenye kero katika jamii zinazo au zilizo sababisha mashirika ya Umma kuporomoka.

Naomba mawaidha yako katika haya mashirika, orodha ya mashirika au habari yoyote itakayoweza kutoa mwangaza kuhusiana na mashirika haya.

Na kama nyongeza tu, je Serikali yetu imejifunza nini kuhusiana na mashirika haya/hayo? Je, Kama wewe umehusika katika kuporomoka kwa shirika la Umma hivi sasa ukiangalia nyuma unajisikiaje, je ulijiuzulu, uling'ang'ania mpaka shirika likafa au basi hatua zipi ulichukua?


SteveD.
 
Mimi Kama Mtanzania Ninaye Lipa Kodi Naniana Uchungu Na Nchi Yangu Naomba Kuuliza Swali Kuhusu Mashirika Ya Umma Kama Tumebinafsisha Mashirika Yaha Lakini Mikataba Ina Mwisho Au Mpaka Mitambo Ichoke Ndio Waturudishiye Kwa Mtizamo Wangu Naona Viongozi Wetu Bado Hawajui Wafanye Nini Mpaka Sahizi Kuhusu Uchumi .nchi Yeyote Ile Inajengwa Na Mwenye Inchi Sio Mgeni Nawaomba Viongozi Wangu Hizi Zawadi Mbaya Sana Kwamfano Mwaka Flani Tanzania Ilipata Janga La Njaa Harafu Viongozi Wetu Wanaenda Kuomba Msaada Wa Chakula Sasa Hapo Tutakuwa Tumetibu Janga Au Tumeongeza Pole Sana Ila Ipo Siku Tutaamka Sisi Vijana
 
Nimesoma IPP kuwa serikali inataka kuagiza magari 200 yaendayo kwa kasi. Nakumbuka zamani kulikuwa na mradi wa UDA hivi hilo shirika bado lipo tena huko nyumbani? na linafanya nini kwa sasa?
 
Nimesoma IPP kuwa serikali inataka kuagiza magari 200 yaendayo kwa kasi. Nakumbuka zamani kulikuwa na mradi wa UDA hivi hilo shirika bado lipo tena huko nyumbani? na linafanya nini kwa sasa?

..uda ipo,ila haina mabasi mengi kama zamani. siku hizi wanakodisha makampuni kuchukua wafanyakazi. nasikia linaendeshwa kwa faida.
 
Nyerere ambaye ndiye alianzisha pasipo a feasible and sustainable plan to maintain and manage
 
Guys,kama kuna kitu hupaswi kumlaumu Nyerere basi ni kwenye mashirika ya umma.

Tatizo viongozi wengi alikuwa anafikiri ana-share nao vision (maono) kumbe walikuwa wanamsanifu tu na ndiyo hao waliokuwa wanayafilisi mashirika ya Umma.

Mpaka leo kwenye mashirika machache yaliyopo,wanaoongoza kuyamaliza mashirika hayo ni viongozi wa kisiasa. Sasa kumlaumu Nyerere kwenye kufa kwa mashirika ya umma si sahihi kabisa.

Tatizo la msingi ni kwamba Nyerere hakupata watu sahihi wakumsaidia kutekeleza kwa vitendo mawazo yake.
 
Wakulaumiwa ni Umma mwenyewe.
Umma siku zote haoni uchungu kuendesha shirika kwa hasara kwa sababau shirika likifa umma anaendelea kupeta.
Shirika ni la umma, kwa nini lawama wapewe CCM?
Umma aulizwe ni kwa nini ameshindwa kujiendesha kwa faida?
Umma afikishwe Mahakamani kujibu tuhuma za uzembe.
Umma akipatikana na hatia afungwe jela milele na asiruhusiwe tena kuendesha biashara au kuwa na hisa kwenye shirika lolote.
Umma amejidhihirisha wazi kwamba uwezo wake wa kuendesha mashirika ni mdogo au haupo kabisa.
Hivi lilikuwa wazo la nani kumpa umma mashirika yote?
Zamani zile walikuwako wengine walioendesha mashirika aliyopewa yeye kwa faida lakini bado walinyang'anywa akapewa yeye umma.
Hivi umma alipewa mashirika hayo kwa sababu ya uwezo wake au kwa sababu za kisiasa?

Je umma alaumiwe peke yake au yupo mwingine wa kubeba lawama zote za umma?

Umma ndiye wa kulaumiwa kwa kushindwa kuendesha mashirika yake.

Amen.
 
Kumekuwepo na ufanisi duni katika mashirika ya Umma mengi ambayo serikali emeendelea kuyamiliki. Mashirika ya aina hii yamekuwa yakiongezea nchi mzigi ambapo mara kadhaa yamekuwa yakifanyiwa bail out au hata kupewa ruzuku ili majina yao yasibaki kuwa ndoto. Machache ni kama TANESCO, TRL, ATCL, NIC nk. Ingawa taarifa zinaonyesha hasara TANESCO imepungua.
Serikali kwa upande wake imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuepusha kuyachangia mashirika haya mara kwa mara kama kuyabinafsisha na wakati fulani hata kukodi menejiment.
Msingi wa hoja yangu ni kwamba pamoja na udhaifu wa serikali katika usimamizi na kuingiza siasa katika utendaji( pesa za NIC kusaidia kwenye SIASA na kuajiri bila kufuata mpangilio kama ilivyo kwa TRL na mikataba mibovu ya TANESCO) bado kwa kiasi kikubwa saaana Watanzania kwa kiasi kikubwa saana ndio wanaouwa haya mashirika na kuanza kupiga kelele. Mf ukisafiri kwa treni kwa njia ya kati utakutana na wale wanaoitwa TT ambao nao wanawatoza watu pesa bila tiketi, unajiuliza tunaelekea wapi.
Nadhani sasa ni lazima tuwe wakweli Watanzania na sisi tuache kuishi maisha ya kuwaza kuibaiba na kutoaminika. Tubadilike kwa kweli. Tutajua saaana kulalamika lakini tunafanya nini tukipewa nafasi.
Kifupi; Nchi yetu ipo hivi kama tunavyoiona kwa sababu yetu wenyewe hatutaki kuwajibika
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keisy Mohamed (CCM) ametaka walioua mashirika ya umma wakamatwe, wanyongwe.

Mbunge huyo amesema bungeni mjini Dodoma kuwa, walioua mashirika ya umma ni wauaji kwa kuwa matendo yao yamesababisha wananchi wapoteze maisha kwa kukosa huduma.

Mohamed amesema, kuna sheria mbaya nchini zinazolinda wezi na kwamba, kama walioua mashirika ya umma wamekufa, pingu ziwekwe kwenye makaburi yao.

Keisy pia amesema, uamuzi wa Serikali kutumia chenji ya fedha zilizotumika kununulia rada kununua vitabu ni ufisadi.
Mbunge huyo amesema bungeni kuwa, fedha hizo zipelekwe kwenye halmashauri zitumike kununua madawati. Kessy amehoji, walioingia mkataba wa kununua rada wapo wapi?

MY TAKE:
Haya CCm mnayoyaongea mko tayari kutatekeleza au ni porojo tu muda uishe mlambe posho msepe????

Source: HABARILEO


 
Mhebunge ameshauri bungeni kuwa mafisadi na wahujumu uchumi wanyonge. Wabunge wengi wameonekana kumshangaa kwa msimamo wake huo. WanaFJ, mnasemaje?
 
Ninamuunga mkono 100% kwani isipodhibitiwa hii hali watapora na kukuuza rasilimali zote za nchi. Nchi kama China imefanikiwa kwa kuwa na sheria za namna hii.
 
Hilo tumelizoea kulisikia ndani ya hili Bunge letu na mbunge anavyoamua kulisema hilo hakuna tofauti na ngonjera kama bunge lingekua na dhamira ya dhati juu ha hili sheria ingetungwa na ndo tungeweza kuona ukweli wa suala lenyewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom