Mashinji saka'Panya' wanaotafuna pesa kama mchwa ndani chadema, anachana na Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Chadema kinaposema kuwa Rais Magufuli ni mkwapuaji wa sera za Chadema lakini hana uwezo wa kuzitekeleza kwa vitendo kawani anatoka ndani ya chama chenye msingi way a wizi na serikali yake haiwezi kuwa safi na ataishia kufanya maigizo.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa chama hicho Vicent Mashinji wakati akifungua Kongamano la Baraza la vijana chadema (BAVICHA) na umoja wa vyuo vikuu (CHASO) mjini Dodoma.

Maana nyepesi ya neno ‘mkwapuaji ni’ ni mporaji ambapo Chadema wanataka kuuaminisha umma kuwa anachofanya rais Magufuli hewani ama ni sera zao.

Wanasahau kuwa Magufuli ameingia Ikulu kutokana na kufaulu kunadi vyema mkataba na wananchi ujulikanao kama ilani ya Uchaguzi ya CCM ambazo ndizo sera zenyewe anazozitekeleza leo hii.

Hapo ndipo ninapomshangaa Mashinji atasemaje Magufuli ni mkwapuaji wa wa sera za Chadema zilizokataliwa na wananchi kupitia sanduku nla kura na kuacha kuteleza sera za CCM zilizokubaliwa na kumpeleka Ikulu?

Chadema wanajivika joho la wapambanaji dhidi ya ufisadi nchini, wakati hakuna uhalisia wa kauli hiyo zaidi ya porojo tu wanazojaribu kuwaeleza wananchi huku wakifurahia nafsini mwao.

Labda nimwambie jambo moja Mashinji, halafu kwa upande mwingine nimshauri kijana huyo ambaye ni mchanga sana katika siasa za Tanzania kwa ujumla wake. Nilimuheshimu sana pale aliposema kuwaasa wana chadema wenzie kuwa kupayuka payuka ndani ya chama chao sasa basi, lakini ajabu yeye ndiye amegeuka kuwa mpayukaji wa kwanza tangu atoe kauli hiyo, hii inachesha sana.

Mashinji anapaswa kuacha siasa nyepesi za kutafuta kick ili atokee mgongoni mwa Rais Magufuli jambo ambalo litampoteza kabisa tofauti na matarajio yake, anapaswa kutumia nafsi hiyo ya ukatibu mkuu wa chadema kujenga chama na kutafakari wapi walipoanguka na ikibidi kumueleza Mbowe waziwazi bila kumficha kuwa alikosea sana alipobadili gia angani kwa kuchukua makapi ya CCM.

Mashinji anapaswa kuanza kazi ndani ya chadema kwa kusaka ‘panya’ waliojaa ndani ya chadema wanaotafuna pesa kama mchwa badala kupoteza muda kwa kujinasibu kuwa wapambanaji dhidi ya ufisadi

Mashinji anajua kuwa Chadema wanapokea pesa kutokana serikali takribani milioni 500 kila mwezi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa nchini kama ruzuku. Lakini leo hii wanashindwa hata kumiliki ofisi za chama chao iwe mikoani , wilayani na hata kwenye kata zao huku wakipokea mamilioni kila mwezi pasipo kuonyesha jamii matumizi ya mamilioni hayo.

Pesa zinapokwenda hazijulikani halafu bado wanajiita wapambanaji wa vita dhidi ya ufisadi nchini wakati wao wana lebo ya ufidai?

Ukiachana na ruzuku, Mashinji anapaswa kumuuliza Mbowe kinagaubaga kuhusu misaada ya chama hicho kutoka kawa mfanyabiashara maarufu nchini mzee Mustapha Sabodo amabapo kuna wakati aliwapa chadema pesa ya kuchimba kisima kila jimbo lenye mbunge wa chadema, akawapa pesa za ujenzi wa makao makuu lakini mpaka leo hakuna ofisi wala kisima kilichochimbwa.

Mashinji anapaswa kuelewa kuwa Rais Magufuli si mkwapuaji wa sera bali ni mtekelezaji wa sra na ilani ya CCM ambayo ndiyo iliyomuingiza Ikulu. Magufuli ameonyesha kuwa Mzalendo, Mchapakazi anayewajibika na mwenye maono ya malengo ya kutuvusha kutoka hapa tuliko na kuelekea kwenye mafanikio na maendeleo
 
Back
Top Bottom