Mashirika ya tanapa/ncaa yana kazi gani

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Ninafahamu mashirika ya TANAPA/NCAA kazi yake ni kusimamia hifadhi za taifa pamoja na hifadhi ya Ngorongoro. Kazi yao ni kusimamia kwa maana ya kutunza ili nature iendelee kuwepo ili wanyama waendelee kuwepo. Kazi ya kutangaza utalii wa nchi ni kazi ya TTB - Tanzania Tourists Board pamoja na makampuni yenyewe ya utalii.

Chakushangaza sasa hawa mabwana wa TANAPA/NCAA wanatumia pesa nyingi sana na muda mwingi kwenye kusafiri nje ya nchi kwa kisingizio cha kufanya marketing kitu ambacho si kazi yao.
 
Unachokisema ni kweli kabisa. Ila tatizo lipo kati ya TANAPA vs NCAA. Haya mashirika ni pinzani kwelikweli. TANAPA wanaona kama NCAA wangepaswa kua chini yao,wakati NCAA kwa kuingiza pesa mingi kuliko TANAPA wanakua na kiburi.Ivyo competing business interests ndo inawadrive hao TANAPA na NCAA kuingilia kazi ya TTB.
 
Jamaa wanalipana mishahara minono balaa!nafikiri baada ya BOT,TRA,TCRA ni wao kwa package nzuri!
 
Jamaa wanalipana mishahara minono balaa!nafikiri baada ya BOT,TRA,TCRA ni wao kwa package nzuri!

Kiongozi ujue pia mazingira ya kazi pia ni magumu sana. Usilolijua ni kama usiku wa giza...
 
Kiongozi ujue pia mazingira ya kazi pia ni magumu sana. Usilolijua ni kama usiku wa giza...
Hakuna kazi yoyote ys maana wanayofanya. Kazi kupiga soga tu maofisini. Wewe lazima ni mmoja wao na tukikuomba job description huna.
 
Back
Top Bottom