Mashine za NIDA zote wilaya ya Arusha zaibwa

state agent

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
1,764
2,511
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Jery Muro ameiambia ITV muda mfupi kuwa mashine za kutengeneza vitambulisho vya utaifa wilayani humo zote imeibiwa usiku wa kuamkia leo.

Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutoa ratiba ya kuandikisha na kusajili vitamburisho hivyo kwa mkoa huo wiki hii mpaka tarehe 20/01/2020.

Watu hao wasijulikana mpaka muda huu hawajakamatwa hata mmoja wao

Chanzo: ITV habari za hivi punde

IMG-20200106-WA0027.jpeg

Taarifa zaidi;
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema Ofisi ndogo za NIDA zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha zimeibiwa vifaa vyote na Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo

Amesema vifaa vilivyoibwa ni pamoja na Kompyuta Mpakato nne na Kamera si chini ya tatu pamoja na vifaa vingine vilivyokuwa vikiingiza majina kwenye mifumo na katika wizi huo unaonekana ni wa ndani kwani milango haikuvunjwa

Aidha, amesema tukio hilo limewashtua na ni mara ya pili tukio kama hilo kutokea ikiwa mara ya kwanza lilitokea ofisi za NIDA Makao Makuu Wilaya ya Arumeru ambapo baadhi ya vifaa viliibwa taratibu kwa muda mrefu

Ameida kuwa wizi huo unaonekana umefanyika kimtandao kwasababu Ofisi ndogo za NIDA kwenye ukanda huo zipo karibu kabisa na jengo la NMB lenye walinzi na Halmashauri ina Walinzi wake

Amewaomba Wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho yeye na Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaendelea kufuatia na vile vile ameeleza kuwa kwa sasa hakutakuwa na huduma katika ofisi hiyo ya Halmashauri ya Arusha
 
MChezo wa kizamani sana umefanya Mrisho Gambo, Jerry Muro na MaCCM wenzio. Mmechukua mashine ili mjitengezee vitamburisho vingi. Badae mpate kutengeza vitamburisho feki vya kupigia kura kwa wingi.
Hakuna mashine iliobiwa zipo kwa Mkuu wa mkoa.

Nchi imekua ya hovyo sana hii
 
1578303371391.png
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro ameeleza kuwa vifaa vya NIDA vinavyotumika wakati wa mchakato wa usajili vyaibiwa.

Aidha, katika kufafanua zaidi tukio hilo Jerry Muro alisema “Vifaa vyote vimeibiwa, kompyuta nne, camera si chini ya tatu na vifaa vingine, tumepata mshtuko, milango haikuvunjwa inaonekana ni wizi wa kimkakati umefanywa ndani, vifaa vya NIDA ni mali za Taifa sasa hawa wanapata wapi ujasiri wa kuiba!"


Chanzo: Millard Ayo
 
Trillion, Uko sahihi, kwanini zipotee kipindi ambacho Gambo ametumia akaunti zake za mitandao ya kijamii the whole weekend kupromote ratiba ya uandikishwaji? Kwanini azungumze Jerry na sio Daqaro? Kwakua Jerry Ana access na media? Hiyo syndicate ya kuibiwa kwanini haikugundulika? Hapa kitakachotokea utaskia polisi wakuta mashine zimetelekezwa porini, stupid
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom