Mashirika ya ndege yamepokea dola bilioni 123 kama msaada wakati ya mzozo wa COVID-19

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Serikali mbalimbali duniani zimetoa dola bilioni 123 kuyasaidia mashirika yao ya ndege yaliyoathirika na janga la virusi vya corona, shirika la kimataifa la usafiri wa anga IATA limeripoti jana.

Wakati asilimia 45 ya fedha hizo zilikwenda katika ruzuku ya mishahara, gharama za mitaji pamoja na unafuu wa kodi, kiasi kilichobaki cha asilimia 55 ni mikopo ya serikali ambayo inapaswa kulipwa, shirika hilo limesema katika mkutano na waandishi habari mjini Geneva.

Serikali zinapaswa kuelewa kuwa mzigo huu wa madeni yanayoongezeka utakuwa na madhara yake, mtendaji mkuu wa IATA Alexandre de Juniac amesema.

Ameonya kwamba hali hii itafanya hali ya ufufuaji kuchukua muda mrefu na ngumu.

Shirika hilo linakadiria kuwa mashirika ya ndege duniani yatabeba deni jumla la dola bilioni 550 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ikiwa ni ongezeko kutoka deni la bilioni 430 mwishoni mwa mwaka 2019.
 
Back
Top Bottom