Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 539
- 531
Hivi Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya pamoja na Watu wako wa Mipango Miji wakati mlipokuwa mnawahamishia Wafanyabiashara katika Soko la Sido hivi mlifikiria suala la afya zao?
Mlikuwa mnajua kabisa kwamba lile ni eneo la viwanda ilikuwaje mkawahamishia Wafanyabiashara pale?
Kipindi hiki mtu ukienda katika Soko hilo unakuta mapumba yametapakaa kila sehemu na kusababisha magonjwa ya kifua na mafua kwa Wafanyabiashara na Watu wengine.
Soko la Sido lipo katika eneo linalomilikiwa na Shirika la Viwanda Vidogo na eneo hilo lipo katikati ya Jiji la Mbeya.
Mashine za mpunga pamoja na zile za kukamua Alizeti vikiwemo viwanda vya sababuni na mafuta ya kupaka vyote vipo katika eneo hilo.
Hivi imeshindikana kabisa kuwarudisha Wafanyabiashara katika Soko la Mwanjelwa?
Kama imeshindikana basi hamisheni hivi viwanda ambavyo vipo katika eneo hilo na vikafungwe kule Iyunga ambako ndiko limetengwa eneo la viwanda.
Hizi mashine hasa za mpunga zimekuwa kero kubwa sana hapa sokoni, yaani upepo ukipuliza tu ni tatizo, Soko zima linatapakaa mapumba ya mpunga.
Mbaya zaidi pumba zimekuwa mengi na wahusika hawana sehemu ya kuzipeleka, hivyo zinabaki zikijaa eneo hilo.
Mwanongwa nawakumbusha tu kuwa afya ya binadamu ni Bora kuliko fedha.