Mashirika na taasisi mmejipangaje na tahadhari ya kimbunga ili kuondoa usumbufu na hatari kwa wateja wenu?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Matamko na Tahadhari zinapotolewa na wataalam;
Serikali za kiafrika hasa Tanzania kumekuwa na kasumba ya baaadhi ya mamlaka/mashirika kujitoa kuwajibika ipasavyo kwa watu wake!

Je, tahadhari hii ya kimbunga awamu hii Taasisi na mashirika mmejipangaje kupunguza hatari ya kimbunga kiafya na kisaikolojia?

Wakuu na wakurugenzi wa Taasisi zifuatazo toeni majibu, maana nafaham zipo za kitaasisi na zipo za sisi kama wanainchi mmojammoja!
  • Watu wa TEMESA- mmejipangaje na VIVUKO vyenu? Au Mnasubiri hadi vipeperushwe na kimbunga? Mnaonaje mkaomba RATRA Watoe TRB za mda kwa mabus yaongezeke kupita bure darajani ili kuchukua abiria kigamboni ili MSIMAMISHE VIVUKO KWA MDA?
  • Watu wa Zimamoto na uokoaji, Mmejipangaje Kutoa elimu za namna ya kuwapata kirahisi kwasababu inatazamiwa kimbunga kikitokea nataraji hata network haitakuwepo automatic! Ni vitu gani mnawashauri watu wawe navyo?
  • TAA mmejipangaje kuwapunguzia usumbufu abiria wa kukata tiketi then muahirishe safari za ndege ghafla? Mmejipangaje kuondoa usumbufu huo wa kisaikolojia?
  • Watu wa TARURA na TANROADS mmejipangaje kuhakikisha barabara zinapitika! Yapo maeneo kuna miti na miembe mikubwa barabarani iliyo katika hatari ya kuanguka je TARURA mmekosa hata mafuta ya kuweka kwenye CHAINSAWS ili mfanye BUSH CLEARING kwenye wings road mnazosimamia ktk maeneo yenu kuondoa hatari hizo?
  • TANESCO sina shaka na nyie maana mnafahamika wazee wa shortcut ya KUKATA umeme! Hamnaga tabu na mtu kabisa! Lakini vipi zile nguzo mbovu au bajeti hairuhusu?
  • TCRA Wazee wa minara mpo au hampo? Nafaham mabando yamegoma kushuka lakini vipi! Kimbunga kwenye minara ya simu mnasemaje? Mmewaoa Tahadhari wakaazi wa karibu na minara?
Taasisi na mamlaka mmejipangaje! Au TUSUBIRI kwanza kimbunga kije ndo mtoe TAMKO Kwa vipaza sauti!

Hii kasumba ya mamlaka kutokuwajibika kwa wakati tukiiendekeza itakuja kupenya hadi kwenye majeshi yetu! Vita ikitokea utashangaa TUNATANGULIZWA RAIA tukapigane!

Maana navyowafahamu viongozi wetu Majanga yanapokuja WOTE hugeuka wachungaji na kuja na vifungu vya BIBILIA!

NAOMBA KILA MTU ATIMIZE WAJIBU WAKE!
Ya wachungaji tuwaachie wachungaji
 
Nasikia kitaisha nguvu kabla hakijafika nchini
3DB65052-30C4-473D-8B11-ADB6FA0DF46E.jpeg
 
Nimeona baadhi ya Nchi masikini za Asia na Carribean huwa wanakodi magari na kuweka vipaza sauti kuwatataarifu wanaoishi kando kando ya Bahari na wale wanaokaa Mabondeni.
 
Nimeona baadhi ya Nchi masikini za Asia na Carribean huwa wanakodi magari na kuweka vipaza sauti kuwatataarifu wanaoishi kando kando ya Bahari na wale wanaokaa Mabondeni.
Ndo mipango yenyewe hiyo
 
Back
Top Bottom