Mashirika 11 ya Umma hayakupeleka hesabu zao kukaguliwa ikiwemo TANESCO, TTCL, NHIF, Posta na Muhimbili

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,674
2,000
Taasisi ambazo hazikuwasilisha hesabu zake kukaguliwa.

1. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
2. Kampuni ya Mbolea Tanzania
3. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
4. Mfuko wa UTT
5. Shirika la Magazeti Tanzania
6. Shirika la Posta Tanzania
7. Shirika la Reli Tanzania
8. Shirika la Simu Tanzania
9. Shirika la Umeme Tanzania
10. Solo la Bidhaa Tanzania
11. Taasisi ya Mifupa Muhimbili.

6AD7CEDE-FC67-4B84-ABEA-7C744D10402A.jpeg
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,253
2,000
Huko kuna sababu ndio maana hawakumruhusu kukagua, ni madudu tu na upigaji awamu ya 5
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,569
2,000
Shamba la bwana joni, mbuzi wa bwana joni....
Kesi ya tumbili hapelekewi nyani
Huwa wananishangaza sana hawa watu, maana haina sababu kuweka wazi hizi mambo zao ilihali hakuna hatua zozote wanazotaja baada ya hapo.

Utasikia tu CEO katumbulia, akija mwingine business as usual
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,427
2,000
Huwa wananishangaza sana hawa watu, maana haina sababu kuweka wazi hizi mambo zao ilihali hakuna hatua zozote wanazotaja baada ya hapo...

Utasikia tu CEO katumbulia, akija mwingine business as usual
Ma CEO wanayafanya haya Makampuni kama Yao ni kama miungu watu.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
158,622
2,000
Huwa wananishangaza sana hawa watu, maana haina sababu kuweka wazi hizi mambo zao ilihali hakuna hatua zozote wanazotaja baada ya hapo...

Utasikia tu CEO katumbulia, akija mwingine business as usual
Kata matawi acha mizizi ili mti uchipue tena
 

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,527
2,000
Watueleze na adhabu wanazopewa kwa kufanya ukaidi

Hili ni Taifa la Wendawazimu , vichaa na wezi wakubwa.
Haya mashirika hayawexi kuwasilisha Mahesabu yao kwa vile kule ni madudu na Upigaji au Ufisadi wa KUFA MTU!! Hii Jeuri yao ya kutokubali kukaguliwa na CAG ilikuwa ni Hayati Jiwe kwa utaratibu huu:
  1. Kwamba wengi wa Wakurugenzi wa mashirika haya WALITEULIWA NA HAYATI MAGUFULI wakiwa kama Makada wa CCM.
  2. Kuna kipindi Hayati Magufuli akaanza KULAZIMISHA GAWIO TOKA MASHIRIKA HAYA yanayo jiendesha kwa HASARA na walitoa mabilioni ya Fedha Kama Gawio. Matokeo yako hoi bin taaban kiadi cha kushindwa kuruhusu Ukaguzi wa CAG.
Ushauri kwa Rais Sameer Suluhu:
TUMBUA WAKURUGENZI WOTE WA MASHIRIKA HAYA UANZE UPYA.
Kuzuia taarifa za Mahesabu kwenda kwa CAG kwa Ukaguzi ni utovu wa nidhamu na UVUNJAJI WA SHERIA.
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,427
2,000
Mnyonge mnyongeni, Angekuwepo Magufuli hawa Ma CEO wangekaa majumbani kwao na 'mafi' Yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom