Mashine za kutotolesha mayai (Incubators): Upatikanaji wake, aina zake, matumizi na ushauri

Jaman msiwe mnazisema vibaya incubator za watanzania, mimi nmenunua kutoka kwa watanzania incubator ya mayai 1440 na inafanya vizur tu.

bonvize umenunua sh ngapi? inatumia umeme au mafuta ya taa? ni manual au automatic?

pia tujulishe uliponunua basi
 
Hyo incubator n automatic, inatumia umeme, imenigharmu kiasi cha shilingi milioni 3 had naifunga morogoro, wauzaji ni MTANGA GENERAL MERCHANDISE LTD, wanapatkana kibaha. Imeweze kutotoresha asilimia 80 ya mayai nliyoyaweka, kwa sasa nna vfaranga chotara vya mwez mmoja.
 
Incubator inahitaji umakini wa hali ya juu kabisa. Si ishu ya kukurupuka, na uatomatic haupo katika kugeuza mayai tu. Na kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa uvijue b4 ya kununua incubator, hii ni sawa na mitambo ya kumsaidia binadamu kupumua,
 
Mkuu Chasha nilikuomba contacts za wale wachina, nataka kuwasiliana nao waniletee incubator mzee
 
Incubator inahitaji umakini wa hali ya juu kabisa. Si ishu ya kukurupuka, na uatomatic haupo katika kugeuza mayai tu. Na kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa uvijue b4 ya kununua incubator, hii ni sawa na mitambo ya kumsaidia binadamu kupumua,

Sawa mdau ila hi incubator ambayo mimi naitumia ina huduma zote ambazo wewe mwenyewe ulizichambua kwenye post zako zilizopita hapo juu na kueleza n muhmu kwenye incubator, iwe automatic na forced air incubator. Humidity na temperature regulation vyote n automatic.
 
aisee mchina na mashine yake iko poa sana
 
mkuu kama unataka kuagiza incubator china, naeza kukusaidia kwani mimi ni mtanzania nilieko china huku, kitu cha msingi nipe tu specification za incubator unayotaka, then ntakuangalizia gharama zake, then kuhusu kusafirish wala sio tabu (hutaangaika kuilipia bandarini) kwani ukishanunua CBM kwenye container itakayosafirisha (kwani inasafirishwa pamoja na vifaa vingine vya kibiashara), wewe ni kusubiria bongo tu na kuchukua mashine yako, na pia kuhusiana na malipo utailipia itakapofika bongo.
 
mkuu unauhakika halipi Chochote Bandarini? ni hakuna ghalama Bandarini? kwani hilo Kontena lenye vifaa vingine lina kaa bure Badandarini? mkuu kuna Chaji zakufa mtu pale Bandariini, TRA wana kodi ao pale, Bandari wana chao,TBS wana chao pale bado Agent, so si kweli kusema hakuna Malipo pale, VAT inalipwa kama kawaida
 
Mkuu umenifurahisha hapo pekundu!
vipi unaweza kunitafutia photocopy machine aina ya Canon IR 2800?? (samahani kwa kutoka nje ya mada)
 
Mkuu umenifurahisha hapo pekundu!
vipi unaweza kunitafutia photocopy machine aina ya Canon IR 2800?? (samahani kwa kutoka nje ya mada)[/QUOTE
kuhusiana na hiyo kulipia bongo (ni kwa sababu kuna mtu mwingine anahitaji hizo incubetor, so wakati wa kumpakilizia naeza add extra one kwa ajili yake, asipokuja kuichukua still itaingia kwenye projrct ya huyo mtu mwingine ndo maana nimepma hiyo option ya kulipia bongo) ebwana kuhusu hiyo Canon IR 2800, inaeza kupatikana, but nakushauri kama unahitaji huku inabidi ununue mpya manake used ya mchina ina mafambaya kutosha tu unaeza tumia kwa mda mchache sana inaaanza kukusumbua (used ya mchina haina tofauti na used ya hapo bongo kwetu, huku wametuzidi tu utunzaji) otherways kama utataka used kutoka japan au uk, naeza kukupa conection na jamaa yuko bongo hapo anajua na kudeal na hizo mambo
 
mkuu unauhakika halipi Chochote Bandarini? ni hakuna ghalama Bandarini? kwani hilo Kontena lenye vifaa vingine lina kaa bure Badandarini? mkuu kuna Chaji zakufa mtu pale Bandariini, TRA wana kodi ao pale, Bandari wana chao,TBS wana chao pale bado Agent, so si kweli kusema hakuna Malipo pale, VAT inalipwa kama kawaida

uko sahihi kabisa mkuu (nilichokua namaanisha, sio kwamba hatalipa! yeye hatapata ule usumbufu wa kufuatilia, nilivyosema atanunua CBM ndani ya gharama ya Cbm ilishawekwa pia gharama za kodi, ajent nk)
 
Mkuu umenifurahisha hapo pekundu!
vipi unaweza kunitafutia photocopy machine aina ya Canon IR 2800?? (samahani kwa kutoka nje ya mada)

kuhusiana na hiyo kulipia bongo (ni kwa sababu kuna mtu mwingine anahitaji hizo incubetor, so wakati wa kumpakilizia naeza add extra one kwa ajili yake, asipokuja kuichukua still itaingia kwenye projrct ya huyo mtu mwingine ndo maana nimepma hiyo option ya kulipia bongo) ebwana kuhusu hiyo Canon IR 2800, inaeza kupatikana, but nakushauri kama unahitaji huku inabidi ununue mpya manake used ya mchina ina mafamba ya kutosha tu unaeza tumia kwa mda mchache sana inaaanza kukusumbua (used ya mchina haina tofauti na used ya hapo bongo kwetu, huku wametuzidi tu utunzaji) otherways kama utataka used kutoka japan au uk, naeza kukupa conection na jamaa yuko bongo hapo anajua na kudeal na hizo mambo
 
Yes mkuu, niunganishe na huyo jamaa yako ili nichukue used kutoka japan au uk
 
Habari za asubuhi wapendwa!

Naomba kujulishwa/kuelekezwa au hata mawasiliano ya mtu mwenye mashine ya kutotolesha mayai Morogoro au Kilosa mimi niko Mikumi.
 
KUHUSU INCUBATORS
Incubators ni Mashine zinazo tumika kutotoreshea viuombe mbali mabali hasa Ndege,

AINA ZA INCUBATORS
1. Forced Air Incubator
2. Still Air Incubators

FORCED AIR INCUBATOR
- Forced Air Incubators ni mashine yenye Feni kwa ajili ya kutawanya joto ndani ya incubators

STILL AIR INCUBATORS
- Hii ni mashine siyo kuwa na fane

IPI NZURI?
- Inashauriwa kutumia/kununua Forced Air Incubators ndo bora kabisa na haiatakusmbua na hatahivyo kwa incubator kubwa karibia zote ni Fored air, na mara nyingi ndogo ndo still air

3. AINZA INCUBATOR KWENYE OPERATION
- Manual
- Automatic

MANUAL INCUBATORS
- Hizi hutumia mikono katika kugeuuza mayai na katika maswala mengine kama kucontro joto na kazalika

AUTOMATIC INCUBATORS
- Hizi hujiendesha kama Computer, kila kitu hufanywa automatically so kazi za manual hupunguza sana
- Ukiwa na Incubnator Automatic na ikawa na sehemu ambayo inajiongeza maji automatically basi inaweza hata kata wiki bila kuchungulia mashine yako na ikawa inapiga kazi bila tatizo.
-

NI IPI NZURI?
-Kwa kweli kwa maisha ya sasa inahitajika Automati Incubators ambayo haitahitaji wewe kuwepo mara kwa mara katika ku contro mashine, Ingawa kuna wakati Manual inahitajika kuliko Automatic na kuna wakati Automatic inahitajika kuliko manual
NB: Automatic nyingi zina manual, yaani kuna sehemu ya kushft kwenda manual, ila manual karibia zote hazina sehemu ya kushift kwenda automatic

ILA ZOTE ZINAFANYA KAZI KWA UFANISI SAWA, TOFAUTI MOJA NI AUTOMATIC NA NYINGINE NI MANUAL
MAMBO MUHIMU SANA KWENYE INCUBATORS
- Aina ya incubators
- Model of operation
- Manufacture
- Nguvu inazo tumia
- Altenative source of power

4. MANUFACTURE
Incubator nyingi za nje ni nzuri sana, Kuna za Italy, Denmark, Uk, China, USA, India, South Africa Trukey na kazalika na bei zinatofautiana. Na utaona kwamba Incubator kama za Uk, South, USA, Italy ni very expensive compare na za kutoka China au India.
Ila bei kutofautiana sana sio ishu na kama mnavyo jua China wao wna Policy yao kuhusu Internatinal Trade that is why.

Mashine nza Ndani ya Nchi nazo zipo nzuri na zipo zingine ni vimeo ila watengenezaji wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye Utafiti na si kujikita kwenye mauzo, inatakiwa kuboreshwa zaidi na zaidi ili ziwe na viwango vizuri

5. SOURCE OF ENERGY
Incubators karibia zote zinatumia Umeme kama source namba one na jua, makaa yam awe au gas kama source namba mbili, ingawa zipo za mafuta ya taa pia kama source No 1

6. ALTENATIVE SOURCE OF ENERGY
Kila aina ya mtengenezaji ana source yake ya altenative energy, zipo za Gas, zipo za umeme jua na zipo za mvuke wa maji na zipo za mafuta ya taa, na zipo za makaa yam awe.

7. ALTENATIVE SOURCE NZURI
- Kwangu mimi Incubators ambazo altenative source of energy ni Mvuke wa maji nimetokea kuzipenda sana
- Hapa umeme ukikatika unaunga pipe kwenye Mashine na unakuwa na birika special na unaiweka jikoni maji yanachemka na mvuke unapita hadi kwenye incubators, ni source nzuri sana,
- Hata jua nayo ni source poa

ILA BADO SOURCE YA JUA AU GAS INAKUWA NI ALTENATIVE NZURI SANA.

MATATIZO YA INCUBATORS
Incubators nyingi zina shida moja kubwa sana, Incubators inaweza ikaharibika na wewe usiwe na habari kabisa na mpaka uje kushutuka ilisha haribu mayai yote na hilo ni tatizo kubwa sana,

MFANO:
-Heating tube zinaweza kufa na wewe usijue kabisa, na ukija shitikia ilisha haribu kila kitu
-Humidity Tube inaweza kufa na wewe usijue na ukija shitukia ni balaa
-Eggs turning inaweza kufa na usitambue hata siku mbili
- Humidity sensor na temperature sonsor zinaweza kufa na wewe usijue chochote
Na mara nyingi kinaweza kufeli kifaa kimoja za vingine viakendelea na kazi bila shida ila ikawa ndo kama hivyo, Mfano Mashine inaweza kuwa imekufa Humidity tube, na hapo inaweza endelea kufanya kazi na some time ni vigumu sana kugundua.
- Na tofauti na mitambo kama gari, Incunator inapo haribika huku ukiwa umeweka mayai ni balaa tupu, kama huna mashine nyingine ndo inakuwa imeharibu mayai yote.

KUKATIKA KWA UMEME- Endapo umeme utakatika na ukatumia Gas, au mafuta ya taa au makaa yam awe kama source nyingine ni lazima ugeuze mayai kwa mkono, na hapa tatizo liko kwamba ile mashine haiwezi kukubali kugeka ni lazima ubonyeze sehemu ya kubadilisha kutoka automatic kwenda manual. HAPA NDO HUWA KUNA KAZI PEVU

Na Mwisho ni kuhusu uendeshaji wa Incubators, Mara nyingi uendeshaji nao ni tatizo kubwa nasa hasa kwenye seting joto na humidity, make seting lazima zitofautiane kulingana na maeneo au vipindi Fulani, Joto na wakati wa Baridi kari
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom