Mashine za NIDA zote wilaya ya Arusha zaibwa

Ila ccm ni wapiga dili sana hata hao wafanyakazi wa nida wanaweza wakaibiwa

Sent using Jamii Forums mobile app



Wanaweza kuibwa au kuibiwa??-- kuna kuibwa na kuibiwa, mfano; mtu anaweza kusema hivi; "nimeibiwa pesa yangu, pesa yangu imeibwa." --- nadhani utakuwa umeelewa au rejea main post uone jinsi muandishi alivyokuwa mahiri katika upande huo.
 
HAWA WALABATA WA ARUSHA HATARI SANA YAANI WAMEAMUA KUUIBA MFUMO ILI WAKATOE VITAMBULISHO KWA PENGINE WAGENI WASIOSTAHILI KUWA NAVYO KWA PESA NDEFU,ALIMRADI WAENDELEE KUPIGA BIERY.
#WAHUSIKA WAHAKIKISHE VIFAA VYOTE VIMEPATIKANA MARA MOJA.
 
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Jery Muro ameiambia ITV muda mfupi kuwa mashine za kutengeneza vitambulisho vya utaifa wilayani humo zote imeibiwa usiku wa kuamkia leo.

Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutoa ratiba ya kuandikisha na kusajili vitamburisho hivyo kwa mkoa huo wiki hii mpaka tarehe 20/01/2020.

Watu hao wasijulikana mpaka muda huu hawajakamatwa hata mmoja wao

Chanzo: ITV habari za hivi punde


Taarifa zaidi;
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema Ofisi ndogo za NIDA zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha zimeibiwa vifaa vyote na Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo

Amesema vifaa vilivyoibwa ni pamoja na Kompyuta Mpakato nne na Kamera si chini ya tatu pamoja na vifaa vingine vilivyokuwa vikiingiza majina kwenye mifumo na katika wizi huo unaonekana ni wa ndani kwani milango haikuvunjwa

Aidha, amesema tukio hilo limewashtua na ni mara ya pili tukio kama hilo kutokea ikiwa mara ya kwanza lilitokea ofisi za NIDA Makao Makuu Wilaya ya Arumeru ambapo baadhi ya vifaa viliibwa taratibu kwa muda mrefu

Ameida kuwa wizi huo unaonekana umefanyika kimtandao kwasababu Ofisi ndogo za NIDA kwenye ukanda huo zipo karibu kabisa na jengo la NMB lenye walinzi na Halmashauri ina Walinzi wake

Amewaomba Wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho yeye na Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaendelea kufuatia na vile vile ameeleza kuwa kwa sasa hakutakuwa na huduma katika ofisi hiyo ya Halmashauri ya Arusha
Kama huelewi elewa hivi..... bwana mkubwa katoa amri isiyotekelezeka ya siku 21.(haitekelezeki)
ili kuongeza muda mashine zitaibiwa na hawa kina MURRO/ Kwa uongo. baada ya hapo utaongezwa muda katika wilaya husika na kwinginepo ili zoezi likamilike. hapo aibu itakuwa imefichwa.
elewa hivyo, mlinzi aibe yale madude apeleke wapi?
 
MChezo wa kizamani sana umefanya Mrisho Gambo, Jerry Muro na MaCCM wenzio. Mmechukua mashine ili mjitengezee vitamburisho vingi. Badae mpate kutengeza vitamburisho feki vya kupigia kura kwa wingi.
Hakuna mashine iliobiwa zipo kwa Mkuu wa mkoa.

Nchi imekua ya hovyo sana hii
Aisee kweli kabisa
 
Natabiri kuanzia 2021 kila kosa litakuwa ni kosa la kuhujumu uchumi!
Draw%20Over%20Photo1578376423996.jpeg
 
Kwahiyo hizi sasa ni za kukomolea au anapewa mtu kama anavyostahili?
 
Back
Top Bottom