Mashirika ya hifadhi ya jamii yalindwe kwa nguvu ya uma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashirika ya hifadhi ya jamii yalindwe kwa nguvu ya uma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Mar 16, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mashirika haya NSSF, PPF, PSPF na mengine yenye muundo kama huo yanatakiwa kulindwa kwa nguvu zote hata kama ni kwa maandamano kuanzia sasa ili kuepusha ukwapuaji wa pesa ambao uko mbioni kufanywa na Serikali pamoja na CCM.

  Baada ya ukosefu wa pesa serikalini kutokana na uongozi mbovu na matumizi ya kijinga sasa serikali na CCM wanatafuta pesa popote pale zilipo harari ama haramu. vyombo hivi viwili kama kawaida yao na hasa kama vilivyolifirisi shirika la Bima la Taifa (NIC), na kukwapua Mapesa kutoka BOT apo nyuma na kwa sababu hawawezi kurudi uko na kufanya ushenzi wao sasa wanayatolea macho mashirika haya ya hifadhi za jamii.

  Hizi kauli za Jakaya za kutaka kulipa wazee wa Africa Mashariki na nyingine nyingi za kimatumizi zitakazoanza kutolewa hivi punde na hasa baada ya kuanza kuisonta CHADEMA juu ya vyanzo vya mapato yake na kwa sababu watanzania wanatabia ya kushangilia mambo ambayo kwa juu yamepakwa rangi nzuri za kizalendo, utu, maendeleo na uungwana ni utangulizi tu wa ukwapuzi wa mapesa kutoka kwenye taasisi hizi.

  Na zaidi, msukumo wa ukwapuzi huu ni sababu zote walizonazo CCM na serikali katika kujisafisha mbele ya watanzania kutoka kwenye aibu ya kushindwa kusimamia hali tete ya uchumi wa watanzania kwa kadri ambayo CHADEMA wamedhamiria kuwavua nguo, na hasa uoga wa kufukuzwa kazi na UMA.

  Sasa, kwa sababu wakati wanaanza kufanya ivyo mamalaka zilizopewa fursa ya kuzisimamia hazitakuwa na uwezo wa kukataa uso kwa uso kama ilivyokawaida. Chonde chonde watanzania tuwe nyuma yao na kupinga ukwapuaji huu ambao ndio unaweza kuwa wa kutumaliza kabisa watanzania.

  TUYALINDE MASHIRIKA YETU YA HIFADHI YA JAMII DHIDI YA UFISADI KWA NGUVU ZETU ZOTE.
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Tutasaidiwa na nani kupata habari za ndani maana tatizo kubwa liko kwa CEOs wa mifuko hii. Wanajiona kama walipewa nafasi wasiyostahili na matokeo yake kila wakati wanafanyakazi kwa kujikomba ili waendelee na nafasi zao.

  CEOs wamekuwa wakificha taarifa za mifuko hii na hata kuwahonga waandishi wa habari au hata viongozi wakuu kabisa ili wasinyooshewe kidole. Kuna taarifa kwamba Katibu mkuu kiongozi amekuwa akipewa chochote kwa muda mrefu ili kuzuia usawazishaji wa mtindo wa malipo yanayofanywa na mifuko hiyo.

  Pia kumbuka wakati sheria ya kuruhusu uhuru wa kujiunga ktk mashirika haya ilivyogeuzwa dakika za mwisho na wabunge kwa sababu moja kubwa kwamba baadhi ya mifuko kama PPF walitoa kitu kidogo ili wasipoteze wanachama kwa huduma mbaya wanayotoa.

  Nadhani waache wachote ili mwishoni mifuko hiyo ishindwe kulipa mafao, njaa iingie na hapo ndo tutaiona CCM. Dawa ya madikteta ni njaa kwa wananchi.
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tena ataewezesha mpango huo ni ZITTO KABWE m/kiti ya kamati ya bunge ya mashirika hayo, That why anang'ang'ania NSSF ipeme kiwira badala ya TANESCO, ukweli ni kuwa CCM haina pesa. Wamemaliza kwenye kampeni na ruzuku imepungua sana, serikali pia haina pesa matumizi makubwa baraza la mawaziri pia wahisani wamegoma, SASA HIVI WANAITOLEA MACHO HILO MIFUKO.
   
Loading...