Mashirika ya Ujasusi ya Urusi yana nguvu sana kwa sababu ya kukabiliana na mshirika ya ujasusi makubwa hapa dunianai kwa wakati mmoja na hata jeshi

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Wakati wa vita baridi cold war pamoja na mashindano ya kutngeneza silaha kali duniani weapons race, mashirika ya ujasusi yalikua yakichuana vikali sana,hasa pande mbili kati ya USSR na USA.USSR ilikua na washirika wake wa Warsaw Pact,na USA ikiwa na washirika wake wa NATO.

Kwa hali hiyo kila upande ukifanya jambo fulani upande mwingine unapinga kwa kila namna.Hali hii ilipelekea ujasusi mkubwa kutamalaki baina ya pande hizi ,kuchunguzana,kuibiana siri,kuhujumiana.

Hali hiyo ilipelkea URUSI kupambana na majasusi wa Marekani na washirika wake,baadhi yao ni
majasusi wa USA vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa Uingereza vs KGB,GRU,SVR etc

Majasusi wa ujerumani magharibi vs KGB,GRU,SVR etc

Majasusi wa Israel vs KGB,GRU,SVR etc

Majasusi wa Pakistan vs KGB,GRU,SVR hapa ni wakati wa vita ya USSR nchini Afghanistan etc

Majasusi wa NATO vs KGB,GRU,SVR etc

Majasusi wa China vs KGB,GRU,SVR hapa ni wakati wa vita ya USSR nchini Afghanistani

n.k
Wakati wa vita ya USSR dhidi ya Mujahidin nchini Afghanistan USSR ilikua inapigana na mujahidini waliokua wakipewaa sapoti ya silaha, ujasusi na fedha na mataifa ya USA,UK,NATO,China,Pakistan,Saudi Arabia etc

Hawa wote walikabilana ana kwa ana vikali sana na KGB,SVR ,GRU etc.
Nahitimisha kusema kuwa inawezekana kuwa Urusi ina majasusi imara na jeshi imara sana kuliko nchi yeyote ile.

Marekani ilikua ikitoa silaha kali sana kuwapa mujahidini kuangamiza magege na vifaru vya USSR/URUSI,sio tu Marekani bali pia nchi nyingine zilitoa fedha silaha na ujasusi mfano ni china,pakistani,saudia,na baadhi ya memba wa NATO.

Hii inaonesha kuwa huenda Urusi ina jeshi kali na imara sana na ujasusi imara na makini sana.

UWEZO MWINGINE

Baada ya kuvunjika muungano wa kisovieti nchi nyingi zilizokua sehemu ya ya USSR zilizojitenga ziliondoka nasiri nyingi sana za muundo wa kijasusi na kijeshi wa USSR nyingi ziliuza siri hizo kwa US na wenzie,lakini Urusi ya sasa ikaja na miffumo mipya haraka ambayo wa west bado wanashindwa kupenya kirahisi,kijeshi na kijasusi,mfano Ukraine na Georgia n.k hawa watakua wametoa siri nyingi sana lakini haioneshi kuiathiri pakubwa RF-Russian Federation
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Na ikumbukwe kwamba MI6 haiichunguzi sana wala haiishambulii sana kijasusi marekani kama inavyoishambulia Urusi,vivyo hivyo kwa Mossad,na kwa majasusi wa nchi nyingine zote za west na NATO.Ikumbukwe kwamba mashirika makubwa ya kijasusi na yenye nguvu ni ya kutoka nchi za magharibi,na hayo yote hayapambani yenyewe kwa yenyewe bali yote hupambana na Urusi kwa kushirikiana ama mmojammoja kuishambuia Urusi,lakini yeye yuko peke yake.Hii yote inaonesha uwezo wa mfumo wa ujasusi wa urusi kukabiliana na mashirika mengi yenye nguvu kutoka west na allies wao.
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Kumbuka tukio feki la kuwekewa sumu yule mzee wa kirusi na binti yake waliokua wanaishi UK ni MI6 walihusika kwa ushirikianao na CIA lakini njama zao zilizimwa na majasusi wa Urusi kwa kuweka bayana yaliyotendwa nyuma ya pazia,na lengo lao hao west halikutimia.

Halikadhalika issue ya Ukraine inatupa mfano mzuri juu ya maoni yangu. Baada ya Marekani kufanikisha njama za kumuondoa Rais wa Ukraine aliyekuwepo kabla ya Poroshenko Urusi mara moja ikajua juu ya lengo lao na ikaitwaa Crimea maramoja na kuvuruga malengo yao.

Hapo pia nchi za west zikaungana na Ukraine kuanza hujuma za kijasusi dhidi ya Urusi na tukio la kuangushwa kwa ndege ya Malaysia lilitengenezwa ili kuichafua Urusi,lakin Urusi walilikabili na kulizima kikamilifu baada ya kugundua njama hizo.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,903
2,000
Wakati wa vita baridi cold war pamoja na mashindano ya kutngeneza silaha kali duniani weapons race, mashirika ya ujasusi yalikua yakichuana vikali sana,hasa pande mbili kati ya USSR na USA.USSR ilikua na washirika wake wa Warsaw Pact,na USA ikiwa na washirika wake wa NATO.
Kwa hali hiyo kila upande ukifanya jambo fulani upande mwingine unapinga kwa kila namna.Hali hii ilipelekea ujasusi mkubwa kutamalaki baina ya pande hizi ,kuchunguzana,kuibiana siri,kuhujumiana.hali hiyo ilipelkea URUSI kupambana na majasusi wa Marekani na washirika wake,baadhi yao ni
majasusi wa USA vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa Uingereza vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa ujerumani magharibi vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa Israel vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa Pakistan vs KGB,GRU,SVR hapa ni wakati wa vita ya USSR nchini Afghanistan etc
majasusi wa NATO vs KGB,GRU,SVR etc
majasusi wa China vs KGB,GRU,SVR hapa ni wakati wa vita ya USSR nchini Afghanistani
n.k
Wakati wa vita ya USSR dhidi ya Mujahidin nchini Afghanistan USSR ilikua inapigana na mujahidini waliokua wakipewaa sapoti ya silaha, ujasusi na fedha na mataifa ya USA,UK,NATO,China,Pakistan,Saudi Arabia etc
hawa wote walikabilana ana kwa ana vikali sana na KGB,SVR ,GRU etc.
Nahitimisha kusema kuwa inawezekana kuwa Urusi ina majasusi imara na jeshi imara sana kuliko nchi yeyote ile.
Marekani ilikua ikitoa silaha kali sana kuwapa mujahidini kuangamiza magege na vifaru vya USSR/URUSI,sio tu Marekani bali pia nchi nyingine zilitoa fedha silaha na ujasusi mfano ni china,pakistani,saudia,na baadhi ya memba wa NATO.
Hii inaonesha kuwa huenda Urusi ina jeshi kali na imara sana na ujasusi imara na makini sana.
Wa kwetu wanapambana na Mbowe....hahahaaa
 
Sela Son

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
947
1,000
Hakuna shirika la kijasusi lenye nguvu kama la Pakistan

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha ..Hawa Pakistani wanna Nini? Nawazkia Sana? Tujuzane cjwahi ckia chochote kipya walichofanya zaidi ya organization ya mujahidiin nchini Afghanistan dhidi ya wasoviet..
Isitoshe Hawa Ni mabingwa wa kufeli eg wameshindwa Vita zote zid ya India..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
12,296
2,000
Na ikumbukwe kwamba MI6 haiichunguzi sana wala haiishambulii sana kijasusi marekani kama inavyoishambulia Urusi,vivyo hivyo kwa Mossad,na kwa majasusi wa nchi nyingine zote za west na NATO.Ikumbukwe kwamba mashirika makubwa ya kijasusi na yenye nguvu ni ya kutoka nchi za magharibi,na hayo yote hayapambani yenyewe kwa yenyewe bali yote hupambana na Urusi kwa kushirikiana ama mmojammoja kuishambuia Urusi,lakini yeye yuko peke yake.Hii yote inaonesha uwezo wa mfumo wa ujasusi wa urusi kukabiliana na mashirika mengi yenye nguvu kutoka west na allies wao.
Theory nzuri .lakin si kweli kuwa wanamshambulia mrusi. UK, Mossad ni kuwaweka pembeni.. hawa hawana ugomvi mkubwa na mrusi isipokuwa tu america. Ukisema america hapo sawa.. ila sio kweli eti mashirika yote ya west yanamshambulia urusi. Hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Hakuna shirika la kijasusi lenye nguvu kama la Pakistan

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa,sasa hebu fikiria shirika hilo la Pakistani likishirikiana na Mossad,MI6,CIA na mengine kutoka NATO,au EU,yakiishambulia kijasusi URUSI,hapo unaionaje KGB? sisemi kuwa KGB iko juu ya ISI bali iko imara sana kuwakabili maadui wenye nguvu kama hawa wapakistani
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Theory nzuri .lakin si kweli kuwa wanamshambulia mrusi. UK, Mossad ni kuwaweka pembeni.. hawa hawana ugomvi mkubwa na mrusi isipokuwa tu america. Ukisema america hapo sawa.. ila sio kweli eti mashirika yote ya west yanamshambulia urusi. Hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hebu jaribu kufuatilia vizuri story za kweli za vita baridi utaona jinsi MI6,Iilivyokua inaipa tabu KGB,NA JINSI MI6 ilivyokua inabadilishana taarifa za kijasusi na CIA,pia fatilia jinsi MOSSAD ilivyokua inawashughulikia KGB na kuwapa taarifa muhimu sana CIA,kumbuka wakati wa vita baridi kulikua na vita nyingi sana baina ya Waarabu na Israel,kwa wakati huo Urusi ilikua ikiwapa sapoti waarabu kwa silaha kali ,kitu hiki kilikua kinamkera sana Israel,naye akawa anaichunguza Urusi na taarifa nyingine akawa anashea na CIA,MIFANO NI PAMOJA NA MAJASUSI WA Mossad KUIBA ndege MIG ya kirusi iliyonunuliwaa na IRAQ,NA KUWAALIKA wa MAREKANI KUIFANYIA UPEKUZI WA KISAYANSI.Kwa vile USA alikua upande wa Israel,USSR ikawa upande wa waarabu,na kwa vile USSR ilikua upande wa Waarabu inapelekea Israel kuwa upande wa USA na kwa hali hiyo Israel kupambana kijasusi na USSR ili kuhujumu urafiki wake na waarabu.
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Theory nzuri .lakin si kweli kuwa wanamshambulia mrusi. UK, Mossad ni kuwaweka pembeni.. hawa hawana ugomvi mkubwa na mrusi isipokuwa tu america. Ukisema america hapo sawa.. ila sio kweli eti mashirika yote ya west yanamshambulia urusi. Hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu pia angalia jinsi mashirika ya kijasusi ya nchi mojamoja ya nchi za NATO yalivyokua yakiifanyia Urusi ya zamani na ya sasa,shirka la ujasusi la ujerumani magharibi lilipambana sana na KGB,na huyu Putin alikua akiishi Ujerumani mashariki akikabiliana na majasusi wengi wa WEST waliokua wakifanyia shughuli zao West german.
 
lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,201
2,000
Wa kwetu wanapambana na Mbowe....hahahaaa
Mkuu majasusi wa kwetu ni wazuri sana,tena sana,ni kama ninavyoielezea Urusi dhidi ya mataifa yenye mashirika ya kijasusi yenye nguvu,ndio hivyo kwa majasusi wa Tanzania,unakumbuka wakati wa Ukombozi kusini mwa afrika? majasusi wetu waliiva sana kwa sababu ya kukabiliana na Makaburu,hawa jamaa makaburu ni noma kiujasusi na kijeshi,pia majasusi wetu walikabiliana na mabeberu wengine amabao walikua hawapendi sera za Nyerere,pia maadui majirani zetu akina Idi Amini.Mobutu seseko,Kamuzu banda,n.k,NA MAJIRANI WENGINE WALIOKUA na NIA MBAYA na sisi.Sasa hapa ndio ungeujua uwezo wa majasusi wetu.Kilichoharibu hapa kwa sasa ni kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi ya kisiasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom