Habari zenu wanajamvini,
Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.
Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.
--------------------
Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.
Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.
--------------------
Kuna jamaa yangu alinunua magomeni, incubator na inayoweza kuhatch mayai elfu tisa (9,000) hapo magomeni, cost ilikuwa arround milioni 20 za kitz, inafanya kazi mpaka leo. Yeye biashara yake ni kutotolesha vifaranga tu, unaenda na mayai yako anakucharge 300 kwa kila yai. Yakitoka yasitoke that's the cost.
Nikavutiwa na biashara nikatafuta vendor china nikapata kwa dola 2900 kila kitu, hiyo iliikuwa ni hatcher ya mayai 5000 na incubator ya mayai 6000, bei ya hatcher ilikuwa dola 700, na incubator 1100, na hizo 1100 zilikuwa ni contena la futi ishirini kuja tz. Sasa hizi habari ni za mwaka 2010 mwanzoni, sijui sasa zikoje.pia kumbuka kuna tra na customs mzigo ukishafika, fanya utafiti wa gharama za kutoa mzigo.
Kama uko interested ingia alibaba.com, jiridhishe mwenyewe na wauzaji kwa kusearch kama unavyofanya google. Halaf malizana nao. Ila kuwa makini, matapeli wengi. Ingekuwa vema ukawatumia watz wanaoenda kununua bidhaa zao huko japo wakachungulie kama jamaa wana kiwanda na wahakikishe usalama wa pesa zako kwa kuthibitisha mzigo unapakiwa melini.
Nb: hata hao watz usiwaamini sana, sanaa zimezidi nchini hapa.
Na kama nilivyo sema hapo mwanzo unapo taka kuchagua Incubators zingatia mambo makuu kama Matatu hivi
1. Automatic au Manual- Mashine ambazo ni automatic ni nzuri sana kwa sababau zinakurahisishia kazi kuliko ambazo ni manual turining
2. Forced Air Incubators
Hii huwa nafeni kwa ndani na hiyo feni husaidia kutawanya joto kwenye mayai, na uzuri wa Forced Air incubators ni kwamba hata Joto ikizidi haitaharibu mayai kwa sababu feni inasaidia kupunguza hilo joto,
Na hii ndo Bora zaidi kwa sababu feni husaidia sambaza joto na humidity ndani ya mashine
3. Still- Air Incubators
Hii haina feni, na inategemea Contro za Nje, so kwa hii aina ni lazima mtu awe karibu na mashine 24 hour ili kucheki, lakini kwa ile aina ya kwanza ukiwa na uhakika na umeme na ukawa umeongeza maji ya kutosha kwenye mashine unakuwa hauna haja ya kuwepo muda wote
Hizi ndo aina kuu za Incubators na unapo enda kununua incubator hakikisha unajua hili, make mara nyingi katika ununuzi wa Incubators unatakiwa kutambua hiyo.
Na kwa ishu ya Power nyingi za hizi kubwa kutoka China zina sehemu ya kutumia Gesi kama altenative energy ila unapo tumia gesi maana yake hata kama Incubators ilikuwa ni Automatic itabidi ubadilishe mayai kwa mkono au manual kwa sababu gesi inakuwa haifui umeme bali inasaidia katika kutoa joto kwa incubators
KUHUSU INCUBATORS
Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viuombe mbali mabali hasa Ndege,
AINA ZA INCUBATORS
1. Forced Air Incubator
2. Still Air Incubators
FORCED AIR INCUBATOR
- Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators
STILL AIR INCUBATORS
- Hii ni mashine siyo kuwa na fane
IPI NZURI?
- Inashauriwa kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haiatakusmbua na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara nyingi ndogo ndo still air
3. AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION
- Manual
- Automatic
MANUAL INCUBATORS
- Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika
AUTOMATIC INCUBATORS
- Hizi hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za manual hupunguza sana
- Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila kuchungulia mashine yako na ikawa inapiga kazi bila tatizo.
-
NI IPI NZURI?
-Kwa kweli kwa maisha ya sasa inahitajika Automati Incubators ambayo haitahitaji wewe kuwepo mara kwa mara katika ku contro mashine, Ingawa kuna wakati Manual inahitajika kuliko Automatic na kuna wakati Automatic inahitajika kuliko manual
NB: Automatic nyingi zina manual, yaani kuna sehemu ya kushft kwenda manual, ila manual karibia zote hazina sehemu ya kushift kwenda automatic
ILA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA UFANISI SAWA, TOFAUTI MOJA NI AUTOMATIC NA NYINGINE NI MANUAL
MAMBO MUHIMU SANA KWENYE INCUBATORS
- Aina ya incubators
- Model of operation
- Manufacture
- Nguvu inazo tumia
- Altenative source of power
4. MANUFACTURE
Incubator nyingi za nje ni nzuri sana, Kuna za Italy, Denmark, Uk, China, USA, India, South Africa Trukey na kazalika na bei zinatofautiana. Na utaona kwamba Incubator kama za Uk, South, USA, Italy ni very expensive compare na za kutoka China au India.
Ila bei kutofautiana sana sio ishu na kama mnavyo jua China wao wna Policy yao kuhusu Internatinal Trade that is why.
Mashine nza Ndani ya Nchi nazo zipo nzuri na zipo zingine ni vimeo ila watengenezaji wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye Utafiti na si kujikita kwenye mauzo, inatakiwa kuboreshwa zaidi na zaidi ili ziwe na viwango vizuri
5. SOURCE OF ENERGY
Incubators karibia zote zinatumia Umeme kama source namba one na jua, makaa yam awe au gas kama source namba mbili, ingawa zipo za mafuta ya taa pia kama source No 1
6. ALTENATIVE SOURCE OF ENERGY
Kila aina ya mtengenezaji ana source yake ya altenative energy, zipo za Gas, zipo za umeme jua na zipo za mvuke wa maji na zipo za mafuta ya taa, na zipo za makaa yam awe.
7. ALTENATIVE SOURCE NZURI
- Kwangu mimi Incubators ambazo altenative source of energy ni Mvuke wa maji nimetokea kuzipenda sana
- Hapa umeme ukikatika unaunga pipe kwenye Mashine na unakuwa na birika special na unaiweka jikoni maji yanachemka na mvuke unapita hadi kwenye incubators, ni source nzuri sana,
- Hata jua nayo ni source poa
ILA BADO SOURCE YA JUA AU GAS INAKUWA NI ALTENATIVE NZURI SANA.
MATATIZO YA INCUBATORS
Incubators nyingi zina shida moja kubwa sana, Incubators inaweza ikaharibika na wewe usiwe na habari kabisa na mpaka uje kushutuka ilisha haribu mayai yote na hilo ni tatizo kubwa sana,
MFANO:
-Heating tube zinaweza kufa na wewe usijue kabisa, na ukija shitikia ilisha haribu kila kitu
-Humidity Tube inaweza kufa na wewe usijue na ukija shitukia ni balaa
-Eggs turning inaweza kufa na usitambue hata siku mbili
- Humidity sensor na temperature sonsor zinaweza kufa na wewe usijue chochote
Na mara nyingi kinaweza kufeli kifaa kimoja za vingine viakendelea na kazi bila shida ila ikawa ndo kama hivyo, Mfano Mashine inaweza kuwa imekufa Humidity tube, na hapo inaweza endelea kufanya kazi na some time ni vigumu sana kugundua.
- Na tofauti na mitambo kama gari, Incunator inapo haribika huku ukiwa umeweka mayai ni balaa tupu, kama huna mashine nyingine ndo inakuwa imeharibu mayai yote.
KUKATIKA KWA UMEME- Endapo umeme utakatika na ukatumia Gas, au mafuta ya taa au makaa yam awe kama source nyingine ni lazima ugeuze mayai kwa mkono, na hapa tatizo liko kwamba ile mashine haiwezi kukubali kugeka ni lazima ubonyeze sehemu ya kubadilisha kutoka automatic kwenda manual. HAPA NDO HUWA KUNA KAZI PEVU
Na Mwisho ni kuhusu uendeshaji wa Incubators, Mara nyingi uendeshaji nao ni tatizo kubwa nasa hasa kwenye seting joto na humidity, make seting lazima zitofautiane kulingana na maeneo au vipindi Fulani, Joto na wakati wa Baridi kari
Wakuu kama una mashine za kuangulia mayai unaweza pata kutoka kwangu.
1. Spare parts zote za incubators
2. Trays za kuwekea mayai kwenye mashine
3. Tray za kutotoleshea
4. Kufanya repair za mashine mbovu/iliyo haribika
Natengeneza Incubator Temberea Uzi umeandikwa natengeneza Incubator
Hizi ni incubator Ninazo tengeneza View attachment 164925View attachment 164926View attachment 164927View attachment 164928View attachment 164930hii imeisha kula mzigo tayari View attachment 164931