Mashirika ya mifuko ya Jamii.... Ni kupe! Mnanyonya wananchi na kujinufaisha wenyewe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashirika ya mifuko ya Jamii.... Ni kupe! Mnanyonya wananchi na kujinufaisha wenyewe!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, Jun 12, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,246
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kuangalia haya mashirika ya mifuko ya jamii nakugundua kuwa ni wadharimu wanyonyaji wakuu wa wananchi!!
  haiwezekani mwananchi achangie pesa yake na yeye asifaidike!!
  Na wakati walumlipa unampa pesa ile ile aliyoiweka bila hata kumwongezea riba!!Wanatudanganya na kupewa masaada wa mazishi kuna mtu anahitaji kuzika??kama siyomatusi nini?Waweke utaratibu wa matibabu kwa insurance kama kweli wanataka kuwajali wanachama wao!
  SWALI:
  *Kodi mnazozipata kutokana na majengo zinafanya kazi gani??
  *Mwananchama anafaidika vipi na vitega uchumi hivi?
  *Je CAG anaenda kukagua kodi mnazokusanya kwa mwaka??
  *Kwanini mfanyakazi anapo staafu asipewe angalau riba kwa pesa yake aliyoiwekesha tangu aanze kuchangia!!

  SERA
  :
  *Sera za kukopesha wananchi zinasemaje je zinahitaji kurekebishwa??
  *Je ni lazima kuweko na ulazima wakustaafu ndo upewe pesa yako?kwanini unapoacha kazi usipewe pesa yako bila ya shariti lolote??
  *Iangaliwe upya kuwepo na ongezeko la thamani kwa kila pesa ya mwananchama.
  *Na mabenki yaanzishe akaunti za uzeeni unaweka pesa inakuwa inakuwa ila unakuwa uwezi kuitoa mpaka hapo utakapo staafu au kuacha kazi.

  hii imifuko nilazima ibadilike ili kwenda na wakati kuliko kuwa mifuko ya wakubwa pekee ndiyo wanaruhusiwa kukopa badala ya wanachama.
   
 2. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  si lazima mpaka ustaafu ndio ukachukue mafao yako hata unapoacha kazi from one organisation and move to another one unaweza kwenda kufuata mafao yako endapo utapata barua ya huidhinisha kuacha kazi kwenye hilo shirika la kwanza. My sister do that hapo ni barua tu kutoka shirikani then unapewa chako #KakaKiiza

  [HR][/HR]
  Nimetafuta Kazi,
  Nimepata Kazi,
  Sitaona Kazi,
  Kufanya Kazi
  :coffee:
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nchi itajengwa na wenye moyo italiwa na wenye Meno na ambao sikuhizi ukiwagusa utasikia wananionea mimi kwa sababu mimi ni....... kuhalalisha Ubadhilifu wao,
   
 4. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,491
  Trophy Points: 280
  Kwa NSSF kuna riba ya 1.8% kwa mwaka ambayo unatakiwa ulipe
  Kwanza hawatangazi hiyo riba mimi nilipata baada ya kuwafatilia kwa karibu lakini watu wengi hawajui kama wanapaswa kulipwa hiyo riba
  Kama wanachama wengi hawalipwi hiyo pesa inaenda wapi
  Hiyo riba ni ndoigo kulinganisha na riba za kibenki kama wanawekeza pesa yako na hawakupi hisa kwanini watoe riba ndogo namna hiyo
  shirikisho la wafanyakazi pamoja na kuwa na mwakilishi kwenye bodi za mifuko hifadhi ya jamii lakini hawajahi kutoa tamko llolote badala yake wamekuwa weakipiga kelele za kuongezwa mishahara bila ya kulinda maslahi ya wafanyakazi
  unapoenda kuchukua pesa yako hawakupi kwa wakati,jeuri njoo kesho nyingi na kumbukumbu zao hazipo sahihi
   
Loading...